Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ni vema ukayafahamu haya mapema kwa faida yako
Bali wadau wengi wanajiuliza kwamba ni kitu gani ambacho Serikali ya Tanzania inaweza kufanya, maana unaambiwa ni afadhali hata mtoto mwenye Polio waweza kumpa Magongo akatembea mwenyewe
Kampuni sita za Kitanzania ni miongoni mwa kampuni kadhaa ambazo zimeonyesha nia ya kushirikiana na serikali katika kuendesha Reli ya Standard Gauge (SGR).
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kufuatia kutangazwa kwa Kanuni za Matumizi ya Miundombinu ya Reli kwa Watoa Huduma Binafsi za mwaka 2024.
Akizungumza na Mwananchi leo Juni 19, 2024, Kadogosa amezitaja kampuni hizo kuwa ni GSM, Bakhresa Group, Mohammed Enterprises Company Limited, Lake Oil, Azania na Jambo.
Orodha hiyo pia inajumuisha kampuni kadhaa kutoka China na Ulaya.
“Kati ya kampuni zilizotajwa hapo juu, Jambo ndiyo kampuni pekee ya Kitanzania ambayo imeonyesha nia ya kuanzisha treni ya kifahari ya abiria kwa ajili ya watalii. Asilimia 99 iliyobaki wana hamu ya kuwekeza kwenye usafirishaji wa mizigo,” amesema.
Amesema kwa sasa TRC inajitahidi sana kuhakikisha ujenzi wa sehemu zote za SGR unakamilika ifikapo 2028 ili wawekezaji watumie fursa hiyo na kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.