Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Just to annouce the Stimulus Package

Hii Stimulus Package ya JK Itabidi tuianzishie thread yake, tuone in and out yake....to me imekaa ki EPA EPA tu...tena with 2010 mlangoni.....?????
 
Jamani wabunge, nyie ndio mliobaki kuliokoa taifa kwenye huu wizi wa mchana.

Stimulus package hela za serikali haziendi bure kwani hata hizo hela IMF walizoleta ni mkopo.

Serikali ikilipa madeni ya vyama vya ushirika na hayo makampuni makubwa ya kununua pamba, kahawa ya kina ELna RA lazima serikali ipate stake ya ownership kama ambavyo US govt imepata kwenye GM, AIG na kila sehemu hela za serikali zilipoenda.

Hayo makampuni yakipata faida uko mbeleni yanalipa hela back na stake inarudishwa.

Otherwise huu utakuwa usanii wa kusaidia wafanyabiashara wachache ambao wakipata faida wanakula, wakipata hasara serikali inawapa hela za bure.

Halafu lazima transparency ya hali ya juu iwepo, ili serikali itangaze imetoa hela kiasi gani kwa kila kampuni kwa majina ili wabunge na wananchi tuweze kuhakikisha hayo makampuni yapo na uko mbeleni yanalipa hizo hela sio usanii kama wa EPA hatujui nani karudisha hela wala nini.

Sasa wale wakulima kule Vijijini waliolima kahawa, mahindi, maharage wao watafidiwa vipi na hasara walizopata???

Moelex23,

Niko nyuma yako. Mimi sikupata nafasi ya kuisikiliza hiyo hotuba lakini kama ulivyosema ni lazima iwekwe wazi ni kiasi gani kimetolewa kwa kila kampuni na
na kuwe na uhakika na uwepo wa hizo kampuni na mikakati ya jinsi na namna ya kufanya monitoring ili kuhakikisha kwamba pesa hizo zinarudishwa at a later stage. Mimi ningependekeza iundwe kamati huru ya bunge kwa ajili ya kusimamia matumizi ya hii package la sivyo itakuwa njia rahisi kutoa pesa kwa makampuni hewa ili zisaidie kununua kadi za kupigia kula, kupika pilau na soda kwa wapiga kura na hatimae wapate ushindi wa kishindo!!!!!

Tiba
 
Kwa mtazamo wangu, hotuba hii ni nzuri kuliko nyingi alizowahi kuzitoa. Uzuri wake utatimia kama mipango aliyoizungumzia itatekelezwa kwa uadilifu. La sivyo, pesa nyingi itapotea, na wakulima/kampuni zinazokusudiwa kufaidika na pesa hizo kukosa pesa kama inavyokusudiwa. Hiyo ikitokea, madhara yatakuwa ni makubwa zaidi.

Tatizo dogo ninaloliona kwenye hotuba hii ni;

1. Serikali tayari ina deficit katika bajeti yake kutokana na mapato iliyotegemea. Kwa mujibu wa Rais, kuna deficit ya zaidi ya 4bil. Je, watawezaje kukamilisha mipango iliyowekwa wakati tayari wana deficit hiyo?
2. Rais amezungumzia kimzaha kidogo kuhusu mabenki kushindwa kutoa mikopo kwa viongozi watakaoiomba. Je, malengo ya pesa hizo yanasukumwa na viongozi wanaoshughulika na biashara za mazao?
3. Makisio ya mtikisiko wa uchumi ni miaka miwili. Je, serikali inaweza kuhakikisha kuwa mipango hii itadumu na kukwepa balaa linaloweza kujitokeza endapo baada ya muda huo uchumi utakuwa bado haujatengemaa?
4. Sijasikia mipango ya serikali katika kuchukua hatua za kurekebisha hali ya uchumi kwa kutafuta njia mbadala za kukuza uchumi. Je, serikali inategemea kuendelea kufanya yale yale (kama alivyosema kwenye mkutano na IMF - Dar) bila kuangalia fursa nyingine za kukuza uchumi hasa katika kipindi hiki?

Naamini kuwa ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua ya kuokoa hali ya kiuchumi nchini. Jukumu hilo halina mwingine wakulifanya zaidi ya serikali yenyewe. Hatua alizoainisha Rais ni za muhimu sana hasa wakati huu.
 
