Leo Waziri wa Ujenzi ameliomba Bunge kupitisha TZS 2.564 trilioni kwa mwaka 2026/27.
Lakini kabla Bunge halijapitisha, kuna tatizo moja la msingi linalohitaji ufafanuzi:
📍 Mei 2025, Wizara ililiomba Bunge kupitisha TZS 2.280 trilioni kwa mwaka 2025/26.
📍 Mei 2026 (leo), Wizara inasema bajeti iliyoidhinishwa kwa 2025/26 ilikuwa TZS 1.904 trilioni.
📍 Tofauti: TZS 376.5 bilioni (sawa na asilimia 16.5 ya bajeti ya mwaka mzima)
Hotuba haitueleza kilichotokea kwa fedha hizo.
HAYA SI YOTE.
Karibu kila ongezeko la pendekezo la 2026/27 linaibua maswali zaidi:
Mfuko wa Barabara unaongezwa kwa asilimia 52
— wakati mwaka huu wa fedha umetoa asilimia 47 tu (TZS 324.9 bn kati ya TZS 688.8 bn iliyoidhinishwa).
Fedha za nje zinaongezwa kwa asilimia 53
— wakati bajeti ya mwaka jana ilizidiwa kwa asilimia 0.9 bila maelezo (TZS 609.6 bn dhidi ya TZS 604.0 bn iliyoidhinishwa).
Hati Fungani (Infrastructure Bond) inatangazwa
— bila kiasi, bila riba, bila muda, bila chanzo cha malipo. Ni deni. Lakini deni la shilingi ngapi?
Bajeti ya usimamizi (OC) inapungua kwa asilimia 10
— wakati miradi ya maendeleo inaongezeka kwa asilimia 36.
TAFAKURI YA HARAKA
Wizara ya Ujenzi inadaiwa TZS 1.221 trilioni kwa wakandarasi (chanzo: CAG 2024/25). Hili ni jambo lililoshafichwa wala halijatajwa katika hotuba ya leo. Lakini suluhisho la Wizara ni kukopa zaidi kupitia Hati Fungani — bila kueleza Bunge ni kiasi gani.
Mfuko wa Barabara unaopaswa kuwa mhimili wa matengenezo ya barabara umetoa asilimia 47 kwa miaka mitatu mfululizo. Sasa tunaombwa kuongeza asilimia 52 zaidi. Tunaongeza pesa kwenye mfumo usiotumika.
RIPOTI KAMILI (kurasa 19, ulinganifu na ripoti tatu za CAG, mchanganuo wa tathmini ya hatari, marejeo kamili) imeambatishwa.