BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

CCM yapinga madai ya waraka wa Waislamu kupendelea wakristo

Leon Bahati na Salim Said
Mwananchi

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga madai ya waislamu kuwa chama chake kinawapendelea wagombea Wakristo na kuwanyima nafasi wale wa Kiislamu.

Aliyasema hayo jana baada ya Shura ya Maimamu Tanzania kuzindua waraka wake ambao umejaa shutuma dhidi ya serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa makanisa.

Waraka huo ulioitwa ‘mwongozo kwa waislamu’ umetolewa ikiwa ni miezi michache tangu Kanisa Katoliki litoe wa kwake ukilenga kuelimisha wananchi kuwachagua viongozi waadilifu bila kujali dini au kabila na kusisitiza waumini wasichague wagombea mafisadi.

Katika kifungu cha 14 cha waraka huo, waislamu wanadai kuna upendeleo ndani ya vyama ambao umesababisha wabunge Wakristo kufikia asilimia 95 huku waislamu wakibakia na asilimia tano.

Sehemu ya kifungu hicho kilichopo ukurasa wa 39 wa waraka huo, inaeleza: “Hata hivyo katika maeneo ya Waislamu, Wakristo hupewa vipaumbele katika uteuzi ndani ya vyama na hatimaye kusukiwa mbinu kuhakikisha wanavuna kura za Waislamu.

“Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya.”

Makamba amepinga madai hayo ya upendeleo akisema mfumo wa kanuni za CCM za kuwapata wagombea wake ziko wazi na mtu yeyote bila kujali ana dini au la, ana nafasi sawa za uongozi ili mradi ana sifa kwa mujibu wa katiba ya chama.

"Sisi hatutazami dini ya mtu, awe ana dini au hana dini, anaweza kupata nafasi yoyote ya uongozi au kugombea," alisema Makamba ambaye chama chake ndicho chenye wabunge wengi zaidi ya asilimia 60

"Sisi siyo kama wenzetu (vyama vya upinzani) ambako wanaweza kuteuana tu bila taratibu. Sisi tuna mfumo usioweza kuruhusu upendeleo...Kuna kura za maoni ambapo watu wanapiga kura na anayepata kura nyingi ndiye anayeshinda. Suala la upendeleo hapa liko wapi?"

Hata hivyo, Makamba alikataa kutoa maoni ya jumla kuhusiana na waraka huo kwa maelezo kwamba yeye kama kiongozi wa siasa, mambo ya dini siyo kazi yake.

"Mimi ni kiongozi wa siasa, wenzangu wanaongoza dini. Mimi niulize mambo ya siasa nitakujibu," alisema Makamba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo jana aliliambia Mwananchi Jumapili kwamba Watanzania wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya nyaraka hizo kwa sababu ni hatari na zinaweza kuchochea machafuko na kuvuruga amani nchini.

"Niliwahi kusema na narudia tena, viongozi wa dini wanapaswa kuwa makini sana wanapotoa nyaraka kama hizo. Watanzania nao wanapaswa kuwa makini wanaposoma nyaraka hizo kwa sababu zinaweza kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa wananchi," alisema Marmo.

Hata hivyo, Marmo ambaye ni waziri katika serikali ambayo imeshutumiwa kwa kufanya ubaguzi wa kupendelea Wakristo, alikataa kusema lolote kuhusiana na waraka huo wa Waislamu akisisitiza kwamba hajausoma na hadi jana alikuwa hajaupata.

Kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye siku za karibuni amekuwa akisikika mara kwa mara akipinga waraka wa wakatoliki, jana alipata kigugumizi kuzungumzia huu mpya wa maimamu.

Mzee Kingunge ambaye alipinga vikali waraka wa Kanisa Katoliki akiashiria ni msimamo wa CCM, jana alikataa kusema lolote kwa kuwa hakuwa ameusoma.

"Sijausoma, siwezi kusema lolote," alisema Mzee Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa kuteuliwa na rais.

Tofauti na awali alipotoa msimamo bila kuzungumzia maudhui ya waraka, kwamba waraka wowote unaotolewa kupitia dini ni hatari kwa taifa na kuwanyoshea kidole maaskofi wa Katoliki, jana alionyesha wazi kutotaka kutoa msimamo wake.

Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum alipinga waraka huo wa Shura ya Maimamu Tanzania akisema utachangia kuleta vurugu nchini.

Vile vile, alitaka usichukuliwe kama ni msimamo wa Bakwata kwa sababu wanaamini Koran Takatifu na Suna za Mtume Mohammad SAW, zinatosha kabisa kuwaongoza Waislamu katika kuwapata viongozi wazuri kwenye chaguzi zijazo.

Alisema kama Bakwata ilivyoupinga waraka wa Kanisa Katoliki, vivyo hivyo wanaupinga huu wa Shura ya Maimamu.

"Sisi hatuoni sababu yoyote ya kutoa mwongozo wakati tuna Koran na Suna za Mtume," alisema Sheikh Salum.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kitendo cha waislaamu kutoa muongozo huo kimesababishwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi na kushindwa kukemea baadhi ya taasisi za dini kutoa nyaraka.

Profesa Lipumba alisema waislaamu wamefanya hivyo baada ya kuona kwamba wenzao Wakatoliki wametoa waraka na ilani kuieleza serikali yale yanayowasumbua katika maisha yao ya kila siku bila ya kukemewa.

Alifafanua kuwa, kushamiri kwa nyaraka na miongozo ya taasisi za dini kwa waumini wao nchini ni tatizo na kwamba linasababishwa na ukosefu wa uongozi katika serikali legelege ya rais Kikwete.

“Hizi nyaraka haziashirii mambo mazuri hata kidogo, zinaonyesha kuchoshwa kwa wananchi na utawala dhaifu wa rais Kikwete unaoshindwa hata kudhibiti na kukemea mambo madogo ambayo yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani na usalama wa nchi,” alisema profesa Lipumba.

Alisema serikali ya Chama cha Mapinduzi iliwaahidi mambo mengi wananchi wake wakiwamo waislaamu, wakristo na wa dini na madhehebu mengine, yakimo ya kiimani, kisiasa, kiuchumi na kijamii halafu imeshindwa kuyatekeleza.
Alisema muongozo wa waislaam umekuja baada ya serikali kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi na kuona kuwa Ilani ya Kanisa Katoliki kueleza kwamba, mahakama ya kadhi isianzishwe nchini.

Alisema katika muongozo wa waislaamu kuna baadhi ya mambo ni mazuri likiwamo suala la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili tuweze kuwa na chaguzi zilizo huru na za haki.

“Ni jambo zuri na la msingi kwamba hata Shura ya Maimamu imeweza kuliona tatizo la kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yenye misingi ya kidemokrasia. Ni imani yangu kuona waumini wa dini zote nchini wanasimama kiimani zao kudai vitu hivi,” alisema Profesa Lipumba.

Kuhusu mambo mabaya ndani muongozo huo Lipumba, alisema hasingeweza kutoa maoni yake kwa sasa kwa sababu hakuwa ameusoma bali amesoma na kusikiliza yaliyoandikwa na vyombo vya habari.
 
Haya ndio matatizo ya jazba! Mimi lilidhani baada ya kuusoma waraka wa wenzao Wakatoliki hawa nao wangekuja na waraka ulioboreshwa zaidi ili kujenga kitu kimoja. Sasa waraka huu wa Shura ya Maimamu haujengi chochote. Unabomoa. Sasa ndio wakati wa watu kama Kingunge Ngombale Mwiru kuzungumza. Wanataka kutupeleka wapi hawa???
 
This is a demonstration of short-sightedness on the part of the Council of Imams. It's a piety!
 
KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga madai ya waislamu kuwa chama chake kinawapendelea wagombea Wakristo na kuwanyima nafasi wale wa Kiislamu.

Naona anajipinga na yeye mwenyewe, au keshabatizwa?

Katika kifungu cha 14 cha waraka huo, waislamu wanadai kuna upendeleo ndani ya vyama ambao umesababisha wabunge Wakristo kufikia asilimia 95 huku waislamu wakibakia na asilimia tano.

JK itabidi mawaziri wote wawe waislamu, au vp presida?

Sehemu ya kifungu hicho kilichopo ukurasa wa 39 wa waraka huo, inaeleza: “Hata hivyo katika maeneo ya Waislamu, Wakristo hupewa vipaumbele katika uteuzi ndani ya vyama na hatimaye kusukiwa mbinu kuhakikisha wanavuna kura za Waislamu.

