CCM yapinga madai ya waraka wa Waislamu kupendelea wakristo
Leon Bahati na Salim Said
Mwananchi
KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga madai ya waislamu kuwa chama chake kinawapendelea wagombea Wakristo na kuwanyima nafasi wale wa Kiislamu.
Aliyasema hayo jana baada ya Shura ya Maimamu Tanzania kuzindua waraka wake ambao umejaa shutuma dhidi ya serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa makanisa.
Waraka huo ulioitwa mwongozo kwa waislamu umetolewa ikiwa ni miezi michache tangu Kanisa Katoliki litoe wa kwake ukilenga kuelimisha wananchi kuwachagua viongozi waadilifu bila kujali dini au kabila na kusisitiza waumini wasichague wagombea mafisadi.
Katika kifungu cha 14 cha waraka huo, waislamu wanadai kuna upendeleo ndani ya vyama ambao umesababisha wabunge Wakristo kufikia asilimia 95 huku waislamu wakibakia na asilimia tano.
Sehemu ya kifungu hicho kilichopo ukurasa wa 39 wa waraka huo, inaeleza: Hata hivyo katika maeneo ya Waislamu, Wakristo hupewa vipaumbele katika uteuzi ndani ya vyama na hatimaye kusukiwa mbinu kuhakikisha wanavuna kura za Waislamu.
Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya.
Makamba amepinga madai hayo ya upendeleo akisema mfumo wa kanuni za CCM za kuwapata wagombea wake ziko wazi na mtu yeyote bila kujali ana dini au la, ana nafasi sawa za uongozi ili mradi ana sifa kwa mujibu wa katiba ya chama.
"Sisi hatutazami dini ya mtu, awe ana dini au hana dini, anaweza kupata nafasi yoyote ya uongozi au kugombea," alisema Makamba ambaye chama chake ndicho chenye wabunge wengi zaidi ya asilimia 60
"Sisi siyo kama wenzetu (vyama vya upinzani) ambako wanaweza kuteuana tu bila taratibu. Sisi tuna mfumo usioweza kuruhusu upendeleo...Kuna kura za maoni ambapo watu wanapiga kura na anayepata kura nyingi ndiye anayeshinda. Suala la upendeleo hapa liko wapi?"
Hata hivyo, Makamba alikataa kutoa maoni ya jumla kuhusiana na waraka huo kwa maelezo kwamba yeye kama kiongozi wa siasa, mambo ya dini siyo kazi yake.
"Mimi ni kiongozi wa siasa, wenzangu wanaongoza dini. Mimi niulize mambo ya siasa nitakujibu," alisema Makamba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo jana aliliambia Mwananchi Jumapili kwamba Watanzania wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya nyaraka hizo kwa sababu ni hatari na zinaweza kuchochea machafuko na kuvuruga amani nchini.
"Niliwahi kusema na narudia tena, viongozi wa dini wanapaswa kuwa makini sana wanapotoa nyaraka kama hizo. Watanzania nao wanapaswa kuwa makini wanaposoma nyaraka hizo kwa sababu zinaweza kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa wananchi," alisema Marmo.
Hata hivyo, Marmo ambaye ni waziri katika serikali ambayo imeshutumiwa kwa kufanya ubaguzi wa kupendelea Wakristo, alikataa kusema lolote kuhusiana na waraka huo wa Waislamu akisisitiza kwamba hajausoma na hadi jana alikuwa hajaupata.
Kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye siku za karibuni amekuwa akisikika mara kwa mara akipinga waraka wa wakatoliki, jana alipata kigugumizi kuzungumzia huu mpya wa maimamu.
Mzee Kingunge ambaye alipinga vikali waraka wa Kanisa Katoliki akiashiria ni msimamo wa CCM, jana alikataa kusema lolote kwa kuwa hakuwa ameusoma.
"Sijausoma, siwezi kusema lolote," alisema Mzee Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa kuteuliwa na rais.
Tofauti na awali alipotoa msimamo bila kuzungumzia maudhui ya waraka, kwamba waraka wowote unaotolewa kupitia dini ni hatari kwa taifa na kuwanyoshea kidole maaskofi wa Katoliki, jana alionyesha wazi kutotaka kutoa msimamo wake.
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum alipinga waraka huo wa Shura ya Maimamu Tanzania akisema utachangia kuleta vurugu nchini.
Vile vile, alitaka usichukuliwe kama ni msimamo wa Bakwata kwa sababu wanaamini Koran Takatifu na Suna za Mtume Mohammad SAW, zinatosha kabisa kuwaongoza Waislamu katika kuwapata viongozi wazuri kwenye chaguzi zijazo.
Alisema kama Bakwata ilivyoupinga waraka wa Kanisa Katoliki, vivyo hivyo wanaupinga huu wa Shura ya Maimamu.
"Sisi hatuoni sababu yoyote ya kutoa mwongozo wakati tuna Koran na Suna za Mtume," alisema Sheikh Salum.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kitendo cha waislaamu kutoa muongozo huo kimesababishwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi na kushindwa kukemea baadhi ya taasisi za dini kutoa nyaraka.
Profesa Lipumba alisema waislaamu wamefanya hivyo baada ya kuona kwamba wenzao Wakatoliki wametoa waraka na ilani kuieleza serikali yale yanayowasumbua katika maisha yao ya kila siku bila ya kukemewa.
Alifafanua kuwa, kushamiri kwa nyaraka na miongozo ya taasisi za dini kwa waumini wao nchini ni tatizo na kwamba linasababishwa na ukosefu wa uongozi katika serikali legelege ya rais Kikwete.
Hizi nyaraka haziashirii mambo mazuri hata kidogo, zinaonyesha kuchoshwa kwa wananchi na utawala dhaifu wa rais Kikwete unaoshindwa hata kudhibiti na kukemea mambo madogo ambayo yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani na usalama wa nchi, alisema profesa Lipumba.
Alisema serikali ya Chama cha Mapinduzi iliwaahidi mambo mengi wananchi wake wakiwamo waislaamu, wakristo na wa dini na madhehebu mengine, yakimo ya kiimani, kisiasa, kiuchumi na kijamii halafu imeshindwa kuyatekeleza.
Alisema muongozo wa waislaam umekuja baada ya serikali kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi na kuona kuwa Ilani ya Kanisa Katoliki kueleza kwamba, mahakama ya kadhi isianzishwe nchini.
Alisema katika muongozo wa waislaamu kuna baadhi ya mambo ni mazuri likiwamo suala la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili tuweze kuwa na chaguzi zilizo huru na za haki.
Ni jambo zuri na la msingi kwamba hata Shura ya Maimamu imeweza kuliona tatizo la kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yenye misingi ya kidemokrasia. Ni imani yangu kuona waumini wa dini zote nchini wanasimama kiimani zao kudai vitu hivi, alisema Profesa Lipumba.
Kuhusu mambo mabaya ndani muongozo huo Lipumba, alisema hasingeweza kutoa maoni yake kwa sasa kwa sababu hakuwa ameusoma bali amesoma na kusikiliza yaliyoandikwa na vyombo vya habari.