BAKWATA ni mwakilishi halali wa Waislam wote?

.

sasa kwa waislam kuna madhehebu mbalimbali nayo yana jumuiya zao kama Jumuiya ya Sunni, Jumuiya ya Hibadhi( Istiqama) mimi ni hibadhi., Jumuiya ya shia, Jumuiya ya bohora n.k.

sasa ninavyona Ilitakiwa Serikali iwaeleze waislam waunde kitu kama umoja wa madhehebu ya kiislam ndani ya tanzania (the Council of muslims of Tanzania.) na wao Serikali wangepata na kupokea kauli za waislamu toka katika chombo hicho kama wanavyopata taarifa za wakristo toka CCT.

Mimi naona Kuna siri kubwa sana kwa Serikali ya Tanzania kuwahifadhi BAKWATA.
Tukumbuke BAKWATA ilishindwa hata kufanya mkutano wake mkuu mpaka Mrema alipohitisha harambee na Makanisa yakachangia kufanikisha hilo. hapo utaona Serikali ina jambo kubwa ya kuilinda na kudhibitisha chombo hiki kinakuwa kwa njia yoyote.

Bakwata haina wafuasi zaidi ya viongozi wa Serikali.
 

Soma kitabu hicho kanisa katoliki na Siasa za tanzania cha Padre sivalon bila shaka utaelimika zaidi kuhusu mambo haya
 
Soma kitabu hicho kanisa katoliki na Siasa za tanzania cha Padre sivalon bila shaka utaelimika zaidi kuhusu mambo haya

Siyo wote tuna access na hicho kitabu. Ingekua vizuri ukitoa point uka cite basi na hizo source kama unazo. Hapa tunaelimishana mkuu so usione uvivu kuandika mistari michche kutoka kwenye hicho kitabu au source nyingine.
 

Serikali iwaeleze waislamu waunde chombo chao kwani wao wakiunda bila kuelezwa na Serikali chombo hicho hakitakuwa halali? Si mtaanza tena kudai kuwa chombo hakiko huru kwa kuwa kiliundwa kwa maelekezo ya serikali? Halafu kuhusu usalama wa taifa, wako kila mahali hata makanisani, mbona inaonekana kama wamejichimbia BAKWATA tu? Na je, katiba ya BAKWATA ikoje, kuna clause (vifungu) zozote zinazoonyesha kwamba kuna mkono wa serikali? Mimi bado sijapata mantiki ya ndoa ya Serikali na BAKWATA, japokuwa sikatai moja kwa moja kwamba ipo au la!
 
.

Ni moja kati ya kazi za Serikali kwa wananchi wake ni kuwapa mwongozo. Sasa ni vizuri ikawapa mwongozo wa kuunda chombo hicho ambacho kitakuwa kina uakilishi wa kila dhahebu ndani ya uislam.

Mfano mzuri hivi sasa huko Tanzania. Serikali imetoa mwongozo kuhusu mazungumzo yake na waislam kuhusu mahakama ya Kadhi. Imetaka waislamu wote waungane na kuleta wawakilishi ndio wakapatikana wale 25 nao wakamchagua Shehe wa Bakwata kama kiongozi wao. Na tena Serikali imetoa mwongozo mwingine kuwa sasa inataka wawakilishi waTano tu miongoni mwao. Ambao mpaka sasa unaendelea mchakato.


Kwa kifupi katiba ya bakwata ni utata mtupu ipo sawa kabisa na katiba ya CCM ile ya mwaka 1977 especially kwenye kipengele cha uongozi. Shehe mkuu ana madaraka makubwa mno ya hata kumfukuza mtu yoyote bila kuhojiwa na chombo chochote.
Sina uhakika kama katiba hiyo itakuwa imebadilishwa
 

MwanaFalsafa.

Waislam hawana hoja ya msingi kila mara wanakuja na malalamiko yasiyokuwa na kichwa na wala miguu.
Ukiondoa mabohora na aga khan ambayo ni madhehebu ya kiislam yanayo ongozwa na waislam wahindi wana maendeleo lakini wenzetu wabantu hawana akili kabisa wako kwaajili ya familia zao na si uislam kwa ujumla.
 
.

Vipi umeshapiga mswaki lakini? Mbona bado una matongotongo mpaka saa hizi?
 

Inasemekana Nyerere Aliivunja East African Muslim League Kuepusha Taifa...,Kwani Ingeweza Kuwa kama Boko Haram au Al shabaab
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…