BAKWATA iingilie kati uvaaji wa wanawake wakiwa JKT

Katika dini ya kiislamu wanawake hawaruhusiwi kunyoa nywele pia ni wajibu kwao kusitiri mwili mzima. Ukihitaji ushahidi unaeza patiwa sio ujinga kuzungumzia suala hili bali kuna group linaathirika kimyakiya
Yaani ukitaka issue ya dini isimamie kila kitu inabidi iwepo serikali ya Kiislam au Kikristo.

Humo ndimo utaona askali (Ke) mafunzoni wote wamevaa hijab na nikabu wakilala chini, wakirukaruka, kupanda ukuta au kutambaa na tumbo wakiwa hivo unataka.

Hata Gaddafi alikuwa na walinzi (mabinti wa kiislam) wengine hadi wana sijjida ila walivaa kombati zinaonesha bastola (shape) zao sikuwahi kukuona ukimpinga ndg Gaddafi, kuwa anawadhalidhalisha.
 
Sasa hao hapo si kwenye hafla maalum.

Wadhani wakiwa field kwenye mafunzo watavaa hizo?
 
Askari polisi tu wa kiislam hawavaagi ushungi.
Waanzie huko kwanza.
 
Umeanza kama unaelewa unachoandika kumbu wewe ni kenge maji kabisa. Jinga
 
Si umeonyeshwa mpaka picha za wanajeshi wa Kiislamu katika nchi ambazo hata hazina Waislamu wengi ki asilimia, lakini hizo nchi zimeona umuhimu wa kuheshimu Imani za watu as long as haziathiri utendaji. ISLAMOPHOBIA wa hapa kwetu wanaona kama vile hizo taratibu/sheria zimetokana na Holy Scripts other than Qur an, hivyo kuzirekebisha ni sawa na kunajisi NENO LA MUNGU.
 
Hilo ni jeshi, taratibu ndugu
 
Kama mnataka kuishi kwa kufuata misingi ya dini yenu nendeni mkaishi Afghanistan kwa talban, tofauti na hapo mtafuta taratibu zilizopo mnataka au hamtaki
Kamanda, hii ingekuwa ni nchi ya kikristo sawa tungekubali yote hayo, lakini hii nchi ni yetu sote, mkristo hana haki zaidi kuliko muislamu and vice versa. Kitendo cha wewe kudhani kwamba haki ya upande mwengine haina uzito na inafaa kupuuzwa ilhali haipunguzi wala kuongeza chochote katika dini yako hii ni mentality mbaya ya udini. Tabia hizi zisipokemewa huzaa vichochezi vingi vya magomvi katika jamii.

Unachopaswa kufanya ni wewe kusimamia dini yako na kwamba Serikali ikuruhusu kuabudu kwa kadri ya dini yako inavyotaka, bora tu hauvunji haki za wengine katika hilo.
 
Pumba kabisa

Nimepiga kozi na sister wa katoliki na alifata sheria zote kama jeshi linavyoelekeza.
Acheni kujipa uspesho ambao hauna maana.

Sio lazima kuhudhulia mafunzo .
Tatizo lako wewe ni kuwa blocked minded.

Unasahau ya kwamba benchmark yetu sisi ni western countries especially UK na wakati wao ni taifa la Kikristo (Anglican). Hawa hawawezi kutupa suluhisho la matatizo yetu sisi ambo ni taifa lenye dini kuu mbili (with almost equal population distribution), na ieleweke pia Arab countries as well haziwezi kuwa benchmark yetu because they are Islamic countries as well. Tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuheshiamiana kiujumla katika nchi yetu sio tu katika hili linalojadiliwa bali hata katika mengine yote yanayogusa dini.

Kwa mwenye busara ni rahisi kujua kwamba dini zote mbili hakuna inayotufundisha kumdhulumu mwengine, zote zinatufundisha upendo na amani ila miongoni mwetu kuna wanaofata dini kibubusa na ndo wanakuwa na mihemko ya kuleta tofauti na UMIMI kwa kudharau haki za wengine.

