Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Du! mtuhumiwa Peter Noni in da TIB haus! Mtamtaka!

Maumivu ya kichwa huanza polepole...
 
Nina maswali yafuatayo tu:

a. Serikali ina mpango gani wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (wasteful spending)

b. Serikali ina mpango gani wa kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha za umma kama ilivyoanishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali?

c. Serikali ina mpango gani wa kuchochea ulaji wa ndani (domestic consumption)?

d. Kwenye mashirika ya binafsi ambayo serikali inataka kuysaidia serikali ina mpango gani wa kuchukua hisa kwenye makampuni hayo kama nchi zilizoendelea vimefanya badala y akutoa tu fedha za walipa kodi?
 
kumbe mtikisiko wa uchumi umetuathiri!ha ha haaaaa,mbona hawajaacha kuagiza mashangingi? god help these unsure leaders!
 
Nina maswali yafuatayo tu:

a. Serikali ina mpango gani wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (wasteful spending)

b. Serikali ina mpango gani wa kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha za umma kama ilivyoanishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali?

c. Serikali ina mpango gani wa kuchochea ulaji wa ndani (domestic consumption)?

d. Kwenye mashirika ya binafsi ambayo serikali inataka kuysaidia serikali ina mpango gani wa kuchukua hisa kwenye makampuni hayo kama nchi zilizoendelea vimefanya badala y akutoa tu fedha za walipa kodi?

Serikali ya kisanii haihangaiki kabisa na mambo kama haya ya msingi, wao sasa target ni 2010. Usijeshangaa kuna wataalamu walisuggest such measures na zikapigwa chini ikiaminika hazina mvuto kisiasa. Mimi siamini kabisa kama JK has even a clue of rescuing bizness ya mama ntilie mmoja inayoyumba.
 
Yaani poa sana kila mtu alipe kodi!

This is fair..hii ni pamoja na mashirika ya dini!

Mashangingi ya Maaskofu nayo pia yatozwe kodi!
 
Mie nilidhani kampeni za uchaguzi mkuu ziliisha mwaka 2005.. kumbe bado tupo kwenye kameni...
maana tupewa ahadi juu ya ahadi utekerezaji sufuri....

umeshindwa kwa kila jambo...sasa wanatapatapa.... hazina ilito achwa na chinga wamekomba yote.... hakuna kitu sasa ngoma kasheshe

TANZANIA WILL NEVER EVER DEVELOP UNDER CCM
 
leo waziri wa fedha wa kenya bw. uhuru amesema kuanzia leo watendaji wa ngazi wa juu wote wa serikal watanza kutumia magari ya injin si zaid ya 1800cc....hii ni ktk jitihada ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikal.......Mkulo leo kimya....sijasikia hata mahali akizungumzia jitihada za kupambana na matatizo ya kiuchumi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...matumizi ambayo yanazidi hata hiyo stimulus package iliyotangazwa jana....
 
hiyo baketi sasa kwa ujumla imesikia kilio cha mwananchi wa kipato cha chini au ndo aendele kuhadithiwa yanayojiri ,EPA,RICHIMOND etc
 
Kama ni kweli Tanzania ni Taifa lenye mandondocha,basi amani itabaki milele,lakini kama then ni kweli kuwa Taifa si la mandondocha,then sioni amani ikiendelea kuwepo kwa muda mrefu,unless something really serious happens.
 
JK amezungumzia Stimulas si kwamba kwa kuelewa bali kwa kuiga. Maana sasa mafisadi wamemchanganya akili. Ndiyo maana Mkuu wa kaya anasema jambo mafisadi ambao ndiyo watekelezaji hutekeleza kulingana na faida watakayo ipata. Hata hiyo Bajeti ukiichungulia sana haina faida kwa wananchi.
 
22: To this end Mr. Speaker, I have reduced from ceilings of all ministries, the following non-prority expenditures that I believe will have no material impact on service delivery. These entail reduction as follows:
  • 80 percent on furniture and fittings
  • 60 percent on advertisement publicity
  • 40 percent on telephone expenses
  • 20 Percent on hospitality supplies and services, which include and I emphasize payment to various taskforces appointed by the government and
  • 10 percent on domestic and foreign travel and subsitence

.....extract from Uhuru Kenyatta Budget Speech. Jun 11th 2009 for republic of Kenya.
 
23. Mr. Speaker, government expenditure on transport has increased substantially over the years and unless checked, it will soon become unsustainable. In this regard, I will be requesting the cabinet to approve a new Transport Policy to address this problem early in this financial year. With this in mind, I have put a moratorium on purchase of new motor vehicles, except for security purposes. Any purchase of new vehicles will be allowed only under very exceptional circumstances. Mr. Speaker, we will also introduce use of fuel cards for the purchase of fuel for government vehicles because we believe this measure will significantly reduce the amount of money the government is spending on fuel.


.....extract from Uhuru Kenyatta Budget Speech. Jun 11th 2009 for republic of Kenya.
 