Hivi tz kuna maeneo ya waislamu?
Kama ni ya waislamu, wakristu wanatoka wapi?
Huu upendeleo wanapewa na nani?
Hiyo mbinu inayosukwa ni ipi?

“Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya.”

Hapana,hapana, inabidi waislamu waingie msituni, haiwezekani, wanaonewa sana, sana, aslimia tano tuu!!!

"Sisi siyo kama wenzetu (vyama vya upinzani) ambako wanaweza kuteuana tu bila taratibu. Sisi tuna mfumo usioweza kuruhusu upendeleo...Kuna kura za maoni ambapo watu wanapiga kura na anayepata kura nyingi ndiye anayeshinda. Suala la upendeleo hapa liko wapi?"

Makamba kasahau huo waraka ni kiislamu, na yeye ni muislamu, sasa anamuuliza mwandishi nini tena?

Hata hivyo, Makamba alikataa kutoa maoni ya jumla kuhusiana na waraka huo kwa maelezo kwamba yeye kama kiongozi wa siasa, mambo ya dini siyo kazi yake.[/QUOTE]

Aliweza kutoa maoni juu ya waraka wa wakatoliki, kwanini leo hawezi toa maoni kwa huu waraka?au anaogopa atanyimwa hati ya kuwa muislamu?

"Mimi ni kiongozi wa siasa, wenzangu wanaongoza dini. Mimi niulize mambo ya siasa nitakujibu," alisema Makamba.

Naam, nilisikia kuwa muislamu akikosea, muislamu mwenzake hamkosoi adhari.Acha unafki Makamba.

"Niliwahi kusema na narudia tena, viongozi wa dini wanapaswa kuwa makini sana wanapotoa nyaraka kama hizo. Watanzania nao wanapaswa kuwa makini wanaposoma nyaraka hizo kwa sababu zinaweza kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa wananchi," alisema Marmo.
Marmo wewe ni mkristu, tulia hii ngoma mwachie JK, kwanini unakubali kutumika?

"Sijausoma, siwezi kusema lolote," alisema Mzee Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa kuteuliwa na rais.

No comment kama kawaida.
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum alipinga waraka huo wa Shura ya Maimamu Tanzania akisema utachangia kuleta vurugu nchini.

Vile vile, alitaka usichukuliwe kama ni msimamo wa Bakwata kwa sababu wanaamini Koran Takatifu na Suna za Mtume Mohammad SAW, zinatosha kabisa kuwaongoza Waislamu katika kuwapata viongozi wazuri kwenye chaguzi zijazo.

Alisema kama Bakwata ilivyoupinga waraka wa Kanisa Katoliki, vivyo hivyo wanaupinga huu wa Shura ya Maimamu.

"Sisi hatuoni sababu yoyote ya kutoa mwongozo wakati tuna Koran na Suna za Mtume," alisema Sheikh Salum.

Acha kutuzuga wewe, ninyi wote ni kitu kimoja.

“Hizi nyaraka haziashirii mambo mazuri hata kidogo, zinaonyesha kuchoshwa kwa wananchi na utawala dhaifu wa rais Kikwete unaoshindwa hata kudhibiti na kukemea mambo madogo ambayo yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani na usalama wa nchi,” alisema profesa Lipumba.

Mbona wa wakatoliki uli comment kwa mrengo mwingine?Nasikia wewe pia ni mmoja wa walio-engineer huo waraka.

“Ni jambo zuri na la msingi kwamba hata Shura ya Maimamu imeweza kuliona tatizo la kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yenye misingi ya kidemokrasia. Ni imani yangu kuona waumini wa dini zote nchini wanasimama kiimani zao kudai vitu hivi,” alisema Profesa Lipumba.

Huna jipya zaidi ya pumba=lipumba.
 
Lipumba amezungumza mikakati ya kisiasa na si kidini jamani watu wengine kama hamuwezi kuchambua basi bora mtulie tu,sasa kusema Lipumba hana jipya ,hivi Tanzania ya leo kuna jupya naona sote tupo kwenye Round about na U-Turn kibao.
 