Amani ya kweli haipatikani kwa waislamu kuifanya nchi kuwa ya kiislamu wakati kuna an equal portion ya wakristo katika nchi, lakini pia haipatikani kwa wakristo kuifanya nchi kuwa ya kikrsto as well. Kubwa zaidi utulivu haupatikani kwa kuuweka mbele upagani ilhali hiyo ndo population ndogo zaidi ya jamii yetu.
 
ACHA upunguani na kujivimbisha kichwa. Kuna mambo yanataka uniform. Sio Kila jambo lazima lioneshe utofauti wa kiimani na kimatabaka katika jamii. Yaani UNATAKA mtu Kila mahali alipo AVAE kwa kuonesha yeye ni dini gani? Yaani jeshini ukienda ukiangalia TU, ujue huyu ni Rasta farrian, huyu ni Budha, huyu muislamu, huyu mkristo, huyu Chadema, UDP, CUF, ACT nk. Maana ndiko tunakoelekea. Ukianza kujitofautisha kwa dini, itafuata vyama, itaenda kabila, ukanda nk, je Bado kutakuwa na JESHI hapo?. Unaeleweshwa lakini Bado umeshupaza shingo, je una agenda Yako Nyuma ya pazia hili? ACHA UPUMBAVU wa kuligawa Taifa. Unayajua madhara ya hiki unachokipigania?. Tunaweza kupiga marufuku dini zote Tanzania, ila hatuwezi kupiga marufuku JESHI. ACHA ujinga.
 
Kwani bakwata ni nani kwenye nchi hii?
 
Kamanda, don't panic! just improve your argument!

Usishindwe kujadili hoja na kukimbilia kumpachika mtu sifa mbaya, eti "unaligawa taifa", "una ajenda nyuma ya pazia" ... nonsense!!! Ikiwa baadhi ya western countries wanafika mbali kuruhusu polisi wa kike ambao ni minority group (Muslims) kuvaa hijab nini ajabu katika nchi yetu iliyo katika balanced ratio?

Tunaweza kupiga marufuku dini zote Tanzania, ila hatuwezi kupiga marufuku JESHI. ACHA ujinga.
Hii inadhihirisha udogo wa akili yako. Nani amekwambia jeshi lipigwe marufuku? kama ni watu kujulikana tu hata majina pia yanawajulisha wengi tu ni wa dini gani, mbona jeshi halijasema ukiingia jeshini unafutwa jina lako la dini flani na kubatiza watu majina mapya?

Kuwa open minded, if u have a stronger argument then ur argument will prevail not otherwise.
 
Jeshi halinaga hijab bwa mdogo.
 
mambo ya kutupia hijabu jeshini wapi na wapi pelekeni huko msikitini ....nchi ya tanzania haina dini...mjomba
 
Mkuu wewe ukivaa hijabu inatosha
 
Punguani anapomuona mwenzake ndio punguani. Maajabu haya.
Hawa watu chuki ndizo zinazowatoa akili.
 
Sheria inayo tuongoza ni Sheria ya nchi sio Sheria ya dini yoyote sasa unapotaka kuanza kuleta Sheria za dini yako kwenye mambo ya nchi huoni kama unakosea wasiokua wa dini yako🤔🤔 vipi na wao wakitaka Sheria za dini yako zitumike kuna usalama tena hapo 🤔🤔
 
Sheria inayo tuongoza ni Sheria ya nchi sio Sheria ya dini yoyote sasa unapotaka kuanza kuleta Sheria za dini yako kwenye mambo ya nchi huoni kama unakosea wasiokua wa dini yako🤔🤔 vipi na wao wakitaka Sheria za dini yako zitumike kuna usalama tena hapo 🤔🤔 tubaki kwenye Sheria za nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…