Bakhresa, Mo Dewji na GSM wajitosa kuwekeza kwenye SGR

Bakhresa, Mo Dewji na GSM wajitosa kuwekeza kwenye SGR

Cha msingi SGR ifike Mwanza na Kigoma tena kwa haraka ili kuua uchumi wa Kenya ambao wao walidhamiria kuua uchumi wetu japo waliiba mkopo reli yao ikaishia njiani.

Bakhresa biashara ya usafirishaji anaweza nashauri apewe mkopo na kipande cha reli ya SGR Tabora -Kigoma amalizie kujenga na kuwekeza treni zake.

Hapa ndipo tulitakiwa kufika miaka mingi yule mjamaa akawa anazuia.
 
Cha msingi SGR ifike Mwanza na Kigoma tena kwa haraka ili kuua uchumi wa Kenya ambao wao walidhamiria kuua uchumi wetu japo waliiba mkopo reli yao ikaishia njiani.

Bakhresa biashara ya usafirishaji anaweza nashauri apewe mkopo na kipande cha reli ya SGR Tabora -Kigoma amalizie kujenga na kuwekeza treni zake.

Hapa ndipo tulitakiwa kufika miaka mingi yule mjamaa akawa anazuia.
Ngoja mfike kwanza ndio muanze kumlaumu yule mjamaa 🙄
Msianze kukata mbeleko kabla mtoto hajazaliwa 😳
 
Kati ya kampuni zilizotajwa hapo juu, Jambo ndiyo kampuni pekee ya Kitanzania ambayo imeonyesha nia ya kuanzisha treni ya kifahari ya abiria kwa ajili ya watalii. Asilimia 99 iliyobaki wana hamu ya kuwekeza kwenye usafirishaji wa mizigo,” amesema.
Kuna fursa kubwa tena ya wazi kwenye reli ya zamani ya meter gauge kwenye utalii. Inashangaza kuona wote wanaamka na tongo tongo kuikodolea macho TZ_SGR train. Zile steam engines zikifufuliwa pamoja na mabehewa chakavu ya enzi zile, reli ya kati kuanzia DAR-DOM-TBR : MZ/KGM iunganishwe na MV.Liemba kule ziwa Tanganyika, ni circuit ya utalii iliyoshiba matukio ya wiki nzima.
 
Kanji ana taka aichape tren mo kiberit had kwenye vioo
 
  • Kicheko
Reactions: Cyb
...lakini usivimbiwe
Sasa wanavimbiwa mpaka Mbunge Shabiby naye amesema Bungeni watu wanaiba mpaka kuvimbiwa 😳🙄

Kisha wanajaribu kumhadaa Mama kwamba anaupiga mwingi kumbe wao ndio wanaupiga mwingi kwa kukwapua pesa za Umma 🙄😳
 
HONGERA SANA KUFIKIA MAAMUZI SAHIHI ya kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma ya usafiri wa treni kwa kutumia miundombinu ya reli ya serikali. Nilishasema humu ya kwamba kwa mfumo wa sheria za utumishi wa umma zilivyo, ni vigumu sana sector ya umma kutoa huduma y viwango na ya uhakika ya usafiri wa treni, hasa ya SGR. Ingekufa tu mapema sana. Uamuzi huo ni mzuri sana unaenda kuleta ushindani,ubora na uhakika wa usafiri wa treni, hasa SGR.
Uko sahihi
 
Kwani matabaka katika jamii hujengwa vipi?

Hawa matajiri sasa wanayo serikali yao. Hawa ndio kipaumbele cha serikali. Wao wana sauti nzito zaidi serikalini kuliko hao akina hohehahe.
Hawa ndio wanaoiamrisha serikali ifuate mipango yao, ya kuwafaidisha zaidi kupitia mgongoni kwa hahehoi.
Badala ya kukaa vijiweni kuongelea uhohe have kanunue train na wewe na hohehahe wenzio
 
Fanya research uone USA private railway ni imejengwa na private kweli.

Serikali inamiliki 30% ya railway road pekee na wanatumia sana ‘Amtrak’ kampuni ambayo kila mwaka inapata hasara uwepo wake ni kwa sababu ya subsidies tu.

Huko Europe serikali Inamiliki karibu 100% ndio wanakodisha private kuendesha, hizo conditions zake za kupewa railway line Bakhresa athubutu kuomba tender.

Fixed costs
Mishahara ya wafanyakazi ni wewe (na wanachukuliwa ni public servants).

Pension zao ni wewe na watumishi wa umma mwajiri anachangia kuanzia 25% ya mshahara

Maintance costs ya line ni wewe na non-negotiable hiyo lazima ulipe inavuka £300m in some lines annually.

Train unanunua wewe

Services za train ni wewe

Variable costs
Ni faida tu serikali inaweza kupa kiwango kwa mwaka kwenye hiyo line labda £250m baada ya kulipa kodi ya faida, kilichobaki ndio chako.

Ukichelewesha train ni wewe

Ukikwama njiani mabasi utayakodi wewe kufikisha abiria wanapokwenda, hakuna kulala njiani siku kadhaa huko train ikipata hitilafu

Hapo labda ndio wanaweza punguza kama ujapata faida kubwa wanaweza chukua percentage badala ya £250m kama huna, hiyo baada ya kulipa kodi zao.

Huko kwenye fixed costs hakuna mjadala usipolipa utakutana nao mahakamani utoe kwenye faida zako sehemu nyingine hiyo aina mjadala.

Bakhresa ataendesha train saa ngapi. Wameshaona jinsi alivyogawa bandari basi kila kitu kugaiwa kinawezekana.

Upuuzi wa Tanzania is beyond me.
 
Back
Top Bottom