Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Mwakjj,
Tofauti moja kubwa ni kwamba serikali ya Obama inaaminika. Sijui kama unaweza kusema hivyo kuhusu serikali ya Kikwete. BTW Susuviri yuko wapi?

Serikali ya Obama inaaminika na nani? Wewe na Susuviri? Obama is ruining the country.
 
Asante sana nimeisoma hiyo hotuba
lakini maswali hakuyaruhusu huenda ikiwa kwamba mkuu ameogopa
maswali hayo nayo makubwa.

ila sasa hao wajamaa wanalipiwa madeni yao
hasa hao wa pamba serikali haioni kuwa itaingia mkenge
kwa wao kuonunua pamba ya wananchi
kwa kuwa kama kuna pamba nyingine iko ghalani
hakuna soko wanunue nyingine waweke wapi.
mambo yatakuwa yaleyale

huenda wachumi mnisaidie kutatua hili? kwangu naona huu
makakati ni wa kisiasa zaidi.
 
Kama kweli Jakaya amedhamilia kuinusulu nchi yetu na mtikisiko wa uchumi duniani ,kitu cha kwanza kabisa lazima aondokane na uanamtandao wake katika kuwateua watu watakaosimamia na kutekeleza mpango alioutangazia taifa;Appointments ziwe on merit sio urafiki, asipofanyahivyo ataendelea kuwateua mashwahiba wake ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa na mwishowe nchi haitafaidika na mpango huu!! Dalili zinaonesha kuwa tusipokuwa makini wakina RA & co. wameishaanza kukaa mkao wa kula kwa kuanza kubuni makampuni feki ili wakombe hiyo RUZUKU aliyoitangaza leo!!
 
Hii sio hotuba...ni copy and paste with a scale of one to one ya ripoti aliyopelekewa mezani.....

someni kumbukumbu ya hotuba yake alipokuwa akizima mwenge TANGA alisema nini na sasaanasema nini..

In short alidai Tanzania haiadhiriki na mtikisiko wa uchumi wa dunia.....anakula matapishi yake sasa.....

This COUNTRY WILL NEVER DEVELOP UNDER CCM
 
Ili kutekeleza kazi yake serikali imekipa kikosi kazi majukumu yafuatayo: (i) Kufanya uchambuzi kuhusu hali halisi ya madhara yatakayotokana na msukosuko wa masoko ya fedha pamoja na kuporomoka kwa uchumi wa dunia kwa uchumi wa Tanzania
(ii) Kushauri,kwa kuzingatia uchambuzi wa hali ya uchumi, hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari za msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na
(iii) Kuchunguza fursa zinazotokana na msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na jinsi ambavyo Tanzania inaweza kufaidika na fursa hizo ili uchumi ubaki imara na kukua zaidi.
Ripoti hii inajumuisha uchambuzi wa athari za msukosuko kwenye sekta mbalimbali, mapendekezo ya hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari hizo na inabainisha fursa mbalimbali zinazotokana na msukosuko huo.

Unaona madhara ya copy and paste hayo......yeye anadai kukipa kikosi kazi majukumu mbele anasoma mapendekezo yao....yaaani kabla ya kumaliza kusoma hotuba jamaa wamesha maliza majukumu na kutoa mapendekezo!!!!!! hii kali

TANZANIA WILL NEVER EVER DEVELOP UNDER CCM
 
Kama kweli Jakaya amedhamilia kuinusulu nchi yetu na mtikisiko wa uchumi duniani ,kitu cha kwanza kabisa lazima aondokane na uanamtandao wake katika kuwateua watu watakaosimamia na kutekeleza mpango alioutangazia taifa;Appointments ziwe on merit sio urafiki, asipofanyahivyo ataendelea kuwateua mashwahiba wake ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa na mwishowe nchi haitafaidika na mpango huu!! Dalili zinaonesha kuwa tusipokuwa makini wakina RA & co. wameishaanza kukaa mkao wa kula kwa kuanza kubuni makampuni feki ili wakombe hiyo RUZUKU aliyoitangaza leo!!

Pia kuna haja ya kuweka bayana utaratibu utakaotumika. Kwa mfano TIB itawezeshwa kuwakopesha wakulima/wawekezaji ni muhimu kukafanyika utaratibu mpya wa kuzitangaza upya huduma za TIB, ili wale wanaostahili kupata huduma wakafahamu uwepo wa huduma hizo.
 
