mimi sio mchumi bali bajeti yetu ni ya expenditure, yaani bajeti ya kutumia.
Hiyo mipango ya maendeleo, sio maendeleo ya kweli bali sustainability ya
kilichopo, TRL imepe pesa itafune na ATCL ziingizwe zikazamishwe tena na
wale wafanyakazi 300 wanaohudumia ndege 2.
Jana rais ametangaza Stimulus Package ya 1.7 Trilion na leo asubuhi Waziri
Mkulo amewasilisha duplicate ya aliyoyasema rais jana.
Hili fungu sio la kusisimua ukuaji wa ujumi bali ni kutia tumboni kufidia
anguko la uchumi na wafaidikaji wakuu ni vyombo vya fedha na sio kumpatia
ehueni yule mkulima aliyeshindwa kupata pesa, bali unailipa benki kwa vile
mkulima ameshindwa kurudisha mkopo.
Hivyo mdodoro wa uchumi kwa mkulima na mwananchi wa kawaida uko pale pale.
Bajeti hiyo ina technical problems za kiufundi, kama ni kweli hali ya
kiuchumi imedidimia, hii serikali yetu inayoongeza expenditure kila mwaka
huku ikiweka projection za kupata pesa zaidi bila vyanzo vyovyote vipya vya
mapato, ni uwongo unless mipango imepangwa halafu rais akatembeze tena
bakuli as usual.
Kwa mtazamo wangu mimi ambaye si mchumi, watanzania tunapigwa changa la
macho. Serikali itayakopesha mabenki bilioni 80 at 2% interest. Mabenki
yatatakiwa kutoa Bilini 120 hivyo jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 200
zitakuwa open kwa wakopaji, amini usiamini, masharti ya kuzikopa hizo fedha
yatakuwa yale yale na interest zile zile 15%-20% interest na kuendelea.
Nilimtegemea rais angesema kwa vile serikali itakopesha at 2% interest,
mabenki yangelazimishwa kutoa mikopo at less 10% inerest