Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Nimeipokea na kuileta hapa wakuu, Imfikie Mufti Mkuu wa Bakwata.
Katika Msikiti wa Kisumu, Mtaa wa Mtambani, Magomeni Mikumi, Dar es Salaam kuna Mgogoro mkubwa unafukuta mwaka sasa na ajabu Mufti wa Mkoa ana makazi yake kama mita 100 toka kwenye huo Msikiti.
Hapo nyuma ilitokea kuna Uchaguzi wa Viongozi wa Msikiti na katika wakati huo aliyekuwa Mwenyekiti wa sehemu hiyo alijaribu kuwania moja ya nafasi Msikitini hapo, lakini akaja kuenguliwa kwa kigezo cha kuwa ni kiongozi wa kisiasa hivyo kanuni haziruhusu yeye kuwania nafasi yeyote msikitini kama kiongozi. NINA IMANI KANUNI AU KIPENGELE HICHO kiliwekwa mahususi kuepuka mgawanyiko wa maslahi kwa itikadi za kisiasa katika misikiti.
Ajabu ni kuwa katibu wa sasa aitwaye Abdallah Kitumbi, alichukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa hapo Mtambani. Na baadaye akashinda huo uchaguzi na kuwa Mwenyekiti anayehudumu nafasi hiyo mpaka leo. Waumini wengine walikuja kuhoji na kuomba kikanuni aondolewe katika nafasi yake ya ukatibu wa msikiti lakini mpaka leo hii halijafanyika na yeye kuendelea kung`ang`ania mpaka ilifika hatua Mkuu wa wilaya na OCD wa sehemu husika kuingilia kati na kupiga marufuku mkutano mkuu uliyoombwa na waumini kwa ajili ya kufanya uamuzi wa jambo hilo.
Mufti wa Bakwata imekuwaje hapa mmeruhusu huu mgogoro kwa muda mrefu na mpaka sasa kuna mpasuko mkubwa ndani ya msikiti kwa sababu ya huyo katibu kukumbatiwa na viongozi wengine wa msikiti kwa kigezo cha kupata sapoti ya chama tawala hapo mtaani?
Kuhusu ukiukwaji wa kanuni au kilichofanyika hapo nyuma je hamuoni kama ni unafiki na dhambi ndani ya nyumba ya ibada?. Kuhusu malalamishi ya waumini je ni kwa nini hamtaki kuingilia na kwenda kuwasikiliza na kuacha itikadi na migogoro ya kisiasa ndani ya msikiti wenu?
Je, ni nani alipeleka suala hilo polisi na hatimaye polisi kuzuia huo mkutano mkuu? Kwa maslahi ya nani? Je, hamuoni kuwa mmewanyima haki waumini kusikilizwa na kufanya maamuzi ya kuheshimu kanuni? Je, inawezekanaje kisheria Polisi kuingilia kati na kuvunja mkutano mkuu wa msikiti?
JERAHA LIKITOWEKA, KOVU LITAKUKUMBUSHA!