Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Huo ni mkakati wa serikali kujiongezea mapato na wala sio kwa ajili ya watu kujionesha kuw wanapesa...

Hii inatupeleka kwenye swali la ziada; ni kweli mtu anayelipa 5m kwa ajili ya plate number analipa kodi ya mapato halali kweli?
 
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?
Gari yenyewe Corolla ya mil 7, na umejipinda pinda hadi ukanunua, registration ya mil 5 ya nini?
Kiwese chenyewe waweka shil 10 elf kila ukifika sheli, watanzania tuache matanuzi.

Hao wa kuweka namba maalum ni wale wa mashangingi ya milioni 200-500, kwao mil 5 ni vijisenti!
 
Hii safi sana lazima nitafuta kamkweche cha kama milioni 4 kisha naweka namba ya millioni 5, lazima wabongo washike vichwa mwaka huu.
 
Aaaaaa 5 mil ni three much tena! Ka plate namba chenye jina lako tu? Its just an identity the same as numbers! 5 mil ni nyingi sana ata kama ni kwa kuuza sura
Mbona wacheza kamari wanatumia zaidi ya hiyo 5m tena kwa siku? Sio lazima kuweka jina lako kwa plate number, by the way gari si linabaki kuwa lako.
 
Nadhan hii ni poor Thinking!! Hivi hii Nchi haina wachumi? Inakuwaje uanzishe kitu kipya for such High Tax rate? Mimi nilitegemea kama wangekuwa na uelewa mzuri wangeanzisha kitu kama Hiyo ila kwa Kiwango cha TZS labda 900,000 kwa Two years then watu wakiwa wengi Unapandisha kwani watu waliokwisha Ingia Wataona Noma Kutoka kwani wataonekana wamefilisika!! Just simple PHYSICS IN ECONOMICS!!
 
Kwenye special number plates mi naona ni sawa tu; tena wangeweka kuanzia 10M, ndiyo maana ya kuwa "special", nyie mnataka muwe special kwa laki? acheni masihara bana!
Weka bei kubwa ili wenye ziada wachangie pato la serikali!
 
Mh. Waziri wa fedha amemaliza kuwasilisha bajeti moja ya kitu kipya ni usajili wa magari kwa namba maalum (ie jina lako)unalipa mill 5, Great Thinkers nini mtazamo wako, je ni kuaisha wenye uwezo waonekane hata katika plate namba za magari yao au lengo ni kukuza mapato ya serikali bila kuangalia mitazamo ya kijamii.

Ni magari binafsi tu au na yale ya biashara?
 
Nadhan hii ni poor Thinking!! Hivi hii Nchi haina wachumi? Inakuwaje uanzishe kitu kipya for such High Tax rate? Mimi nilitegemea kama wangekuwa na uelewa mzuri wangeanzisha kitu kama Hiyo ila kwa Kiwango cha TZS labda 900,000 kwa Two years then watu wakiwa wengi Unapandisha kwani watu waliokwisha Ingia Wataona Noma Kutoka kwani wataonekana wamefilisika!! Just simple PHYSICS IN ECONOMICS!!

Unaelewa unachozungumzia lakini mkuu? special number si kwa wengi, si kwa kila mtu, hiyo ni luxury tu haina umuhimu wowote, wewe unayelialia na hiyo M5 utashangaa special number kibao barabarani-hao ndiyo wanastahili!
 
Hivi kweli nchi masikini na inayosindikiza nchi nyingine tunathubutu kuijilinganisha na mamtoni ni aibu,majengo yako kibao watu wanachukua kodi kubwa lakini hakuna kodi zinatozwa kwa ajili hiyo,cha ajabu wameshupalia wafanyakazi ambao kipato chao wengine kidogo mno inauma kwa kweli

Vipi mkuu, unataka wapunguze kiwango ili na wewe mfanyakazi uweze kuaford special number? .....hahahaaa!
 
Nadhani itakuwa na mtundo wa T Synthesizer 1. Ukiwa na gari ya pili T Synthesizer 2

Au pia wakaamua T1 Synthesizer na gari ya pili T2 Synthesizer

Ila huwa kuna sheria kwamba idadi ya digits isizidi kiasi fulani, sasa yale majina kama Rugamaikamuwaitu au Mwakisakagafijo inabidi tu ufupishe!
 