Kama kweli ana nia ya ya kuunusuru uchumi wa nchi yetu basi kwanza kabisa aanze kutekeleza moja ya ahadi zake zilizomsaidia kuchaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi wa 2005. Moja ya hadi hiyo ni kuhakikisha kwamba mikataba ya uchimbaji madini yetu inakuwa na maslahi kwa nchi yetu na siyo 'wachukuaji' waachiwe kuendelea kuchukua 97% ya mapato ya madini yetu huku Watanzania tukiachiwa 3% tu. Pili wezi wote akina Rostam, Mkapa, Chenge, Idrissa Rashid, Mramba, Yona, wahusika wote wa EPA wakiwemo akina Manji, Jeetu, Subhash, Chavda na wengineo wengi wachukuliwe hatua za kweli kabisa na kufilisiwa mali zao zote walizozipata kwa njia za haramu na mali hizo kurudishwa katika mfuko wa hazina.

Hapa kwa maoni yangu ni kampeni tu za 2010 zimeanza rasmi, kwani hadi hii leo hakuna chochote katika ahadi zake za 2005 alichokifanikisha, na huwezi kutoa ahadi mpya kabla ya zile za zamani kutekelezwa hata moja au angalau kutoa sababu za kushindwa kuzitekeleza ahadi zile. Ni USANII mwingine wa hali ya juu umeanza rasmi huku tukielekea katika kinyang'anyiro cha 2010.
 
Date::6/10/2009
Rais Kikwete asafisha njia ya bajeti 2009/10

Rais Kikwete Jumatano ametangaza mpango wa kutumia Sh17bilioni kunusuru uchumi na kusafisha njia ya bajeti 2009/10.

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete, ametangaza mpango wa serikali utakaotumia Sh1.7 trilioni kunusuru uchumi na kumsafishia njia Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Mustafa Mkulo katika bajeti ya serikali atakayoisoma bungeni leo.

Muda mfupi baada ya hotuba hiyo, Waziri Mkulo alikiri kuwa hotuba ya Rais Kikwete itamrahisishia bajeti yake kupita kwa kuwa imeweka mazingira ambayo yatamsaidia yeye na wizara yake.

Hotuba ya Rais ambayo ilichukua zaidi ya saa moja na kusubiriwa kwa hamu, kwa sehemu kubwa imetangaza nusu bajeti ikiwa ni pamoja na kueleza kiasi hicho kuwa fedha kimo katika bajeti ya 2009/10 na kutangaza ukosefu wa mapato ya ndani ya Sh 472.9 bilioni, ambayo tayari yaliingizwa katika bajeti hiyo.

Wakati siku zote serikali akiwemo rais imekuwa ikisema mtikisiko wa uchumi hautathiri Tanzania, lakini katika kutangaza mpango huo jana mjini hapa mbele ya wazee na wabunge, Rais alikiri mtikisiko kuathiri uchumi wa nchi na kuonya kwamba hali hiyo isipodhitiwa inaweza kurejea historia ya mwaka 1980.

Akitangaza mpango huo, alisema serikali imeamua kuchukua dhamana za mabenki, fidia na kuweka misingi endelevu ya kiuchumi.

Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msukosuko wa uchumi duniani na kuwahakikishia kuwa serikali itapambana kiume na tatizo hilo.

Alisema Tanzania ina uzoefu wa kupambana na matatizo kwa kuwa tangu mwaka 2006 imepitia katika vipindi vigumu yakiwemo ya mgao umeme, njaa, mfumuko wa bei ya mafuta na ambayo hayajawahitokea ambayo serikali ilipambana nayo kiume.

Rais Kikwete alisema hayo mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na wazee pamoja na wabunge kuhusu hali ya msukosuko wa uchumi unaoendelea duniani hivi sasa.

"Tutapambana kiume, kwa kuwa tayari yameshatutokea kama haya tangu mwaka 2006 tulipopata mgawo mkubwa wa umeme na kupambana nao kiume kama ilivyokuwa kwa matatizo mengine yaliyofuatia," alisema Kikwete.

Alisema serikali imejiwekea mkakati wa kutumia kiasi Sh1.7 trilioni kupambana na hali hiyo na fedha hizo ziko kwenye bajeti inayotarajiwa kutolewa bungeni leo na Waziri wa Fedha, uchumi na Mipango, Mustafa Mkulo.

