Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
BAKAR HAMAD ASHINDA KURA KWA 73.7% UWAKILISHI - JIMBO LA WAWI
Aliyekuwa Mwakilishi katika Jimbo la Wawi, Ndugu Bakar Hamd Bakar ameongoza kwenye kura za maoni zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Wawi ambapo amepata kura 399 sawa na 73.7% kati ya kura 541 zilizopigwa.
Bakar Hamad amewapita kwa kura nyingi wapinzani wake watatu, ambao ni Ndugu Rashid Mjaka Mkuu ambaye amepata kura 73; Ndugu Suleiman Juma Said amepata kura 62 na Ndugu Isha Kassim Said amepata kura 4 ambapo alikuwa akichuana nao katika kinyang'anyiro hicho
Akizungumza mara baada ya kutangazwa matokeo hayo, Ndugu Bakar Hamd Bakar amewashukuru sana wajumbe kwa kumpa kura za kishindo huku akiahidi kuwatumikia wananchi Jimboni endapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampitisha kuwania Uwakilishi Jimbo la Wawi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
#KaziIendelee