Kwa nini iwe 5m na siyo 1m au hata 500K? Plate kuwa na jina binafsi kuna gharama gani za ziada kwa serikali? Nafikiri serikali inaweza kupata mapato mengi kwa kuwapa hao wapenda sifa rate ambayo wanaweza kuimudu bila ya kuwakomoa.

kwa mfano: kama rate ni 500k na serikali ikapata wapenda sifa 1000 mapato ni 500m. Lakini rate ikibaki 5m na wauza sura ni 20 mapato ni 100m.
 
Hapo umenena mkuu! ku-define uchakavu wa gari kwa kuangalia year of manufacture is not correct at all, though nakubaliana kwa namna fulani kutumia kigezo cha mileage coz at least it gives sense! gari inaweza ikawa imenunuliwa recently lakini ndani ya muda mfupi ikawa imetembea mileage nyingi kuliko iliyonunuliwa zamani na hii inatokana na matumizi ya gari, na mileage ndo kigezo cha ubora au ukuukuu wa gari ambacho wateja hupenda kuzingatia.

Pamoja na ukweli huo, serikali inatakiwa kufahamu kuwa wanunuzi wa magari yaliyotumika ni watu wa kima cha chini ambao uwezo wao haufikii kule wanakofikia wenye pesa kununua magari mapya na ya miaka ya karibuni. Kwa mtindo huu ni kuzidi mumwumiza mnyonge ambaye anatafuta njia ya kujikwamua kutoka umaskini. Sijaona mataifa ya ulaya kudai kodi ya namna hiyo, nilipoona mara ya kwanza bongo nilishangaa. Badala ya kutoza kodi nyumba za kupangisha zinazomilikiwa na vigogo wao wanatoza kodi kubwa magari ambayo ni aseti ambayo muda wo wote inaweza kufa bila habari.

Serikali inatakiwa kufanya ubunifu wa kodi za magari kwa kufanya registration ya kila mwaka badala ya kuunganisha registration mara moja tu kwa maisha. Magari mengi yalivyozagaa Tanzania kwa kuanzisha mpango huo ni source kubwa sana ya kupata pesa kila mwaka. Eneo jingine la kupata pesa kwenye magari ni kuanzisha computerized system ya kukagua magari ambayo kabla ya kupata registration lazima ikaguliwe kupata kibali cha ku-renew registration. Hii ikifanyika kila mwaka ni eneo zuri sasa la kuchuma pesa kuliko kupandisha kodi ya kuingiza magari kwa wakati mmoja na kuendelea kuwatesa wanywa soda na bia bei ya juu na joto lote la dar na kweningeko. Ubunifu umetushinda kila kona na kinachofanyika ni kuwanyonga walalahoi na wenye nazo wanaendelea kudesa tui.
 
Nadhan hii ni poor Thinking!! Hivi hii Nchi haina wachumi? Inakuwaje uanzishe kitu kipya for such High Tax rate? Mimi nilitegemea kama wangekuwa na uelewa mzuri wangeanzisha kitu kama Hiyo ila kwa Kiwango cha TZS labda 900,000 kwa Two years then watu wakiwa wengi Unapandisha kwani watu waliokwisha Ingia Wataona Noma Kutoka kwani wataonekana wamefilisika!! Just simple PHYSICS IN ECONOMICS!!

Absolutely right. Kwa kweli hii nchi ina matatizo zaidi, yaani wachumi wote hawa ndo wameshindwa kung'amua ujinga hu; hivi wanadhani private plate number ni nini hasa. Huu ni ujinga uliotukuka, kama wangelikuwa makini katika hili wangelipata mapato makubwa sana lakini kwa hali hii, sidhani.
 
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?

Njoka Ereguu,

Nakushauri uwe unaangalia angalau TV , huyu Mgimwa na Comissioner wa Budget sijui wamechoka na maisha. Huko Kenya walianzisha mtindo aw matajiri haswa wanamichezo kuandika majina yao kwenye namba plate Kama show biz lakini serikali ya Kenya imepiga marufuku. Sasa nashangaa hawa mbuzi wa Iringa wanataka kutumia Kama chanzo cha mapato. Hivi ni wanyalukolo wangapi wanaweka hizo ante na how much is Mgimwa expecting to get into gvt coffers from this joke!