Kikwete alifanua zaidi akisema: "Katika kukabili athari hizi nilizozitaja, tunalenga mambo mawili makuu. Kwanza ni kupunguza makali ya msukosuko na pili kulinda uwekezaji ambao ni muhimu katika kudumisha ukuaji endelevu wa uchumi katika kipindi cha muda wa kati".

Alisema mkakati wa kuhami na kuunusuru uchumi unalenga kukabili matatizo ya mpito na dharura, hasa ya ukwasi na siyo ufilisi.

"Mkakati huu sio mbadala wa mipango ya maendeleo na bajeti ya Serikali ya kila mwaka. Chini ya mkakati huu Serikali imepima matatizo kwa uzito wake na kushughulikia yale tu yaliyojitokeza hivi karibuni kutokana na msukosuko wa uchumi na si vinginevyo."

Alisema pamoja na kuwa na mkakati huo wa kiasi hicho cha fedha uchumi wa nchi unatarajiwa kushuka kama lilivyobashiriwa mwaka huu kutoka asilimia 7.4 hadi kufikia asilimia 5 hadi 6 kutokana na msukosuko wa uchumi duniani.

Kikwete alisema pia makusanyo ya serikali yanatarajiwa kushuka kwa asilimia 10 ambayo ni sawa na kupoteza Sh472.9 bilioni katika mapato ya taifa.

"Mwaka huu ni mgumu sana kwenye uchumi wa dunia kwa kuwa hata mapato ya nje yatashuka kutoka Sh2.89 bilioni hadi kufikia Sh2.86 bilioni lakini tuna mikakati ya kunusuru hali hiyo," alisema rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakulima kukopa fedha katika mabenki hapa nchini, mikopo ambayo inaweza isirejeshwe na kuleta mgogoro mwingine, serikali itapunguza mzigo wa madeni na kuwasaidia wanunuzi wa mazao ili wanunue mazao ya wakulima.

Alisema serikali Serikali imeamua kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao kwa msimu uliopita wa 2008/09. Hasara hiyo ni kiasi cha Sh21.9 bilioni na Serikali italipia hasara hiyo ambayo imetokana na kushuka ghafla kwa bei ya mazao ya Tanzania kwenye soko la kimataifa

Alisema kutokana na hilo serikali itayakopesha mabenki ili yaweze kuwakopesha wanunuzi wa mazao, kusaidia sekta ya utalii, viwanda na kadhalika ambapo itatoa kiasi cha Sh270 bilioni kwajili ya hilo.

"Tutatoa udhamini wa kuahirisha mikopo ya wale walioathirika na kiasi cha udhamini ni Sh 45 bilioni hivyo benki zitatakiwa zisidai riba kwa miaka miwili na kutoa mitaji ya biashara kwa riba nafuu,"alisema Kikwete.

Alisema Serikali imeamua kuongeza kasi ya uzalishaji chakula kwa kutoa mikopo ya thamani ya bilioni 20 kupitia Benki ya TIB, na kutoka kiasi kingine cha Sh 20 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo kupitia taasisi za karadha na kuongeza idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku na kiasi cha Sh90 bilioni kitatumika kwa ajili ya mbolea hiyo.

Alisema katika kupambana na msukosuko huo serikali itaongeza idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku, kupunguza viza kwa wageni na kutumia Sh43 bilioni kuboresha Kampuni ya Reli Tanzania kwa kuwa si mali ya Kampuni ya Rites ya India na kuboresha usambazaji wa umeme mkoani Mtwara.

Alisema serikali imeweka kiasi hicho cha fedha ili kupunguza makali ya maisha, kulinda uwekezaji, kulinda ajira, miundombinu, kusaidia upatikanaji wa chakula na kukabiliana na matatizo ya jamii kama magonjwa na kufidia makampuni na wakulima.

Rais Kikwete alifahamisha kuwa kutokana na msukosuko wa uchumi, hadi kufikia Juni mwaka huu watu 48,000 wamepoteza ajira zao.

Kuhusu hali ya benki hapa nchini alisema zipo salama kwa kuwa hayajafungamana na soko la fedha duniani lakini kibiashara nchi imeathirika.

Habari hii imendikwa na

Ramadhan Semtawa na Taus Mbowe, Dodoma na Boniface Meena Dar es Salaam.
 
Haya Waungwana msamiati mpya huo wa kutumika 2010.

