Unalinganisha volume na value ya bajeti bila ya kufanya mazingatio ya maana katika uendeshaji wa uchumi wa nchi hizi mbili. Angalia madeni, mishahara ya watumishi na viongozi wa kisiasa, aina ya vyanzo vya kodi na kodi halisi inatokusanywa pamoja na athari zake katika ujuaji wa uchumi na maendeleo ya ustawi wa jamii.
Ndugu mtaalam, ulinganifu unaoufanya utakunyanyasa bure maskini. Sio kwamba natetea serikali ya URT kwa kuwa na bajeti ndogo kulinganisha na Kenya, ila hujatenda sawa kulinganisha variable mbili zennye tabia tofauti tena bila ya kuweka ama kuchagua vigezo mahsusi vya kufanya ulinganifu unaoutaka.
Angalia mgawanyo wa bajeti yenyewe katika maeneo mahsusi, kwa mfano, fedha zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo, fedha zilizotengwa kwa matumizi ya kawaida. Pengine angalia aina ya vyanzo vipya vya makusanyo, ongezeko la kodi katika maeneo yenye kugusa maisha na ustawi wa jamii wa mtumishi wa ngazi ya chini na mwananchi wa kawaida.
Aaaaaa kiongozi wangu haya mambo ya bajeti za serikali wakati mwengine tuzitazame tuu. Mwisho wa siku unaeza kuta jumla ya fedha zilizotumika mwisho wa mwaka wa bajeti ni 55% tuu ya zile zilizokadiriwa kukusanywa na kutumika.
Na haswa kwa hawa mabepari wa kikikuyu na kikamba walivyo na mafuta ya uso ndio usiseme. Kwao wao lolote linawezekana.
KARIBU KIBERA MKUU.