Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

wapi ndama mutoto ya ng'ombe,wapi muzamir katunzi,wapi papa baghdad,wapi papa musofe,wapi chief kiumbe the big boss,wapi kimbau,wapi omary tall,wapi akayesu,wapi papa felician muta,wapi hasheem thabeet supa tolu,wapi muuza nyago na kavitz kako,magari yanayofaa kuwekwa hzo plate no customised ni hummer,vogue,benz v8 biturbo,phantom royce rolls,aston martin,buggati,limousine,jaguar,x5,lamborgine.

Usishangae unapita Moshi pale town unapishana na Stout au 109 imekula chapa ya kimario! Ha ha! Kitu Bedford au mbaula!
 
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?

Huu sasa ni usanii. Wangeweka bei kufuatana na herufi (characters). Hivyo, ingewekwa character iwe milioni 5. Wenye
majina kama MWAKASAFYUKA, wangeingizia taifa pato kubwa.
 
Kama lengo ni kuepusha nchi kuwa dampo la magari chakavu ni vyema pia tungekuwa na sheria ya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na magari bora barabarani kwa kuhakikisha magari yenye zaidi ya miaka 8 yanatozwa ada zaidi ili watanzania wasipende kununua magari yaliyokwisha tumika nchini na kuacha fikra za kufufua mikweche yao. Sawa watu wataagiza magari mapya na baadae yatakuwa chakavu je haya machakavu si yataendelea kuwapo barabarani au uchakavu wa Japani ni tofauti na wa Tanzania? Kwa wenzetu wanayo sheria ya kuyazuia magari chakavu kutembea barabarani je hiyo sheria kwetu ni hai?
 
Mie ninacikitika hapa uchakavu wameongeza na kuwa asilimia 20 toka asilimia 10 na wamepunguza miaka ya uchakavu.. toka miaka 10 mpaka minane.. Kazi kweli kweli.. Haya magari ya kuanzia 2005 ntaweza kununua mie..
 
Kama sikusikia vibaya, ukilipia hiyo, unajiachia kwa miaka mitatu baada ya hapo unalipia tena

ulipaji wake umekaaje wakuu.....? Je ukilipa kwa mara ya kwanza mil 5 utaendelea kulipa figure hiyo hiyo au itakuja kwenye rate ya kawaida?
 
Lazima ada iwe kubwa ili wachache na wenye uwezo ndio wanufaike...kimsingi si jambo lenye athari kwa wananchi,hata mamtoni ipo hivyo. Wenye uwezo waweke tu!

Hivi kweli nchi masikini na inayosindikiza nchi nyingine tunathubutu kuijilinganisha na mamtoni ni aibu,majengo yako kibao watu wanachukua kodi kubwa lakini hakuna kodi zinatozwa kwa ajili hiyo,cha ajabu wameshupalia wafanyakazi ambao kipato chao wengine kidogo mno inauma kwa kweli
 
kwa mfano mimi naimport kitu used toka brazil kwenye mambo yetu ya world cup 2014 nacho wananichaji uchakavu?maana naenda kuoa mie huko sasa vitu vingi nadhani vinakuwa tayari used!!!
 
Kwa kuwa bado mifumo yetu ya usimamizi bado siyo makini, ili kuepuka matatizo yote haya, sheria hiyo iseme moja kwa moja kuwa hakuna kuingiza gari ambayo ni zaidi ya miaka 8. Unajua kusema kuwa itatozwa tu kodi ya bidhaa haisadii, soko litajiadjust na magari ya yenye umri wa miaka 8 kuja chini bei zake zitakuwa juu zaidi, na zile za zamani kuwa more cheaper, kwa maana hiyo mtu akifanya uwiano anaona hata pamoja na hiyo 20% bado ni gharama nafuu kununua gari ya zamani kuliko ya chini ya miaka 8.

Huundio ukweli, hiyo sheria iseme moja kwa moja ie no more magari ya aina fulani ya chini ya miaka 8 kuingia nchini basi.

Hawawezi kutoa kauli ya namna hiyo hata mara moja.
 
Naomba kuuliza wadau, sasa ina maana ile tax calculator ya excel inayotolewa na TRA ndio haitumiki tena au inakuwaje?

Kwa anayejua naomba ufafanuzi.

Nami ningependa kujua hilo, je hizi NYENZO FEKI zao hazitumiki tena? ingawa [TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]zilisaidia kidooogo ......Valuation Calculator for Used Motor vehicles and CRSP List [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
nakuunga mkono aslimia mia moja!yapo magari ya miaka ya nyuma imara mno na sio makaratasi kama ya sasa.kuchakaa kwa gari ni kutumika kwake,yaani kama limetembea kilometa nyingi.

Watanzania mmezowea kuweka makorokoro, hata makopo matupu ya Lactogen kuna watu mpaka leo wanayo.
 
Hii bajeti ni ya kumsaidia mlalahoi au kumkandamiza?

Kila juhudi zinafanyika waliobaki kwenye ulala hoi waondoke huko na wawe walala hai.

Bahati nzuri mimi nilizaliwa kwenye ulala heri na bado nadunda hukohuko.
 
Millioni 5? Hapa Maryland tags maalumu unalipa dola 50 tu.

Mkuu usilinganishe Us na hapa.. hapa watu wana hela za kupiga wananchi wenzao(ufisadi). hamna mtu anayetafuta hela yake kwa uhalali ataenda kuiweka kwenye hizo tags... hujasikia bilioni kadhaa za safari ya mkuu zimepigwa? ndio tanzania yetu hiyo
 
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?
mkuu kumbuka ni kila baada ya miaka mitatu na si kila mwaka unalipa iyo million tatu..then kama unaona nyingi si lazima kuweka maana ni kitendo cha hiari tu
Lakini sio unacolora yako unaweka jina aisee utachekeshaa
 
Nimelifikiria hili, nikaona eidha serikali haitaki watu wawe na namba binafsi, au hawajui maana ya namba binafsi. Mtu yeyote mwenye akili ya kiuongozi (nina shaka sana na hili juu ya wengi wa viongozi wetu) angeweza hata kuulizia viwango vinavyotozwa katika nchi nyingine ambako wana utaratibu huu, hata hapa jirani South Africa. Angalia kwamba tozo waliloweka ni zaidi hata ya depreciation ya gari kila mwaka. Nani atataka kulipia Tshs 5M ya namba hata kwa gari ya thamani ya Tshs 10/- ? Sasa jiulize, watu waliofanya uamuzi huu wana uwezo wa kufikiri kweli? Au wanataka kina Ridhiwani na Rostam tu ndio wawe na hizi namba.

Na suala la kusema kuanzia sasa gari zaidi ya miaka 8 ushuru unaongezeka zaidi kwa asilimia 20. Nilishasema awali, hii ni sawa na kusema walala hoi mnatutia kero barabarani na Corola au Noah zenu. Sasa tunawazuia kuziagiza.

Utawekaje sheria kama hii wakati nchi haina viwanda vya magari? Suala la mazingira ni kisingizio tu. Tuambieni wazi kwamba serikali haiko tayari kutafuta suluhisho linalofaa kupunguza magari Dar es Salaam, na wanachukua njia ya mkato kuzuia watu wa kipato cha kawaida kununua magari.
 
Back
Top Bottom