"Serikali ilipambana kiume na mafisadi na ufisadi sasa hivi nchi umepungua sana."

Huku Watanzania tukifahamu fika kwamba mafisadi wote wanapeta uraiani na mabilioni yao wakiingia na kutoka nchini kama wanavyotaka. Huu ni usanii wa hali juu. Kazi ipo.
 
hiivi ni tatizo gani jipya kati ya yale raisi aliyoyataja leo halikuwepo kabla uchumi kuwa mbaya duniani? na kama yote yalikuwepo ni kitu gani ambacho hakikumfanya kuyatatua matatizo hayo wakati alipopewa nchi na badala yake anataka kutatua sasa hivi wakati anajiandaa kugombea kipindi cha pili? na kama kweli ana uchungu wa nchi hii na anaogopa nchi itakuwakatika matatizo makubwa kutoka na uchumi mbovu ,inakuwaje anashindwa kuwaadhibu mafisadi mpaka leo?
 
Haya Waungwana msamiati mpya huo wa kutumika 2010.

"Serikali ilipambana kiume na mafisadi na ufisadi sasa hivi nchi umepungua sana."

Huku Watanzania tukifahamu fika kwamba mafisadi wote wanapeta uraiani na mabilioni yao wakiingia na kutoka nchini kama wanavyotaka. Huu ni usanii wa hali juu. Kazi ipo.
hivi kwanini sisi watanzania tunafanywa wajinga kiasi hiki? au kwa vile viongozi wetu wajinga kwahio wanafikiria sisi wote ni kundi moja? lini tutaweza kumzomea raisi in public? hata kama uoga sio kiasi hiki jamani.najua kwamba wana control uchaguzi lakini sio kiasi hiki cha mpaka kuweza kutu control akili zetu.
 
Du! Kumbe kwenye mambo mengine mkuu wewe ni mweupe sana?

Yaani huoni kwamba dhani yenyewe na jambo lenyewe lilistahili ku-be-addressed lenyewe bila kuchanganywa na issue ya bajeti?

Naomba nikuulize tangu lini zaidi ya miaka ya 70 ni mwaka gani tena dunia ilikubwa na mtikisiko kama huu?

Unataka kutuambia rahisi ameongelea mambo ya kawaida ya kila siku...

Kama sisi ni wazalendo... ni vyema kuchukua mambo kama ya kweli machungu kama yalivyo.

Mimi nadhani tungemsaidia rais kwa kumwambia serikali yake iendelee kupunguza matumizi... badala ya kubeza hali ambayo ni mbaya kwetu tayar.
Kasheshe,
That was what I was expecting from this "unpopular" President. But mind you: Tanzania needs a Marshall Plan NOT a Stimulus package! We do not have any economy to be revamped. We must build our economy! huyu anatupa pesa jalalani!! Sisi wala hatueleweki tupo wapi, sijui great depression, recession, tumefilisika au etc
 
Wakuu, heshima mbele! Mwaka jana siku kama ya leo wataalamu wa humu JF walikuwa wameshatubandikia Budget ya mwaka kabla haijasomwa na waziri husika Bungeni. Mambo vipi mwaka huu? Wakulu hebu fanyeji mambo basi tuanze kuichambua.
 
Maybe wameona hakuna haja ya kubandika kwa kuwa hints zilishaelezwa jana na Muungwana !
 
wakati tikisiko la uchumi limetokea Raisi Obama alitangaza mpango wake wa kutenga mabilioni ya dolla kunusuru uchumi wa marekani, japo alikutana na changamoto kutoka kwa wanadiplomasia na wachumi kuhusu huo mpango wake....Kikwete nae katangaza 1.7 trillioni kunusuru uchumi, hivi mpango huu kauandaa kichumi zaidi akiwa na matumaini ya kushinda au kafuata ya obama na sera zake? kama jibu ni ndiyo basi obama akianguka nasi tumeanguka akisimama nasi tumesimama...Mambo ya cold war. wacha tuone.ila kama kaumiza kichwa na kuona mpango wake ni suluhisho la uchumi basi tumuombee kwa kwa mungu afanikiwe.
 
