Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Wasemavyo hahenga, masikini hasemwi na mwenye njaa hasutwi.
Leo napenda kuongelea tabia ya timu ya yanga kuwa ombaomba huku wakitembeza bakuli wachangiwe, bado lipo palepale.
Sasa limebadilishwa, linakuja kwa jina la kuchangia 29,000 kwa kila mwanachama. Hii ni dalili tosha kuonesha ukata mkubwa ulio ndani ya timu ya Yanga.
Kwa mawazo yangu GSM wameona hawa yanga hawana ubavu wa kutangaza bidhaa zao za magodoro, wameona wapige kolabo na timu zongine kama Azam fc, Namungo FC nk.
Kusema kweli tangu nizaliwe sijawahi kuona timu inadhaminia na kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa magodoro. Kama kuna mtu hapa anyoshe kidole anitajie timu nyingine tofauti na hizi za hapa Tanzania mdhamini wake anauza magodoro.
Tabia ya kuomba omba imekuwa ni jadi ya yanga, kwa sasa wamekuja na kisingizio cha kujiunga. Uanachama gani wa sh. 29,000? Hili ni bakuli la kisasa. Wameshindwa kutengeneza pesa kupitia magodoro sasa wameanza kuwanyanyasa watanzania
Yangu ni hayo tu.