May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Moja ya sifa ya lugha yoyote duniani ni pamoja na lugha hiyo kukua.Hujitokeza misamiati,nahau mpya au hata baadhi ya maneno kuchepushwa kutoka kwenye maana take ya asili.Sina utafiti rasmi ila naamini kwa kizazi kilichopo sasa hivi mambo ndio yanaenda kwa kasi Sana.Hivyo basi imekuwa ni ngumu Sana kujua kama maneno au misemo iliyoibuka kama imerasimishwa au la.Na wenye jukumu hilo kwa Tanzania ni Bakita.Ningetamani Taasisi hii iende na wakati uliopo na spidi iliyopo.Nakumbuka kuna hotuba ya Baba wa taifa akishauri Kuwa kama neno limeshika kwenye jamii na hainekani dalili ya kupotea basi lirasimishwe.Sijawahi kusikia mahali neno kama Tapeli,solemba n.k kama yamewahi kurasimishwa. Huenda yapo yanayofanywa na Bakita lakini wengi hatuna taarifa,ila ni vizuri sasa Bakita nanyi muingie mitandaoni tupeane taarifa.