Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,490
- 38,302
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara ni kwanini serekali imekuwa ikiitambua BAKWATA kama mwakilishi halali wa Waislam wote Tanzania wakati wapo Waislam wengi wasioitambua au wasiofungamanana na BAKWATA. Yapo madhehebu tofauti tofauti katika dini ya kiislam [Shia, Sunni, nk] kama sikosei BAKWATA imeegemea zaid Sunni sasa ni kwanini Shia nao wasiwe na kiongozi wao [Mufti]?
Serekali inatambua katika ukristo yapo madhehebu mbali bali kama vile Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Waanglikani, Wapentekoste, nk, mawasiliano baina ya viongozi [maaskofu] wa madhehebu haya na serekali hayana mgankanyiko kama ilivyo kwa Waislam!
Naomba kupata ufafanuzi wakina hii hali inasababishwa na serekali au labda madhehebu au taasisi zenyewe za kiislam ndiyo chanzo cha huu mparaganyiko?
=====
Maoni ya Wadau
Serekali inatambua katika ukristo yapo madhehebu mbali bali kama vile Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Waanglikani, Wapentekoste, nk, mawasiliano baina ya viongozi [maaskofu] wa madhehebu haya na serekali hayana mgankanyiko kama ilivyo kwa Waislam!
Naomba kupata ufafanuzi wakina hii hali inasababishwa na serekali au labda madhehebu au taasisi zenyewe za kiislam ndiyo chanzo cha huu mparaganyiko?
=====
Maoni ya Wadau
====Napenda kuanza na historia kidogo ya BAKWATA. Hii iliundwa mara baada ya Nyerere kushinikiza kuvunjwa kwa iliyokuwa East Africa Muslim league. Hii ilikuwa na nguvu sana enzi hizo na Nyerere kwa kuhofia hilo alilazimisha kuvunjwa kwa hiyo na akaunda BAKWATA.
hakika aliweka wana USALAMA akina Adam Nassib, Alhaj Kundya na wengine kwa nia na madhumuni ya kuwadhibiti waislamu
Sasa utaona BAKWATA ipo pale kwa nia na madhumuni ya kudhibiti Uislam na waislamu. Na ni chombo mahsusi cha kiserikali kutimiza azma hiyo.
Sasa ni lazima Serikali ifate hilo na inakataa mabalaza mengine yote kama Istiqama, Baraza kuu la taasisi za Kiislam.
Hiyo ndio reason behind kwa Serikali kuikmbatia BAKWATA wakati waislam wenyewe hawaitambui.
.
Ukitaka kujua chanzo cha kuvunjwa kwa EAMWL ni njama zilianzia Iringa na zilianzishwa na nani soma kitabu kinachoitwa Kanisa katoliki na Siasa za Tanzania kilichoandikwa na Padre Silvano.
Kijitabu hiki kilieleza namna kanisa katoliki adui wake mkubwa ni UISLAMU.( pg 23 para 4).
***** ***** ilianza mara baada ya EAMWL ilipotaka kufungua University ya kwanza Tanzania na uanja walipata pale karibu na Uwanja wa Taifa. fedha za ujenzi kila kitu kilikuwa ready. Nyerere na kanisa kuona hilo waliamua kuunda zengwe kwa kutumia vyombo vya serikali kuvunja umoja huo.
nakushauri ukitaka uhondo huo soma kitabu hicho cha Padre Silvano kisha soma hicho kingine utagundua ukweli