Tatizo dogo ninaloliona kwenye hotuba hii ni;

1. Serikali tayari ina deficit katika bajeti yake kutokana na mapato iliyotegemea. Kwa mujibu wa Rais, kuna deficit ya zaidi ya 4bil. Je, watawezaje kukamilisha mipango iliyowekwa wakati tayari wana deficit hiyo?

Mkuu Recta,

Only 4bil....deficit? Hawa watu hawako serious kabisa......wangekuwa serious na mipango yao pia wawe na political will yakuitekeleza mipngo hiyo, I believe hii deficit hawangekuwa nayo kabisa!

4bil inatosha kuwaoffset na tena with big surplus kama ile pesa ya Twin towers ingekuwa managed vizuri.....kwanza gharama ya misafara ya rais pekee yake kwa mwaka itakuwa ni more that hiyo 4bil.....bado hujaangalia viongozi wengine.....then anakuja oooh kuna upungufu.....didn't they know kwamba mismanagement ya funds za walipa kodi ingepelekea huko?
 
stimulus plan ndo imesha tangazwa... Hapa sisi tutaijadilia,kuikosoa,kuipinga.. lakini ndo hivyo.. tutaishia hapa kwenye JF.. thread itapita na wakati thread mpya iatakuja.. tuatafanya the same thing... mi ningeomba tuwe tunafanya review kila baada ya mda fulani tuone kama kujadilia humu kwenye JF kuna impact gani kwenye nchi au jamii.. kunamabdiliko yoyote either directly au indirectly kwenye jamii tangu tuanze kuchangia mada humu...
watu wenye nguvu ya kupresha serikali ni Viombo vya habari.. hivi fikiria jinsi magazeti ya udaku yanavyo waandama wasananiii.. yanawandaa mpaka basi.. sasa vyombo vya habari vingekuwa vinaandamaa serikali.. wangekuwa ina demand transparency katika mipango yote iliyotangazwa na hela zitakavyotolewa.. serikali inajua kabisa kama sisi wengine ni wakubwabwaja tu.. hatuna effect.. ndo mana wametuacha hapa tunatawala huu uwanja... watakapo ona sasa tunaanza kuleta cheche.. utaona zengwe....
 
Nchi iko kwenye shida hata kabla ya huu mtikisiko wa uchumi wa Tanzania.
Mara ya kwanza JK mwenyewe alitamka kwamba mtikisiko huo hautatugusa sisi.
Leo anakuja na story hiyo kesho atakuja na story ya kupanda bei ya mafuta. Kesho kutwa atakuja na story ya kukosekana chakula duniani. Baadaye atakuja na story ya mafua ya nguruwe na ndege. Always he will be coming with strange stories that has no end.
Mbona hii ya shida katika uchumi ni kawaida kwa Tanzania! Kama na stimulas package then tuliihitaji miaka mingi iliyopita maana uchumi wetu umeyumba miaka mingi. Lakini at that time we were told that tuko katika soko huria. Sijui katika soko huria serikali haihusiki, hivi uchumi huwa unajijenga? Yale yale ya maisha bora kwa kila mdanganyika na wadanganyika wakapiga makofi ya matumaini. Nina haki zote za kupuuza upuuzi huu. Maana hauna msaada wowote katika maisha yangu binafsi.
Haya bwana ili mradi kunakucha na napata ugali wa muogo kila leo. Nawaachia wadanganyika tena wengine wasomi muendelee kudanganyika.
 
