.Tofautisha kati ya madhehebu na vyombo vilivyoundwa kuwakilisha madhehebu hayo. Madhehebu ya Kikristo yako mengi kama yalivyo pengine hata ya Kiislamu. Lakini katika wingi wa madhehebu ya Kikristo kuna vyombo ambavyo vimeundwa. Kuna TEC (TAnzania Episcopal Conference = wakatoliki) na CCT (the Council of Churches of Tanzania).
Kwa hiyo kwa waislamu chombo kinachofanana na hivyo ni Bakwata, ambayo ni chombo cha waislamu wote. Sasa sijui kwa nini hamkitaki?
Kumbe usilinganishe madhehebu ya kikristo na taasisi za kiislamu. Taasisi za kiislamu siyo madhehebu ya kiislamu kwa sababu haziko mbadala ya Sunni, Shia, nk. Taasisi hizi ni vyama fulani (associations) au vikundi kama ilivyo VIWAWA, WAWATA, nk kwa wakatoliki.
sasa kwa waislam kuna madhehebu mbalimbali nayo yana jumuiya zao kama Jumuiya ya Sunni, Jumuiya ya Hibadhi( Istiqama) mimi ni hibadhi., Jumuiya ya shia, Jumuiya ya bohora n.k.
sasa ninavyona Ilitakiwa Serikali iwaeleze waislam waunde kitu kama umoja wa madhehebu ya kiislam ndani ya tanzania (the Council of muslims of Tanzania.) na wao Serikali wangepata na kupokea kauli za waislamu toka katika chombo hicho kama wanavyopata taarifa za wakristo toka CCT.
Mimi naona Kuna siri kubwa sana kwa Serikali ya Tanzania kuwahifadhi BAKWATA.
Tukumbuke BAKWATA ilishindwa hata kufanya mkutano wake mkuu mpaka Mrema alipohitisha harambee na Makanisa yakachangia kufanikisha hilo. hapo utaona Serikali ina jambo kubwa ya kuilinda na kudhibitisha chombo hiki kinakuwa kwa njia yoyote.
Bakwata haina wafuasi zaidi ya viongozi wa Serikali.