Huyo Kitilya wa TRA choka mbaya. Hivi caucus ya CCM inafanya nini. Last time Makamba alikuwa na Wazo la kurudisha Rent Restriction Act iliyofutwa na fisadi Mkapa lakini Tibaijuka akamponda and they never saw light at the end of the tunnel.

Makamba Jnr had something big. Sasa nadhani Mgimwa angekuwa na akili ya kwenda Makambako angebuni kodi kutoka kwenye Majengo yote based on the use of the buildings na sio ile property tax ambayo kwa sheria ya 1992 iliyopo hata hiyo haikusanywi. Kama pesa za kodi za Nyumba zingetozwa kodi hata kwa miajiji ya Mbeya, Mwanza, Arusha na Dar es salaam hakuna haja ya kuomba pesa 2 trillion from what they call development partners.

Huna haja ya kwenda Shula ikawa tunao watu wanaopaswa kulipa kodi wasiopungua milioni 15 ili hali wanalipa wasozidi milioni 1 na nusu . I would strongly advise CCM kurudisha kodi ya kichwa iliyofutwa na TANU 1966 or 1967 sikumbuki vizuri hata kwa Kiwango cha kukisia cha Usd 30 or let us say 50,000 per annum for everybody above 18 years excluding students , the aged over retirement age 50 years for wakulima and 60 for wafanyakazi and the disabled or medically unfit tungekusanya kodi ya kututoa hapa tulipo.

Tabia ya kusamehewa kodi kwa sababu tu ya kipato ife kuanzia Leo. Kila mtu alive has to pay tax. Nchi zote zilizoendelea zimefanikiwa kwa watu kulipa kodi. Wagiriki walifanya mchezo na kodi they are the highest tax evaders in Europe ona sasa imekula kwao. Mwambie JK wawekezaji create capital fight with our weak financia controls. Kilmo should be left to the wananchi hao wawekezaji wakubwa ni ndoto ya mchana tuna mashamba ya maua kule Arusha na Yule aliyepewa mbarali just take stock audit and let have the faida in public hata akina Mohamed enterprises waliopewa mashamba ya Mkonge whoa is the out come. Fanyeni utafiti kwanza.

CCM hakuna kodi ambayo sio kero kwa mlipaji. What you have to do mis to widen the tax base and lower the rate compliance is a default. Wacheni Tabia ya kuongeza rates inaongeza ukwepaji na matatizo yanaanzia hapo.
 
Mh. Waziri wa fedha amemaliza kuwasilisha bajeti moja ya kitu kipya ni usajili wa magari kwa namba maalum (ie jina lako)unalipa mill 5, Great Thinkers nini mtazamo wako, je ni kuaisha wenye uwezo waonekane hata katika plate namba za magari yao au lengo ni kukuza mapato ya serikali bila kuangalia mitazamo ya kijamii.
Hii ni sawa kabisa kwa sababu ni njia mojawapo ya kupanua pamoja na kubuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato na hii mtu wa kawaida haimpasi kuilaalamikia kwa hali yeyote kwa sababu haimathiri kimapato kwa njia yeyote na kusema kuwa ni kuwapa mafisadi namna ya kutamba na pesa zao.

N fikra finyu maana kama ni gari tayari analo na hata kama hanalo elewa ya kuwa anao uwezo wa kulinunua akilipa milioni tano kwa ajili ya plate namba amenunua hiyo bidhaa ama huduma kutoka kwenye kituo chetu mimi na wewe cha mauzo hivyo amechangia mfuko wetu wa hazina na asiponunua basi atanunua kutoka kwenye gharama ya shuruti ambayo ni kulipa gharama ya kawaida kisheria ambayo hata m2 mwenye uwezo wa kawaida analipa ili mradi tu kwamba anamiliki gari.

Kwa hili nawasifu lakini nafikiri walipaswa kufikiri na kuangalia tena sekta nyingine kama madini, vitalu vya uwindaji na sehemu kama hizo ili kupanua wigo zaidi...
 
Tanzania sio Kenya wala kuweka plate namba majina sio kama Tanzania wanaanza mbona huu utaratibu upo siku nyingi tu Tanzania, sehemu kubwa ya dunia huu utaratibu upo.
 
Flamboyant life style among the poor will ignite like fuel....let them burn with their names on the plate numbers.....Mgimwa God's willing you will be burnt too.
 
Back
Top Bottom