Nchi iko kwenye shida hata kabla ya huu mtikisiko wa uchumi wa Tanzania.
Mara ya kwanza JK mwenyewe alitamka kwamba mtikisiko huo hautatugusa sisi.
Leo anakuja na story hiyo kesho atakuja na story ya kupanda bei ya mafuta. Kesho kutwa atakuja na story ya kukosekana chakula duniani. Baadaye atakuja na story ya mafua ya nguruwe na ndege. Always he will be coming with strange stories that has no end.
Mbona hii ya shida katika uchumi ni kawaida kwa Tanzania! Kama na stimulas package then tuliihitaji miaka mingi iliyopita maana uchumi wetu umeyumba miaka mingi. Lakini at that time we were told that tuko katika soko huria. Sijui katika soko huria serikali haihusiki, hivi uchumi huwa unajijenga? Yale yale ya maisha bora kwa kila mdanganyika na wadanganyika wakapiga makofi ya matumaini. Nina haki zote za kupuuza upuuzi huu. Maana hauna msaada wowote katika maisha yangu binafsi.
Haya bwana ili mradi kunakucha na napata ugali wa muogo kila leo. Nawaachia wadanganyika tena wengine wasomi muendelee kudanganyika.
ni kweli kabisa.. unajua the biggest problem of Tanzanian Viongozi hasa Maraisi (cjui sehemu nyngine Afrika lakini nadhani wote sawa) wana mipango na plans za kusustain mda wao wa uongozi.. kwahiyo hawana Longterm plans za kuendeleza nchi kabisa... wao ni ilani ya chama watahihutubia..
inakera sana unaona sasa hata ukichangia na kulalamika hakuna chochote kinachofanyika.. bora tunyamaze na sisi tujitahidi kuingia huko anagalau hata tupate chakubangaiza... hii vita ya ufisadi its a cherade.. wengi tunajua kama tukipewa nafasi basi na sisi tunakuwa humo humo.. njaa kali unafanya mchezo..
 
Kama hizi pesa tayari ziko kwenye bajeti, na mipango aliyoianisha tayari imo kwenye bajetu (thus the money), kulikuwa na ulazima gani wa kutoa hotuba hii? maana Kesho Waziri wa Fedha naye atarudia yale yale, ama sivyo? Na baadaye mawaziri watafafanua kwa undani kitu kile kile. Why the speech?

Du! Kumbe kwenye mambo mengine mkuu wewe ni mweupe sana?

Yaani huoni kwamba dhani yenyewe na jambo lenyewe lilistahili ku-be-addressed lenyewe bila kuchanganywa na issue ya bajeti?

Naomba nikuulize tangu lini zaidi ya miaka ya 70 ni mwaka gani tena dunia ilikubwa na mtikisiko kama huu?

Unataka kutuambia rahisi ameongelea mambo ya kawaida ya kila siku...

Kama sisi ni wazalendo... ni vyema kuchukua mambo kama ya kweli machungu kama yalivyo.

Mimi nadhani tungemsaidia rais kwa kumwambia serikali yake iendelee kupunguza matumizi... badala ya kubeza hali ambayo ni mbaya kwetu tayar.
 
(i) Kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao msimu wa 2008/09
Serikali imeamua kufidia vyama vya ushirika na makampuni yaliyonunua mazao ya wakulima na kuyauza kwa hasara. Hasara hiyo inayokisiwa kufikia shilingi 21.9 bilioni imepatikana kutokana na bei ya kuuzia mazao hayo kuwa chini sana ya gharama iliyotumika kuyanunua. Serikali italipa madeni yenye thamani ya hasara hiyo, moja kwa moja kwa mabenki yaliyokopesha vyama na makampuni hayo.
wakulima kila siku wanazulumiwa na wafanyabiashara serikali haiingili kati leo hii serikali inaenda kulipa madeni ambayo chanzo chake ni utata
je nani anawatetea wakulima wadogo

Tumekubaliana pia katika mkakati huu, kuwa lazima kuhakikisha kuwa utulivu wa uchumi unakuwepo ili kuhimiza ukuaji endelevu wa uchumi na kuvutia sekta binafsi kushiriki. Vilevile tuongeze kasi ya kuharakisha uimarishaji wa TIB na uanzishwaji wa Agricultural Development Bank.
kwani TIB hawawezi ku invest kwenye agriculture , kuna umuhimu gani wa kuanzisha benki nyingine tofauti
bank kubwa duniani zina kila kitu under one umbrella ie barclays( barclaycard, barclay capital et al )

kitu kipya kwenye hotuba ni - 2010 ALL EYES ON TIB
 
Hii Stimulus Package ya JK Itabidi tuianzishie thread yake, tuone in and out yake....to me imekaa ki EPA EPA tu...tena with 2010 mlangoni.....?????

Ninakubaliana na wewe. This is another EPA in the making! Ni ngumu kuamini kuwa hii "stimulus package" itatumika ipasavyo.
 
