Wadau naomba tujadili hili suala la stimulus package, kama neno lenyewe linavyo elezea na hatua ambazo Nchi zilizoendelea zinachukua/zimechukua versus hatua ambazo nchi yetu inachukua.
Kwanza stimulus package ni hatua zozote zile zinazochukuliwa na nchi katika juhudi za kuchochea ukuaji wa uchumi, na vitu vinavyo kwenda na ukuaji wa uchumi.
Sasa kwa wenzetu wa nchi zilizo endelea vitu vingi vya msingi vya kuchochea uchumi wanavyo, kama Miundombinu sasa tatizo kwao limetokea katika utekelezaji wa sera zao za uchumi kuanzia kwenye kampuni moja moja mpaka katika ujumla wote wa shughuli za kiuchumi hususana katika utoaji wa mikopo.
Sasa tukirudi kwa tanzania tatizo letu kuu la kiuchumi au la vitu vinavyo weza kuchochea uchumi, ni kukosekana kwa Miundo mbinu, na uongozi bora (ufanisi wetu wa kazi au utekelezaji) upo chini kutokana na Rushwa. Na sis tatizo la mikopo.
Hivyo basi Stimulus Package anayo ongelea Mchumi au mtu wa Kawadi wa Tanzania kwa vyovyote vile inatakiwa kwenye kulenga kwenye vitu vifuatavyo
(1). Ujenzi wa barabara kuu, na si kusema Barabara hiyo ipo kwenye Plan ya 2012 kuelekea 2020 blah blah blah. Hivyo vitu vinatakikana Sasa, sioni sababu za kutosheleza za kutojenga Bara bara ya Arusha Dodoma,Mtera Mpaka Iringa.
Songea Mbinga, Songea-Tunduru na nyingine nyingi.
(2)Kuongeza nyezo za kuelemisha watu iwe kupitia television, Maktaba, Shule Bora, Walimu Bora na hata Serikali ikajikita kuweka watendaji wasomi huko Vijijini ili waweze kuwaelimisha watu njia bora za maisha na kujua shida zao.
Angalia kwa mfano Maktaba kuu toka 1971 mpaka sasa ni hiyo hiyo, na badala kuongezeka ina pungua kwa kupangisha majengo yake, vitaba vimepungua au hakuna, Nenda Mkoa wa Kinondoni hakuna maktaba, nenda Temeka, hakuna na hapa ndio karibu na makao makuu ya serikali au mjini.. sembuse Lindi kwa dada salama
(3) Uwekezaji waUmeme au nishati ya Umeme ambayo ni rahisi, hivyo ningependa kusikia hizo 1.7 billioni sehemu kubwa inakwenda kwenye umeme na barabara
(4) Ujenzi wa miundo mbini ya maji na uhifadhi wa Maji ili watu waweza pata maji safi na waweze kumwagilia na kulisha mifugo yao
(5) Mafunzo ya kilimo na ufugaji bora kwa mifano kwa kutumia Tv , filamu na hata study tour kwa wafugaji na wakulima wetu waone wenzao wanafanyaje.
Hivyo vitu vya msingi vikifanyika ndipo unaweza kumlipia kada wa ccm Mkopo wake au kumpa mtaji arudi tena kwenye biashara