Nandagala One
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 1,913
- 2,286
Wana JF Heshima kwenu.
Za kutoka jikoni kwa walio Karibu na "Mjomba" wanaeleza wazi kuwa bwana Mkubwa baada ya kuona upepo namna unavyokwenda, aneonesha nia ya kutogombea Tena Jimbo la Ruangwa.
Japokuwa watu Bado wanakumbuka kuwa alitamka siku ya "Ruangwa Marathon" mwaka wa jana,kuwa atagombea.
Ameanza maandalizi ya awali ya kutaka kumwachia mjumbe wa Bodi ya uhifadhi wa ngorongoro Bwana Bakari Nampenya Kalembo , japo mpaka sasa hajawasiliana rasmi wala kumjulisha kusudio hilo..
Hiyo inatokana kuwa na wakati ngumu kwake,kati ya kumwachia Bakari Nampenya ,au aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni katibu tawala mkoa wa Dodoma , ambaye kimsingi hana jina kubwa mbele ya wana Ruangwa.
Ugumu huo unatokana na ukaribu wa wawili hao, wakati mh Majaliwa anaingia kwenye uchaguzi mdogo kufuatia kifo Cha mbunge wa zamani wa Ruangwa na jasusi Siegfried Ng'itu , Baba mzazi wa huyo Katibu Tawala alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, ambaye alimpambania sana Mh Majaliwa kwenye Siasa za Ruangwa ambazo zilimpeleka mpaka nafasi ya uwaziri Mkuu.
Upande wa Bakari Nampenya ni mpinzani wake Mkubwa ndani ya CCM, ambaye alikuwa ana kibali Cha kukubalika sana,kuanzia Narungombe, Mbekenyera , Ruangwa mjini, kitandi mpaka Likunja.
Nampenya aliombwa atulie pembeni kwenye kura za maoni daima alipoonesha nia, na kupewa shavu la kuwa kwenye bodi ya hifadhi ya ngorongoro kama namna ya kumpoza.
Yote katika yote mh ameonekana wazi anataka kufuata nyayo za Mzee Pinda waziri mkuu Mstaafu, ambaye Sasa analima zabibu na kufuga Nyuki.
Labda yeye anaweza kujikita zaidi kwenye zao Korosho katika mashamba yake, ili awe bega kwa bega na swahiba wake Brigadier General Mstaafu Aloyce Damian Mwanjile ambaye kimsingi yupo Kijiji chienjele mashambani na Namagondo mda mwingi ndani ya tarafa ya Nandagala.
Uamuzi wake na mazingira ya upepo wa Siasa unaonekana pia kutowaacha Salama,baadhi ya watu, hasa mtia nia mtarajiwa wa CCM Jimbo la Nachingwea maarufu kama Fadhil ambaye kwake kupata Ubunge na jina lake kupita anayegemea zaidi nguvu ya PM kuliko kibali Cha Wana Nachingwea.
Hilo kama litatimia basi mh PM atapata Nafasi zaidi ya kufanya labda PhD, baada ya Masters degree ambayo ameifanya japokuwa Kuna mashaka ya kuwa ni ya kimagumashi, inahisiwa ni ya Mchongo.
Yote katika yote itakuwa ni uamuzi mzuri na wana Ruangwa Bado watashukuru kwa Mema mengi na makubwa aliofanyia jimbo la Ruangwa .
Nandagala One,
Mpumalanga -Afrika Kusini .🙏🙏