Kama hizi pesa tayari ziko kwenye bajeti, na mipango aliyoianisha tayari imo kwenye bajetu (thus the money), kulikuwa na ulazima gani wa kutoa hotuba hii? maana Kesho Waziri wa Fedha naye atarudia yale yale, ama sivyo? Na baadaye mawaziri watafafanua kwa undani kitu kile kile. Why the speech?

We hujui mambo ya PR na kutaka kuonekana kinara tu wakati hamna chochote.
 
Prevention is better than cure.

Kuna makampuni 24 yametwajwa kuwa ni makampuni makubwa yanayofanya biashara ya kahawa nchini. Kama kuna aliye na list ya makampuni hayo ni vyema aiweke hapa ili tuanze mapema kufuatilia wamiliki wake etc.
Tusingoje mpaka ufisadi ufanyike, tuzuie usifanyike. Na hii hotuba imekuwa wazi kwa kiwango kikubwa so ni rahisi kufuatilia pesa zinavyogawanywa.
 
Kuna tofauti gani kati ya mpango huu wa Kikwete na serikali yake na mpango wa Obama na serikali yake?
Mwakjj,
Tofauti moja kubwa ni kwamba serikali ya Obama inaaminika. Sijui kama unaweza kusema hivyo kuhusu serikali ya Kikwete. BTW Susuviri yuko wapi?
 
Wachumi maswali yangu niliyowauliza alasiri siyaoni hivyo nayauliza tena mnisaidie:

1. Hizo hela tutakazotumia kuchochea uchumi ni MSAADA au MKOPO kutoka Benki ya Dunia na Fuko la Fedha la Kimataifa? Kama ni MKOPO je RIBA ni asilimia ngapi na MKATABA wa MKOPO una masharti au makubaliano gani?
2. Huo mrahaba/mrabaha wanaopewa likizo ya kutoulipa ni kina nani hasa - wawekezaji wakubwa au wachimbaji wadogo wadogo wa madini? Na kama ni wachimbaji wadogo, kwani walikuwa wanaulipa hapo kabla?
3. Hii DHAMANA ambayo Serikali itaitoa kama MDHAMANI inamaanisha kuwa wanaodhaminiwa wakishindwa kulipa basi hiyo dhamana inafilisiwa? Na kama ni hivyo Serikali imejiandaa vipi na uwezekano huo wa kufilisiwa?
 
Kama hizi pesa tayari ziko kwenye bajeti, na mipango aliyoianisha tayari imo kwenye bajetu (thus the money), kulikuwa na ulazima gani wa kutoa hotuba hii? maana Kesho Waziri wa Fedha naye atarudia yale yale, ama sivyo? Na baadaye mawaziri watafafanua kwa undani kitu kile kile. Why the speech?

Halafu baadaye watapanga safari za mawaziri kuzunguka mikoa kupromote bajeti. Mwendo mdundo!
 
Baada ya kuipitia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, nimeona kuna haja ya kuanzisha mjadala maalum wenye lengo la kuhakikisha mkakati huo hautumiwi vibaya na wachache wabinafsi.
Ni bayana kuwa kuna watakaonufaika zaidi na mkakati huu ambao umedhamiria kulinufaisha taifa zima. Kunufaika kwao zaidi ni jambo jema iwapo tu hakutaathiri kunufaika kwa taifa kiujumla.
Hivyo basi nakaribisha michango yenu juu ya mianya yoyote inayoweza kutumiwa na wabinafsi kujinufaisha na pesa zitakazotolewa huku wakiacha uchumi wa taifa ukitetereka.
Kwa kuanzia tu nadhani kuna umuhimu wa kuyajua kwa ukaribu makampuni 24 yaliyotajwa kuwa ndio makampuni makubwa yanayofanya biashara ya kahawa nchini.
Karibuni.
 
bla bla bla mpaka 2010!!!! mie naona nafuu kabisa kama hizi hotuba zisingekuwepo tunapotezena muda wafanye vile wanataka mbona wanafanya vile wanataka waendelee tuuuuuuuuuuu mpaka liamba.Nonsense
 
Naomba waungwana mnisaidie JK alikuwa anamaanisha nini aliposema, "Tuliyaweza yale naamini na haya tutayamudu!" Ni yapi haswa ambayo serikali yake iliyaweza ? Je alimaanisha kauli mbiu ya kampeni yake "Maisha bora kwa kila mtanzania."
 