6.4 Encouraging Growth of ICT and Deepening Infrastructure Development
106. First, Mr. Speaker, The East African Marine System Ltd (Teams) and Seacom Kenya Ltd
have invested heavily in under sea fibre optic cables, whose completion and full deployment is
expected to reduce significantly the cost of communication in our country. In addition to other
measures which the Government has so far taken to encourage such investment and to further
encourage the uptake of this facility by the internet service providers and other intermediaries, I
propose:
(i) To allow the internet service providers to offset against their taxable income the cost
incurred in acquiring the right to use the fibre optic cable over a period of twenty years;
(ii) To increase wear and tear on telecommunication equipment including the fibre optic cable
from 12.5% to 20%;
(iii) To provide tax deduction of 5% on computer software.
.....extract from Uhuru Kenyatta Budget Speech. Jun 11th 2009 for republic of Kenya
 
Another EPA in a very vivid form.It's poor farmers who have lost everything and not WACHUUZI.The wachuuzi wanachofanya ni kununua mazao kwa bei ambayo watapata faida bila kujali mkulima ataumia vipi.kama bei katika soko la dunia imeshuka na wao wanashusha bei ya kununulia.Kuwawezesha tena wachuuzi ambao hawakupata hasara ni lazima tujiulize wanapewa fedha kwa ajili gani!!!!!!!!!!
Hivi mnajua kuwa hata kupon za pembejeo zilikuwa zinagawanywa kwa undugu.MASATU(KAMBARAGE) WASIRA,mtoto wa waziri STEVEN WASIRA aliitwa kutoka masomoni marekani ili apewe kupon aweze kusambaza mbolea.
Ndio hao wanaokuwa refunded....
DAMN
''The end of every wicked and oppressing goverment,is of shamefull and agony''


shsssssss!!! wengine tunajifanya hatujui!
 
Another EPA in a very vivid form.It's poor farmers who have lost everything and not WACHUUZI.The wachuuzi wanachofanya ni kununua mazao kwa bei ambayo watapata faida bila kujali mkulima ataumia vipi.kama bei katika soko la dunia imeshuka na wao wanashusha bei ya kununulia.Kuwawezesha tena wachuuzi ambao hawakupata hasara ni lazima tujiulize wanapewa fedha kwa ajili gani!!!!!!!!!!
Hivi mnajua kuwa hata kupon za pembejeo zilikuwa zinagawanywa kwa undugu.MASATU(KAMBARAGE) WASIRA,mtoto wa waziri STEVEN WASIRA aliitwa kutoka masomoni marekani ili apewe kupon aweze kusambaza mbolea.
Ndio hao wanaokuwa refunded....
DAMN
''The end of every wicked and oppressing goverment,is of shamefull and agony''

Sema Notradamus, sema. Mipango ya ku-channel pesa za mikopo na za misaada kwa wapendwa wao kama walivyofanya kwenye EPA imeshaanza.
 
"Tutatoa udhamini wa kuahirisha mikopo ya wale walioathirika na kiasi cha udhamini ni Sh 45 bilioni hivyo benki zitatakiwa zisidai riba kwa miaka miwili na kutoa mitaji ya biashara kwa riba nafuu,"alisema Kikwete.
.....kutumia Sh43 bilioni kuboresha Kampuni ya Reli Tanzania kwa kuwa si mali ya Kampuni ya Rites ya India...
Haya maneno kasema JK au amesemewa?kama sija kosea, nakumbuka JK ndiye alieharakisha mchakato mzima wa kubinafsisha shirika letu la reli... since then amekuwa akitoa fedha za kuendesha hilo shirika kama vile halijabinafsishwa!!! NGONJERA NYINGI ZITACHEZWA KABLA YA UCHAGUZI MKUU!! lakini wajue kuwa tumejiandaa vyakutosha na makombeo zetu this tym...




Something fishy is going on here;
  1. Kuna uhusiano gani kati ya kuwapa RITES pesa na matatizo ya uchumi yanayodaiwa kusababishwa na matatizo ya uchumi wa US/EU?
  2. Nani ni mmiliki wa TRL, serikali yenye 49% ya shares au RITES wenye 51%?
  3. Kwenye website ya RITES India, hawana maelezo yoyote juu ya TRL. Kuna tu namba ya simu ya inayodaiwa kuwa ni overseas ofice in Dar (255-265040), hakuna email wala website link. Inamaana mradi wa Tanzania hauna umuhimu kiasi hiki? Je hawa RITES wa TRL ndio hawa hawa wa India au ni kama ilivyokuwa kwenye deals za Richmond na Dowans?
 
Nawakumbusha Wabunge changamkeni acheni woga na kulala usingizi Bungeni. Changieni hoja zenye kuleta maendeleo si kupitisha bajeti ili mradi mmetia saini kwenye kitabu cha Roll Call, kuwa mlikuwepo Bungeni. Hii bajeti ya danganya toto ati tutaondoa kodi kwenye maziwa ng'ombe wenyewe wako wapi? WAbunge tunafahamu wengi wenu hamyafahamu vizuri hata majimbo yenu ndiyo maana hata shughuli za Serikali zilizomo majimboni mwenu mnashindwa kuzitetea kama vile Shule, Barabara, Dispensaries nk. Pitishen Bajeti inayosaidia kumwondoa Mwananchi katika Ujinga na Umasikini. Angalieni Picha ya Watoto wa Shule iliyoko Nantumbo, Karne hii watoto kukaa kwenye hatari wakati kuna Mafisadi kampuni zao zinalipwa kila siku mamilioni ya shillingi. Je huu ni ungwana?
 
Sijasikia na nina hamu ya kujua. Mfanyakazi amepewa nafuu gani katika mikakati yote ya kukabiliana na mdororo wa Uchumi? Unajua kadi ambazo mfanyakazi kabebeshwa ni kubwa mno na kwa muda mrefu sioni kama Bunge linajaribu kutoa nafuu yeyote kwa Mfanyakazi. Kimsingi kufanya kazi Tanzania na kupata Mshahara unazidi milioni moja (Tzs. 1,000,000) ni mahumivu na karaha tupu. PAYE ( Pay As You Earn) unayotandikwa hapo hadi utajuta na pengine kuona ni heri ungelipwa chini ya laki tano au na zaidi.
Nauliza tena kwa mlioptia hotuba, kuna nafuu yeyote kwa Mfanyakazi wa Kitanzania juu ya kodi anazopigizwa?
 
Back
Top Bottom