Bajeti yawabana mabishoo, ni wale wanaopenda kusajili namba binafsi za magari na kuweka majina yao

Bajeti yawabana mabishoo, ni wale wanaopenda kusajili namba binafsi za magari na kuweka majina yao

Vanity plate ni kwa ajili ya watu wenye pesa na mabishoo,we mwenzangu na mimi wala huna haja ya kulalamika,kwani hujakomolewa wewe na mpaka serikali imeamua kuongeza usidhani wao ni wajinga wameona jinsi watu walivyozipenda na kuzitumia,nina uhakika hao watu wenye kuweka hizo plate wala hawatapungua ndo kwanza wataongezeka,kwani watu wanapenda sana ufahari,na wengi watasubiri kumuona daimond kama ataendelea kuweka au vipi,nna uhakika daimond ataendelea kuweka hiyo namba kwani sidhani kama hiyo milioni 10 ni ishu kwake,tegemea kuwaona wengi wamweka hizo vanity plate.
 
Sijui Serikali wamefikiria nini kuiongeza badala ya kuipunguza....... wangeipunguza au kuiacha pale pale lakini wakapunguza miaka badala ya mitatu iwe miwili, hii ingewafanya wengi zaidi wazimiliki.
 
ABC 123 for 10m na ACB 132 kwa 1m.

Traffic Dept watoe namba nyingi na ziuzwe bei tofauti na wengi wenye uwezo watabadili namba zao

SNIPER 1 Ntailipia nikipata
 
Watendaji wengi wa serikali wana akili mbovu tu. Hawaoni mbali na wala hawajui jinsi ya kupiga pesa.
 
Naona hapa mjadala mkubwa ni kuhusu elasticity of demand. Naamini hadi kufikia hatua hiyo economists watakuwa wametumiwa ipasavyo
Sawa kabisa,na hizo ni luxury gopds aka articles of ostentation. zina violate law of demand,when the price increases it will not lead to fall in demand.
 
Mtoa mada kwanini useme 'mabisho'?...Watu ns heshima zao wanatumia private namba.
 
Tatizo ni kuwa hiyo pesa inakusanywa kwenda kutumika kufanya nini? ikiwa hawataki hata kutuonyesha bunge, wanafunzi wanakaa chini, shida Tupu.. Hata ingekuwa milioni 1 baada ya miaka mitatu, matunda yake mbona hatuoni???? maana imeanza miaka 4 iliyopita, basi hata ingekuwa inaleta picha nzuri kwamba tulipokuwa tunapata mapato kadhaa kitu Fulani kimefanyika, inatakiwa tuongeze hiki na hiki hivyo tunapandisha kodi, ingekuwa afadhali...
 
Kama hela hiyo huna wenzio wanayo, wabongo bhana kwa kufurahia matatizo ya wengine! Tena kwa kujipambanua kabisa eti unaandika "bajeti imewabana mabisho", wewe mbona unatumia simu ya Laki4 wakati zipo za Elfu 26 hatusemi, sio ubisho huo?
 
Ishu ni je wewe binafsi bajeti hii itakusaidiaje? Inaleta unafuu gani? Unashindwa kusikitikia asilimia kumi (10%) ya kila muamala wa M-Pesa unapotuma au kupokea pesa, unashupaa kushangilia mabishoo kupandishiwa gharama za usajili?! Ebu tujadili ya msingi bhana
 
VITU VINGINE VIKIPANDA WALA SIO HATA VYA KULALAMIKIA

Hata hivyo Kupanda kwa gharama ndo kuongeza upekee

Sasa hivi tukiona private sie watembea kwa miguu tuanze kupiga salute kabisa
 
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.

Baada ya kufukuzwa dodoma kisa ukilaza, nilkuwa nawaza kwanini serikali isingeshusha bei ya hizo plate number, yaani zikawepo namba za laki tatu kwa miezi mitatu kwa gari zote ndogo ndogo zisizozidi milioni kumi na tano, ili wale wenye vitz ist e.t.c waweze faidi kumiliki namba hizo. Ziwe kama voucher za simu, ikiisha muda wake unatoa, pia ingeongeza ajira.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.
Mkuu, Kuna vitu vikiwa cheap havileti maana tena.
Private number kuwa expensive ndio selling point. Watu wanataka kuwa na private number kwa sababu ya uchache unao sababishwa na gharama,inafanya waonekane.
Unakuta mtu ana nunua saa dola 30,000 sio kwa sababu it gives better time than the others, ni kwa sababu ya gharama. Probably, saa hiyo hiyo ikipunguzwa bei na kuuzwa dola 3000 watu wanaweza wasinunue na wakaishia kufunga kiwanda.

Mimi binafsi siwezi kununu gari ya milioni 100+ halafu ni weke private number ambayo watu wengi wanaweza ku afford, it makes the car look a bit tacky. Ni bora kuweka number ya kawaida.
 
Mkuu ninavyojua mimi huu ulikuwa ni mpango wa kuongeza vyanzo vya mapato. Sasa kama ni kuongeza vyanzo vya mapato sioni kwa nini waweke bei kubwa sana na kupata bilion 50 wakati wanaweza kupata bilioni 500. Tofauti ya bilioni 450. Hata bei ya shilingi 2.5 milloni kwa miaka mitatu bado ni kiwango cha juu sana kwa Watanzania walio wengi.

Mkuu, Kuna vitu vikiwa cheap havileti maana tena.
Private number kuwa expensive ndio selling point. Watu wanataka kuwa na private number kwa sababu ya uchache unao sababishwa na gharama,inafanya waonekane.
Unakuta mtu ana nunua saa dola 30,000 sio kwa sababu it gives better time than the others, ni kwa sababu ya gharama. Probably, saa hiyo hiyo ikipunguzwa bei na kuuzwa dola 3000 watu wanaweza wasinunue na wakaishia kufunga kiwanda.

Mimi binafsi siwezi kununu gari ya milioni 100+ halafu ni weke private number ambayo watu wengi wanaweza ku afford, it makes the car look a bit tacky. Ni bora kuweka number ya kawaida.
 
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.
Mkuu hapa hakuna weledi wa kuongeza mapato ila kuendeleza falsafa ya wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani (kwa tafsiri ya mkuu mashetani ni raia wa kawaida na masikini)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.
Mi naona kama wameweka ivo ili wa afford wachache ili iwe na thamani,wakipunguza vei wengi wataweka alafu itakua vurugu mtu ana ist ataweka na yeye
 
Back
Top Bottom