Bajeti 2020/21 Watumishi wa Umma mwaka wa 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala punguzo la kodi

Bajeti 2020/21 Watumishi wa Umma mwaka wa 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala punguzo la kodi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Awamu ya tano imeonysha kuwa wafanyakazi sio tu hawamnyimi usingizi bali hata hawana maana kwake. Ukiondoa uvunjaji wa sheria aliofanya kupandisha mishahara na madaraja hata ahadi zake za kupunguza kodi (PAYE) kwa wafanyakazi hajajigusa.

Walidanganya uhakiki ndio kikwazo miaka mitano imepita.

Wakadanganya anajali wafanyakazi wa nchi hii lakini hajaonyesha jambo lolote juu ya kipato cha mafanyakazi zaidi ya kumnyonya kodi toka kwenye mshahara hadinkwenye manunuzi analipa kodi tu

Ni kwa miaka 5 ajira zimeporomoka katika kuajiri na sekta binafsi zikilia ukata.

Ila kaweza kujipitishia sheria ya kutoshitakuwa ndani ya siku 5.
 
Lah, sasa hii ndiyo ndoa ya kikiristo...Yaani mwaka wa saba ndala ni zilezile hadi zimetoboka kwa chini ..misigino minakanyaga lami..

Poleni watumishi wa umma...endeleeni kuvumia huenda neema ikafunguliwa hadi mkabakia midomo wazi! Mvumilivu hula mbivu...
 
Inafikia hatua mtu unachoka na haya malalamiko mitandaoni. Mnashindwa nini kuwaiga USA?
 
Jana nilikuwa napitia page za Raia wa Burundi wengi wanaonyesha kufurahia kifo cha Nkurunziza wengine wameenda mbali zaid nakusema azikwe kama ambavyo alikuwa akiwazika wapinzani na watu waliokuwa wakiikosoa Serikali.
 
Subirini pesa imepelekwa sehemu nyeti.
Unajua sehemu nyeti ni wapi?
SEHEMU NYETI NI KIKUNDI CHA KUSIFU NA KUABUDU ILI KUMWANDALIA NJIA MALAIKA
 
Mkapa hakuongeza mshahara lakini maisha ya wafanyakazi yalikuwaje, dawa si kuongeza mshahara bali ni kudhibiti mfumko wa bei leo hii mshahara ukiongezwa kila kitu kitapanda bei kuanzia daladala, kodi ya nyumba , chakula na vinginevyo inachotakiwa kufanya serikali ni kupunguza mfumko wa bei
 
Mtu haishi kwa mkate tuu, hivyo pamoja na kutoongezwa mishahara, lakini msiwe na hasira bali hapo tarehe 25 October,
unachukua...,
unaweka ...
Waaah...
P
brother mayala ebu tusaidie hiyo 170,000 to 270,000 ni nini na inaenda kwa tabaka lipi tu ajaribu kupitia kurasa za habari vyombo mbali mbali wanandika tu wana kosa udadisi kabisa kutafuta wataalamu kuwahoji na kutoa majibu ili jamii ielewe
 
Back
Top Bottom