Just to share on some salient features of our 2009/2010 budget:
Expenditure is expected to be 9.51 trillion shillings, up 32 percent over 2008/09.
· Recurrent expenditure is put at 6.69 trillion shillings while the rest will go to development. In 2008/09 the government set recurrent expenditure at 4.73 trillion shillings.
· The government sees 3.18 trillion shillings coming from donors, making up 33 percent of the budget. In 2008/09, donors funded 34 percent of the budget.
· Domestic revenue is seen at 5.1 trillion shillings, or 16.4 percent of gross domestic product (GDP), compared with 4.73 trillion shillings, or 15.9 percent of GDP, a year before.
· The government will seek 1.08 trillion shillings from domestic markets, with 506.19 billion for development spending and 576.5 billion to pay for maturing government securities.
· Agriculture, one sector hard-hit by the slowing global economy, will receive 667 billion shillings, up 30 percent from the year before.
· Education will receive 1.73 trillion shillings, up 22 percent from the previous year.
· Infrastructure will receive 1.09 trillion shillings, up 12.7 percent from 2008/09 to improve railways, roads, ports, airports and help the state-run airline, Air Tanzania

Going by what the President said yesterday, Tanzania is going to boost spending to support the economy.
What are your views on this?
 
Kwenye hii hotuba ya Mh. Jakaya Kikwete, kuna mengi ambayo ameyanena yanayoelekea kuwa na utata wa ukweli wake. Hebu tujaribu kuyadodosa tuone jinsi mkuu wetu wa nchi anavyotumia porojo kuhadaa wananchi. Inakuwa vigumu kuelewa ni kwa nini suala ambalo wamelifanyia kazi badala ya kuweka majedwali ya madhara yaliyotokana hiyo shida wanayodai kuikumba nchi na gharama zake wanatoa tu maelezo yaliyoning'inia hewani. Tuendelee...

Rais Kikwete asafisha njia ya bajeti 2009/10

kikwetebajeti.jpg

Rais Kikwete Jumatano ametangaza mpango wa kutumia Sh17bilioni kunusuru uchumi na kusafisha njia ya bajeti 2009/10.Na Waandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, ametangaza mpango wa serikali utakaotumia Sh1.7 trilioni kunusuru uchumi na kumsafishia njia Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Mustafa Mkulo katika bajeti ya serikali atakayoisoma bungeni leo.

Muda mfupi baada ya hotuba hiyo, Waziri Mkulo alikiri kuwa hotuba ya Rais Kikwete itamrahisishia bajeti yake kupita kwa kuwa imeweka mazingira ambayo yatamsaidia yeye na wizara yake.

Hotuba ya Rais ambayo ilichukua zaidi ya saa moja na kusubiriwa kwa hamu, kwa sehemu kubwa imetangaza nusu bajeti ikiwa ni pamoja na kueleza kiasi hicho kuwa fedha kimo katika bajeti ya 2009/10 na
kutangaza ukosefu wa mapato ya ndani ya Sh 472.9 bilioni, ambayo tayari yaliingizwa katika bajeti hiyo.

Wakati siku zote serikali akiwemo rais imekuwa ikisema mtikisiko wa uchumi hautathiri Tanzania, lakini katika kutangaza mpango huo jana mjini hapa mbele ya wazee na wabunge, Rais alikiri mtikisiko kuathiri uchumi wa nchi

Akitangaza mpango huo, alisema
na kuonya kwamba hali hiyo isipodhitiwa inaweza kurejea historia ya mwaka 1980. serikali imeamua kuchukua dhamana za mabenki, fidia na kuweka misingi endelevu ya kiuchumi.

Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msukosuko wa uchumi duniani na kuwahakikishia kuwa serikali itapambana kiume na tatizo hilo.

Alisema Tanzania ina uzoefu wa kupambana na matatizo kwa kuwa tangu mwaka 2006 imepitia katika vipindi vigumu yakiwemo ya mgao umeme, njaa, mfumuko wa bei ya mafuta na ambayo hayajawahitokea ambayo serikali ilipambana nayo kiume.

Rais Kikwete alisema hayo mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na wazee pamoja na wabunge kuhusu hali ya msukosuko wa uchumi unaoendelea duniani hivi sasa.

"Tutapambana kiume, kwa kuwa tayari yameshatutokea kama haya tangu mwaka 2006 tulipopata mgawo mkubwa wa umeme na kupambana nao kiume kama ilivyokuwa kwa matatizo mengine yaliyofuatia," alisema Kikwete.

Alisema serikali imejiwekea mkakati wa kutumia kiasi Sh1.7 trilioni kupambana na hali hiyo na fedha hizo ziko kwenye bajeti inayotarajiwa kutolewa bungeni leo na Waziri wa Fedha, uchumi na Mipango, Mustafa Mkulo.

