Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeidhinishiwa bajeti ya TSh bilioni 519.66 kwa mwaka wa fedha 2025/26, ongezeko la takriban asilimia 82.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/25 ya Shilingi bilioni 285.3.
Pia, Soma: Waziri Kabudi aomba Bunge kupitisha Bajeti ya TSh 519.66 Bilioni kwa mwaka 2025/2026
Maelezo: Bajeti hii iliwasilishwa na Waziri Prof. Palamagamba Kabudi tarehe 7 Mei 2025. Vipaumbele ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo kwa maandalizi ya CHAN 2025 na AFCON 2027, ikijumuisha viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru, uwanja mpya Arusha (TSh bil. 286), na Dodoma (TSh bil. 350), pamoja na viwanja vya mazoezi 10. Pia, zimetengwa fedha kwa kukuza sekta za habari, utamaduni na sanaa nchini.