Bajeti ya mwaka huu ni ya Wizi na ya kinafiki. Hizi Trilioni 49.35 zinaenda kufanyia nini?

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 inatuonesha dhahiri kuwa tulipigwa na kutapeliwa — jamani ebu imagine! Serikali imetangaza bajeti ya TSh trilioni 49.35, tena kwa mbwembwe zilezile za kila mwaka, kana kwamba Watanzania wote ni mabubu na vipofu wa kifikra.

Hii siyo bajeti, huu ni mkakati wa kitaasisi wa kuendeleza grand-scale economic deception. Ni kama sinema mbaya ambayo tumeilazimishwa kuiangalia kila mwaka, tukiambiwa kuwa maendeleo yanakuja, wakati kwa uhalisia tunayopata ni mateso yanayozidi kuhalalishwa kwa lugha ya "vipaumbele vya Taifa".

Serikali inasema bajeti hii inalenga kuimarisha miundombinu, elimu, afya, kilimo, na utawala bora. Hii ni orodha ileile ya maneno matamu ya kisiasa tunayohadithiwa kila bajeti mpya inapokuja, lakini maisha ya wananchi yanazidi kuwa miserable kila uchao. Hivi tunadanganyana hadi lini? Uhalisia uko wazi: barabara za vijijini ni mashimo yasiyopitika, wanafunzi wanakalia tofali darasani, wagonjwa wanakufa kwa ukosefu wa panadol, wakulima wanasota bila pembejeo huku serikali ikijigamba kwa "kwa maendeleo ya watu".

Tujiulize kwa hoja ya msingi: trilioni 49.35 zinakwenda wapi? Tunakatwa kodi kila sehemu — kodi ya mishahara, kodi ya mafuta, kodi kwenye sukari, mchele, huduma, kila mahali kuna makato. Lakini mwananchi wa kawaida hapati value for money. Hii bajeti inatumika kama kifuniko cha kuendesha ulaji wa wachache walio kwenye mfumo. Ni kama serikali imejigeuza kuwa a budgetary cartel, inayotumia mgongo wa maendeleo kuficha miradi ya kifisadi yenye jina la "uwekezaji wa kimkakati".

Tunaambiwa kuwa kuna mikakati ya kuinua sekta ya afya, lakini hakuna hata kituo kimoja cha afya cha kijiji kilichojengwa kwa fedha hizi kilicho na vifaa vya kisasa au wataalamu wa kutosha. Tunaambiwa elimu imepewa kipaumbele, lakini shule nyingi bado hazina vyoo, walimu wanahangaika, na mtaala unazidi kuwa wa mateso badala ya maarifa. Miundombinu? Hii ni hadithi inayokua tu kwenye Excel sheets za hazina na mikataba ya wakandarasi wala rushwa.

Cha kustaajabisha zaidi, wabunge wetu wanapiga makofi na kupongeza kama watoto waliopata pipi ya bure — huku wananchi wao wakiwa kwenye uhalisia wa umasikini wa kutisha. Huu ni budgetary psychosis, watu wamechanganyikiwa na fedha ambazo hawazihisi kwenye maisha yao ya kila siku. Huu ni ujinga uliopangwa — calculated foolishness — wa kuwafanya Watanzania waamini kuwa serikali yao inawajali, wakati ukweli ni kuwa serikali hii inawaibia kisayansi.

Hebu tuulize tena: hizi pesa zimefanya nini? Hakuna impact, hakuna transformation, hakuna maendeleo yanayoonekana. Ni mfumo wa kuandika bajeti kwa tafsida, kuzungumza Kiingereza kingi bungeni, halafu matokeo yake ni sifuri. Na ukisema, unasemwa “una matatizo ya uelewa”. No, this is not a matter of comprehension, it’s a matter of common sense. Tumechoka na propaganda. Tunataka accountability, sio porojo.

Kwa kweli, hii bajeti ya 2025/2026 ni symbol ya mfumo wa kifisadi uliokomaa, ni sindano ya sumu kwa ustawi wa taifa letu. Ni lazima tusimame kwa uelewa, kwa hasira, kwa hoja na kwa uzalendo wa kweli kusema kuwa hii bajeti ni ya wizi mtupu. Hatukubali tena kutumiwa kama chombo cha kulipa mishahara ya walioko madarakani huku sisi tukinyimwa huduma za msingi.
 
Sisi tunajenga makao yetu makuu ambayo Afrika na duniani kote hakuna.
 
Back
Top Bottom