Kikwete alifanua zaidi akisema:
"Katika kukabili athari hizi nilizozitaja, tunalenga mambo mawili makuu. Kwanza ni kupunguza makali ya msukosuko na pili kulinda uwekezaji ambao ni muhimu katika kudumisha ukuaji endelevu wa uchumi katika kipindi cha muda wa kati”.

Alisema mkakati wa kuhami na kuunusuru uchumi unalenga kukabili matatizo ya mpito na dharura, hasa ya ukwasi na siyo ufilisi.

"Mkakati huu sio mbadala wa mipango ya maendeleo na bajeti ya Serikali ya kila mwaka.
Chini ya mkakati huu Serikali imepima matatizo kwa uzito wake na kushughulikia yale tu yaliyojitokeza hivi karibuni kutokana na msukosuko wa uchumi na si vinginevyo."

Alisema pamoja na kuwa na mkakati huo wa kiasi hicho cha fedha
uchumi wa nchi unatarajiwa kushuka kama lilivyobashiriwa mwaka huu kutoka asilimia 7.4 hadi kufikia asilimia 5 hadi 6 kutokana na msukosuko wa uchumi duniani.

Kikwete alisema pia makusanyo ya serikali yanatarajiwa kushuka kwa asilimia 10 ambayo ni sawa na kupoteza Sh472.9 bilioni katika mapato ya taifa.

"Mwaka huu ni mgumu sana kwenye uchumi wa dunia kwa kuwa hata mapato ya nje yatashuka kutoka Sh2.89 bilioni hadi kufikiaSh2.86 bilioni lakini tuna mikakati ya kunusuru hali hiyo," alisema rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakulima kukopa fedha katika mabenki hapa nchini, mikopo ambayo inaweza isirejeshwe na kuleta mgogoro mwingine, serikali itapunguza mzigo wa madeni na kuwasaidia wanunuzi wa mazao ili wanunue mazao ya wakulima.

Alisema serikali Serikali imeamua kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao kwa msimu uliopita wa 2008/09. Hasara hiyo ni kiasi cha Sh21.9 bilioni na Serikali italipia hasara hiyo ambayo imetokana na kushuka ghafla kwa bei ya mazao ya Tanzania kwenye soko la kimataifa

Alisema kutokana na hilo serikali itayakopesha mabenki ili yaweze kuwakopesha wanunuzi wa mazao, kusaidia sekta ya utalii, viwanda na kadhalika ambapo itatoa kiasi cha Sh270 bilioni kwajili ya hilo.

"Tutatoa udhamini wa kuahirisha mikopo ya wale walioathirika na kiasi cha udhamini ni Sh 45 bilioni hivyo benki zitatakiwa zisidai riba kwa miaka miwili na kutoa mitaji ya biashara kwa riba nafuu,"alisema Kikwete.

Alisema Serikali imeamua kuongeza kasi ya uzalishaji chakula kwa kutoa mikopo ya thamani ya bilioni 20 kupitia Benki ya TIB, na kutoka kiasi kingine cha Sh 20 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo kupitia taasisi za karadha na kuongeza idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku na kiasi cha Sh90 bilioni kitatumika kwa ajili ya mbolea hiyo.

Alisema katika kupambana na msukosuko huo serikali itaongeza idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku,
kupunguza viza kwa wageni na kutumia Sh43 bilioni kuboresha Kampuni ya Reli Tanzania kwa kuwa si mali ya Kampuni ya Rites ya India na kuboresha usambazaji wa umeme mkoani Mtwara.

Alisema serikali imeweka kiasi hicho cha fedha ili kupunguza makali ya maisha, kulinda uwekezaji, kulinda ajira, miundombinu, kusaidia upatikanaji wa chakula na kukabiliana na matatizo ya jamii kama magonjwa na kufidia makampuni na wakulima.

Rais Kikwete alifahamisha kuwa kutokana na msukosuko wa uchumi, hadi kufikia Juni mwaka huu watu 48,000 wamepoteza ajira zao.

Kuhusu hali ya benki hapa nchini alisema zipo salama kwa kuwa hayajafungamana na soko la fedha duniani lakini kibiashara nchi imeathirika.

Habari hii imendikwa na Ramadhan Semtawa na Taus Mbowe, Dodoma na Boniface Meena Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom