mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kama ulishawahi kusikia msemo wa "machozi ya mamba", ndicho mabeberu wanakifanya kwa Ukraine! Mamba akikamata mawindo huwa anatoa machozi!! Hayo machozi ya mamba si dalili ya maumivu Bali ni kielelezo Cha kifurahia utamu wa mawindo aliyopata!
Kumekuwa na makelele ya vilio Toka Nchi za magharibi kuhusu "unyama wa Urusi" kwenye vita inayoendelea Ukraine. Lakini kusema ukweli ni kuwa mabeberu wamepata mawindo! Wamepata kisingizio Cha kuipora Urusi zaidi ya Dola bilioni 300! Lakini pia wanailalia Ukraine kwa kuipatia mikopo yenye riba ya mabilioni ya Dola! Watu wanatangaziwa kuwa ni misaada lakini kwenye mkataba inaandikwa ni mkopo wenye riba (hakuna mlo wa bure kwa mabeberu). Benki ya Dunia inaipatia Ukraine mkopo ya Dola bilioni 5!! Hapo sijataja wakopeshaji wengine Kama UK, IMF, UFARANSA, JAPAN nk.
Kwa hiyo mabeberu wanacheka kweli!! Ndio maana hawataki kabisa yafikiwe makubaliano ya amani kati ya Urusi na Ukraine!! Je nani ataiamsha Ukraine ishtuke?