Hivi ni lazima kila dhehebu kutoa waraka? huu waraka ni wa waislamu au shura ya maimu?Waisilamu tanzania huwa wanawakilishwa na BAKWATA taasisi ambayo inatambulika kisheria
 
Vita dhidi ya ufisadi imeanza kutushinda kwa vile wapiganaji tumegawanyika. Penye mgawanyiko hakuna ushindi. Adui yetu ametupiga chenga ya mwili na kuji-camouflage. Katuacha wapiaganaji tukipigana vichwa sisi kwa sisi. Sasa hivi malumbano makubwa yamekuwa kati ya waislamu (shura ya maimamu) na wakristo (wakatoliki). Tumeshindwa kuelekeza nguvu zetu wote kwa adui mmoja. Hakika mafisadi wana akili. Wanajua kuchanganya wapiganaji. Ngoja tuone tunakokwenda, kwani theme ya mapambano inaonekana kuchukua mkondo tofauti.
 
Haya ndio matatizo ya jazba! Mimi lilidhani baada ya kuusoma waraka wa wenzao Wakatoliki hawa nao wangekuja na waraka ulioboreshwa zaidi ili kujenga kitu kimoja. Sasa waraka huu wa Shura ya Maimamu haujengi chochote. Unabomoa. Sasa ndio wakati wa watu kama Kingunge Ngombale Mwiru kuzungumza. Wanataka kutupeleka wapi hawa???
Ni kweli. Wapiganaji tumeshagawanyika. Tunatunishiana misuli sisi kwa sisi badala ya kumshughulikia adui wetu mmoja: ufisadi na yote yanayoendana nayo. Kwa nini Shura imamu wameshindwa kumtambua adui wa kweli wa maisha yetu watanzania?
 
............Kwanini Serikali ya TZ inaikumbatia Bakwata? Kuna agenda gani kwa serikali?

Barubaru,

Kwa kuuliza swali hili jiulize je, kabla ya BaKWATA hapakuwa na umoja mwingine wa waislamu, au jumuiya zingine za kiislamu?, pia jiulize kama zilikuwepo je zimeishia wapi? Pia tafiti iliundwa vipi na kwa kutumia vigezo gani? Ukitafita kwa ndani utagundua na kushangaa sana.
 
vita dhidi ya ufisadi itaishia na vita kamili.

Hili ndilo kosa nililolisema la kanisa Katoliki kutoa waraka.

Kingunge sio kanywea, yeye anajua wazi ikiwa vurugu likitokea yeye na familia yake yote wana uraia wa China, Kyuba na Urusi. Huko watakimbilia na kukaribishwa bila matatizo, sasa tabu ni sisi walala hoi. Hutasikia sauti yake tena, tena CCM sasa hivi wamekubaliana kutozungumza na kuanzisha vurugu la chini kwa chini kati ya waislam na wakristo.

Haya nyie shabikieni tu, mwenzenu Pengo ana uraia wa Vatikan.
 
vita dhidi ya ufisadi imeanza kutushinda kwa vile wapiganaji tumegawanyika. Penye mgawanyiko hakuna ushindi. Adui yetu ametupiga chenga ya mwili na kuji-camouflage. Katuacha wapiaganaji tukipigana vichwa sisi kwa sisi. Sasa hivi malumbano makubwa yamekuwa kati ya waislamu (shura ya maimamu) na wakristo (wakatoliki). Tumeshindwa kuelekeza nguvu zetu wote kwa adui mmoja. Hakika mafisadi wana akili. Wanajua kuchanganya wapiganaji. Ngoja tuone tunakokwenda, kwani theme ya mapambano inaonekana kuchukua mkondo tofauti.

let god give us guidance
 
kwani bakwata anamsemea nani? waislamu wote hatuitambu Bakwata.
 
Kwa kuuliza swali hili jiulize je, kabla ya BaKWATA hapakuwa na umoja mwingine wa waislamu, au jumuiya zingine za kiislamu?, pia jiulize kama zilikuwepo je zimeishia wapi? Pia tafiti iliundwa vipi na kwa kutumia vigezo gani? Ukitafita kwa ndani utagundua na kushangaa sana.
__________________
-------choveki

Mimi ninavyojua na ndivyo ilivyo Bakwata iliundwa mara baada ya rais JK Nyerere kuvunja jumuiya ya waislam ya Afrika mashariki ambayo ilikuwa na nguvu sana.