Kiunagaubaga...
Kutokana na sababu hii, Serikali ya Tanzania imeunda Kikosi kazi cha kuangalia njia na namna ya kukabiliana na athari zinazotokana na msukosuko wa masoko ya fedha pamoja na kuporomoka kwa uchumi duniani kwa uchumi wa Tanzania.

Enhe..🙄


Ili kutekeleza kazi yake serikali imekipa kikosi kazi majukumu yafuatayo: (i) Kufanya uchambuzi kuhusu hali halisi ya madhara yatakayotokana na msukosuko wa masoko ya fedha pamoja na kuporomoka kwa uchumi wa dunia kwa uchumi wa Tanzania
(ii) Kushauri,kwa kuzingatia uchambuzi wa hali ya uchumi, hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari za msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na
(iii) Kuchunguza fursa zinazotokana na msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na jinsi ambavyo Tanzania inaweza kufaidika na fursa hizo ili uchumi ubaki imara na kukua zaidi.
Ripoti hii inajumuisha uchambuzi wa athari za msukosuko kwenye sekta mbalimbali, mapendekezo ya hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari hizo na inabainisha fursa mbalimbali zinazotokana na msukosuko huo.

Hiki Kikosi ni Kina nani? IMF?😱
ATHARI ZA MSUKOSUKO
Siombei hii lakini kunyesha misukosuko kana ya JF VIlle...nimebandika hii kutoka kwenye thread ile...View attachment Wee Simama_Fisadi_ WE!.bmp Tuendelee hapa chini...

Mapendekezo Yanayohitaji Kutengewa Fedha
NAMNA YA KUGHARIMIA MPANGO HUU


Jedwali Na. 10 linaonyesha gharama za kutekeleza mpango huu na vyanzo vya kulipia gharama hizi.

4.1. Serikali kukopa ndani ili kutekeleza bajeti yake

Sikujua 'Sirikali' yetu yaweza kujikopa😉tena ndani, Bank M?🙄


Sielewi kama hiyo hapo juu ndio ripoti yenyewe-ad-hoc
Je Ripoti hii ndio ilinukuliwa?😀

Inavyoonyesha kipande hicho ni-kuwa Kikosi kimeshafanya kazi, sasa kuna haja gani ya kuunda Kikosi kingine?😱😱



😛😉🙄😱😀😀😎
Nasubiria Kipande kingine...usibishe hodiZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
 
Kuna tofauti gani kati ya mpango huu wa Kikwete na serikali yake na mpango wa Obama na serikali yake?

Wao wana "Economic Stimulus Package" which is a Keynessian tool to stimulate the economy by using government spending, might be a bit liberal, but their size of economy can afford it, actually it is more like cannot afford not to do it than can afford it.Sisi tuna "pure unadulterated and unplanned government overborrowing and overspending" which would do insult to the name of John Maynard Keyness if this strange potpourri were to be branded Keynessian.

Huwezi kuwa na stimulus package kwa uchumi ulio almost nonexistent, wenzetu uchumi wanao, umeingia katika msukosuko, wana u stimulate.Sisi tunaiga "fashion".hatuna uchumi wa kuongelea, badala ya kuujenga kwanza, tunataka ku u-stimulate kabla hatujajenga.Tuna cushion industry against world financial downfall, industry gani? Jenga industry kwanza, then utai cushion, sio mchezo wa kuigiza wanataka kuleta "legal EPA".

Huwezi kumfanyia mouth-to-mouth resuscitation mgonjwa anayehitaji coronary artery bypass surgery, unaonyesha usivyotibu ugonjwa na kuhangaika na dalili.Matatizo yetu yalikuwapo tangu kabla ya machafuko ya uchumi wa dunia, na yataendelea hata baada ya machafuko haya, sioni revolutionary ideas, naona more of the same, na kama tunafanya vitu vile vile kila siku (kuombeleza, porojo, kutokuwa na details, siasa nyingi utendaji mdogo, tume juu ya tume, largesse etc) na kutegemea matokeao tofauti, Einstein alishasema tutakuwa vichaa tu.

Si rais peke yake by the way, watu wote tunao m-enable.
 
Back
Top Bottom