Pre GE2025 BAKWATA Arusha yamfanyia Dua Maalumu RC Makonda Ili aweze Kufanikiwa katika Malengo yake ya Uongozi

Pre GE2025 BAKWATA Arusha yamfanyia Dua Maalumu RC Makonda Ili aweze Kufanikiwa katika Malengo yake ya Uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sheikh wa mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma akiambatana na viongozi wengine wa BAKWATA mkoa wa Arusha leo, Mei 07.2024 ameongoza sala maalum ya kumuombea kheri Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ili aweze kufanikiwa kwenye programu yake maalum inayoanza kesho Mei 08.2024.

Makonda atakuwa na siku tatu maalum za kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Arusha kuanzia kesho Mei 08 hadi 10.2024 zoezi ambalo litafanyika kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa hio mjini Arusha.

Sheikh Shaaban Bin Juma amempongeza Makonda kwa maono yake ya kuja na programu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, akisema programu hiyo ni sehemu ya kuhakikisha Arusha inakuwa na amani, usalama na matumaini ya kutosha kwa wananchi na wageni wanaofika mkoani humo.

jamaa wa mihemko watapata gubu tena katika hilo 🐒
 
Kuna nguvu gani nyuma ya Makonda, je taaisi za CCM zilizoko chini ya Mwamvuli wa Dini zimeamua kuonesha jeuri mbele ya Viongozi wakuu wa CCM?

Nani anajua kuwa Makala kila siku hufanya vikao na waandishi wa habari?
 
Respect viongozi wa dini ingine Mkuu hata kama huwapendi. Kila mtu akiponda viongozi wa dini isiyo yake nchi huingia kwenye machafuko.

Sheikh wa mkoa huwa hana njaa maana matajiri wote mkoani wa dini yake huwa nae karibu, misaada yote toka nje kuja mkoani inapita kwake, bakwata mkoa wako nae ili mradi njaa hawezi kuwa nayo labda waumini maskini.
Njaa wanayo sana,wanaishi kwa misaada ya waarabu ,pia posho za serikali
 
Kipaji bora cha Makonda kipo ktk kuteka attention ya waja. Hii kazi anaimudu na kuifanikisha vilivyo, bahati nzuri kwake inamfanikishia shabaha zake pia, maana watanzania wengi ni mashabiki wa attention seekers
 
Kumfanyia dua Bashite ni matumizi mabovu ya Ubani.
 
Huyo hata aombewe na dunia nzima hana jipya anabebwa tuu.Utalii utashuka Arusha soon .
Watalii hawana akili kama ya kwako! Akitoka Arusha anaweza kwenda Mwanza au akaenda Dar! Makonda ni jembe hata Samia mwenyewe anajua hilo!
 
Kuna nguvu gani nyuma ya Makonda, je taaisi za CCM zilizoko chini ya Mwamvuli wa Dini zimeamua kuonesha jeuri mbele ya Viongozi wakuu wa CCM?

Nani anajua kuwa Makala kila siku hufanya vikao na waandishi wa habari?
Makala hata anayemfatilia hamna! Kavimbiana mashavu maana anakula sana bia na kitimoto! CCM walichemka sana!
 
Sheikh wa mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma akiambatana na viongozi wengine wa BAKWATA mkoa wa Arusha leo, Mei 07.2024 ameongoza sala maalum ya kumuombea kheri Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ili aweze kufanikiwa kwenye programu yake maalum inayoanza kesho Mei 08.2024.

Makonda atakuwa na siku tatu maalum za kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Arusha kuanzia kesho Mei 08 hadi 10.2024 zoezi ambalo litafanyika kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa hio mjini Arusha.

Sheikh Shaaban Bin Juma amempongeza Makonda kwa maono yake ya kuja na programu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, akisema programu hiyo ni sehemu ya kuhakikisha Arusha inakuwa na amani, usalama na matumaini ya kutosha kwa wananchi na wageni wanaofika mkoani humo.

Kwa upumbavu huu hii nchi haitakuja kuendelea!
 
Mwambieni mtoto mjinga hafaulu kwa kuombewa.Atie bidii alete matokeo.Maswala yakucheza na wadudu sio ishu,mara bike race.Mkuu wa mkoaana mengi ya kufanyua kazi.
Wazo la ulinzi shikrikishi alikua nalo zuri sana,aanzenalo hilo.
 
Back
Top Bottom