JK alitumia vyombo mbalimbali vya usalama na kuwatumia baadhi ya waislamu makachero kuuwa Umoja huo na baadaye akashinikiza kuanzishwa kwa BAKWATA chini ya katibu mkuu Kachero Adam Nassib, akina Kachelo Alhaj Kundya na wengine wote.

JK aliunda Bakwata kwa nia na madhumuni ya KUWADHIBITI WAISLAMU kwani ni wao waliokuwa tishio kwake katika kuupenyeza Ukatoliki Nchini. Kwa maana hiyo JK alitumia ushawishi wake mkubwa kuhakikisha kuwa Bakwata ni chombo kinachowakilisha maslahi ya madhehebu yote ya kiislamu tanzania na wakati huo huo ni taasisi ya Serikali katika kudhibiti movement za waislamu.

Kwa misingi hiyo. Bakwata sio chombo kinachokubalika miongoni mwa waislamu bali ni chombo kilichoundwa na Serikali ya Tanzania kuwadhibiti waislamu.

Hata Leo hii waislam wapige kura kuchagua kama wanaipenda Bakwata au jumuiya nyingine zilizoundwa za waislam sidhani kama Bakwata watapata hata 5% ya waislam.

Fikirieni Waislamu wa Tanzania pamoja na pesa zao walizonazo wanazojengea miskiti na kupeana misaada BAKWATA ilishindwa hata kupata pesa za kufanya mkutano wake mkuu wa kuchagua viongozi wake mpaka wakafanyiwa harambee na kuchangiwa na kanisa kufanikisha mkutano huo.

Swali lako Dr barubaru mimi sijui kwanini serikali inaipenda bakwata wakati waislamu wenyewe hatuipendi. labda labda wao wanausajili wa juu kulinganisha na taasisi nyingine za kiislamu. Hilo labda utufafanulie kidogo kuhusu usajili kwa mujibu wa sheria.

Namaliza kwa kusema. Bakwata si lolote si chochote kwa waislamu bali ndio sikio kuu la Serikali.
 
Alisema katika muongozo wa waislaamu kuna baadhi ya mambo ni mazuri likiwamo suala la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili tuweze kuwa na chaguzi zilizo huru na za haki.

Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya."

Haya nyie shabikieni tu, mwenzenu Pengo ana uraia wa Vatikan

Hivi hawa Wakatoliki ni asilimia ngapi ya wakristu wa tanzania?

Je wakatoliki ni asilimia ngapi ya Watanzania?
 
Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya."
..katika suala la Ubunge wagombea mara nyingi hujaribu mahali walipozaliwa. kwa hiyo kuna umuhimu wa mgombea kuwa mwenyeji wa eneo husika kuliko dini.

..kwa mfano: Waislamu wa eneo "XY" wako more likely kumpigia kura mgombea mzaliwa wa "XY", hata kama ni Mkristo, kuliko kumpigia kura Muislamu ambaye si mzaliwa wa "XY."

..hata ktk masuala ya upendeleo wa kazi. mfano: kabila "XY" atamsaidia "M-XY" mwenzake hata kama wanaamini dini tofauti, kuliko kusaidia kabila lingine hata kama wanaamini dini moja.

Katika kifungu cha 14 cha waraka huo, waislamu wanadai kuna upendeleo ndani ya vyama ambao umesababisha wabunge Wakristo kufikia asilimia 95 huku waislamu wakibakia na asilimia tano.

“Kwa muktadha huo, Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki asilimia 75, Wakristo wa madhehebu mengine asilimia 20 na Waislamu huambulia asilimia tano. Katika taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya.”

.

Hii imekaaje Wakuu! Hizi Takwimu zinapatikana Wapi?
 
Yes, kama upo tuusome itakuwa jambo la maana maana si busara kuandikia mate wakati wino upo
 
Unatakiwa utambue mantiki ya hii post, ni kwamba hakuna jumuiya yoyote ya Kikatoliki iliyoupinga ule wa Kikatoliki, ila hapa Jumuiya mojawapo ya Kiislamu ie Bakwata, imeupinga waraka wa Jumuiya nyingine ya Kiislamu. Nadhani utakuwa umegundua kwa nini mleta mada ameamua kuiweka humu !

