Tetesi: Bajeti kuu ya Serikali haiwezi kupitishwa bila Wabunge wa Upinzani kuwemo. Tutegemee tamko baada ya kura


Hahaha aisee mnatumia nguvu kubwa kutaka kuhalalisha kila kitu

Wale bado wapo na watakuwepo mpaka 2025, hayo mengine ni porojo tu
 
Kumbe ndio maana Covid 19 hawawezi kuondolewa kabla ya kura hiyo kupigwa vinginevyo mchakato wa kupitisha bajeti utakwama!. Umenifungua macho Mkuu!
 
Waendelee kuvunja katiba na sheria kisa budget?
 
Waendelee kuvunja katiba na sheria kisa budget?
 
Tangu lini Chadema iliwahi kupitisha bajeti ya serikali, na walivyokuwa wanatoka nje ya bunge je bunge lilihairishwa?

Yani katika Wahehe wajinga wa kwanza ni Yericko Nyerere wewe unafuatia.

Ww ndo hauna akili,walikuwa wanatoka nje lakini si walikuwa still ni wa Bunge wa upinzani,na si walikuwa wanapokea na mshahara wa mwezi huo waliogoma wakati wa kupitisha bajeti,na si walikuwa wanarudi kuendelea kupokea posho na mishara mingine?.
 
Hao ni wabunge halali hadi pale Spika Tulia ataka vyotangaza vinginevyo

Maombi ya kuwashtaki chadema ndo yanakasoro sio kwamba wameshindwa kesii....hii nchi mbona tunakalia umbea tu bila kuumiza kichwa kwa kufatilia hii kesi ndogo hivi?
 
Hebu wale mnaopenda kutumia vichwa vyenu kufikiri mshirikiane na mimi kufikiri: Tuchukue kwa mfano; kiongozi mkuu wa dini moja yenye waumini wengi nchini anapata madaraka hayo kwa kuwaua wote waliokuwa wanapinga yeye kuwa Kiongozi mkuu wa dini husika. Kisha baada ya kufanikiwa kuwa Kiongozi analetewa majina 9 ya ya wasaidizi wake yenye mashtaka na ushahidi kuwa wameteuliwa kuwa wasaidizi kwa kuwahonga wateuzi wao! Huyu Kiongozi mkuu atapata ujasiri wapi wa kuwafukuza hawa waliohonga kuja kumsaidia kueneza dini ya huyo kiongozi muuwaji!? Yale maelezo ya "La kuvunda halina ubani" si ndiyo haya? Kwa nini mnapoteza muda wenu na wetu kwenye uozo huu?

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Kuna nyakati unakuwaga na mitazamo iliyojaa busara, hekima kama mwenye jina lako. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…