Inawezekana una mtizamo tofauti na wa alieuweka. Haiwi kuwa amekusudia kuonyesha ukibaraka wa BAKWATA. Waislamu wanahitaji chombo chengine cha kuwasemea na wala sio BAKWATA.
 
Inawezekana una mtizamo tofauti na wa alieuweka. Haiwi kuwa amekusudia kuonyesha ukibaraka wa BAKWATA. Waislamu wanahitaji chombo chengine cha kuwasemea na wala sio BAKWATA.

Hicho chombo kingine nacho kikipatikana mambo yakiwa vipi kinapigwa kibuti kinatafutwa kikingine... kazi kweli kweli!
 
Kakalende mi nakuunga mkono.. TAFADHALI WANAJAMVI MWENYE INFORMATION KUHUSU HII TAASISI NA UFADHILI WAKE AWEKE JAMVINI.tunaweza kuwa tunapambana na mapapa hatujui.Anyway kama miongozo ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu..meaning kuchagua viongozi waadilifu, ni vipi hawa wenzetu waislamu wawe kama wanajazba na hasira kwa wakristo huku wakijifanya eti ni muongozo..kwa mfano sheikh ponda anasema'Akizindua Muongozo huo, Sheikh Ponda alisema wamefikia hatua hiyo kwa vile Waislamu ni jamii iliyodhulumiwa, ambayo inahitaji ukombozi na uhuru.
waislamu wamedhulumiwa na nani? wamedhulumiwa na wakristo au mafisadi ?, kwani ni wasiseme watanzania wamedhulumiwa?mbona walaka wa wakatoliki umejumuisha watanzania wote?
“Lakusikitisha Waislamu leo wanadai uhuru kutoka kwa ndugu zao weusi,” alisema Sheikh Ponda.

hawa ndugu weusi wanaoongelewa hapa ni akina nani?
Jamani nionavyo mimi waislamu wamekuwa wa kulaumu kwamba wanaonewa..
sasa si swala la mafisadi tena bali ni ugomvi wao kwa wakristo, kuna sehemu nimesoma katika quotation kwamba ..eti serikali imetia saini na wakristo kuwapendelea.. that is nosense!!
mimi ninachosema badala ya waislamu kukaa na kulalamika wanaonewa ni bora wakafikiria kuithamini zaidi ELIMU DUNIA na kuacha kuendekeza hiyo wanayoiita elimu akhera..tunahitaji maprofessa wengi wa kiislamu..ukweli ni kwamba bila elimu hakuna maendeleo na bila maendeleo siku zote level yako itakuwa ya chini, na utaona unaonewa.
tunahitaji wawekeze zaidi kwenye mahospitali, mashule, vyuo n.k na siyo vinginevyo.

Inawezekana ukawa na points kwa baadhi ya unayoyaongelea lakini unapojifanya kuwa huoni uonevu juu ya Waislamu unafanya hivyo kwa ajili ya kuvutia upande wako. Hebu tuangalie suala dogo tu la Mahakama ya Kadhi hili lilitaka hiyo unayoiita elimu dunia? Hivyo hili la Wakristo kuhoji kila anapochaguliwa Muislamu kwenye nafasi kubwa huoni kuwa ni tatizo hilo?
Tunapoangalia tabaka au jamii fulani inajiimarisha katika vyombo vya jamii na kuwaacha wengine huoni kuwa hilo linajenga tatizo la kijamii?
Hebu natuangalie hili tatizo la tofauti ya kipato katika jamii yetu, kwanini tunaliona tatizo wakati wenzetu walio na kipato kikubwa waliwahi mapema ikiwa kielimu au kuhodhi rasilimali? Tukae kimya tu na tuache kulaumu na badala yake kama unavyowashauri Waislamu na tuendeleze elimu na tuone jee itafika siku tofauti hii iondoke.
Hili unalolifikiri wewe na pengine wengi wengine ni sawa na kuona kuwa Waislamu wanajitaki wenyewe kwa lililowakuta lakini unasahau kuwa kwa kipindi kirefu kuwa elimu ulikuwa chini ya KANISA na kuipata kulihitajika kupoteza imani ya mtu. Hali hivi sasa imerudia tena kwa utitiri wa vyuo vya kikiristo na ni siri iliyowazi kuwa upo mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa hali hii inaendelea.
 
Back
Top Bottom