BAKWATA waiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini Bungeni

Waunde tu chama cha siasa. Wananiudhi tu kelele ya masipika hasa maeneo ya kunduchi mtakuja pale
 
Dawa ya huu ujinga wote ilikuwa ni ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Sema ndiyo hivyo tena; wanasiasa kutokana na ubinafsi wao, wameona waturudishe miaka zaidi ya 40 nyuma.
 
Kujisimamia wenyewe tu hawawezi ,chuo kikuu mpaka Mzee Mkapa akawapa majengo, kwanza kila mwaka wawe wanaenda Lupasu kuhiji, huko bungeni watawakilisha nini, watafute vyama wakagombee, waliopo mule tunaona wengi sana alaa! Wakatafute mapori walime huko!
 
HUU NI UPUUZI,DINI ZA NINI BUNGENI WAKATI NCHI HAINA DINI?

HIVI MTU HADI KUWAZA KIWANGO HIKI KUWA AMETOKA KULA NINI?
 
Halafu wenzao wanaendelea wanaanza kulalamika wanapendelewa, hivi tasisi wamejenga hosp na vifaa wameweka serikali itashindwa kuwalipa wafanyakazi ili hali wanasaidia wananchi! Sijui wapoje wale watu.
 
Ni waislamu wachache wanaweza kuwa na vision kama yako.
 
Expert sikubaliani na mawazo yako,kwahiyo waache kupinga mambo haramu kwakuwa hawajatoa solution ya nini kifanyike,naona hapo umeingia chaka

Kwa maana nyingine hawa viongozi wa dini au taasisi za dini zisikemee uovu kisa hawajatoa njia mbadala? Hivi kabla ya betting watu walikuwa wanaendeshaje maisha yao?

Unazungumzia sijui wananyima tende,hivi una ushahidi au na wewe yale unayoyasikia vijiweni nawe unayaamini tu,natambua kama wewe ni muislamu tunaambiwa katika qur'aan tukufu kwamba anapo wajia mtu na kuwapa habari yoyote basi kwanza muichunguze ili msije mkawa dhuru watu bure pasina kujua

sasa expert mwenzangu,je umejiridhisha na habar hii au unataka kuwavunjia watu heshima bure,tuchunge sana vinywa vyetu
 
Nchi itaongozwa zaidi kwa maombi badala ya kazi na ubunifu tukiruhusu ajenda hii ya maaskofu na masheikh

Wamealika sana katika mikutano ya kiserikali na kisiasa, sasa wamenogewa wanataka madaraka ya ki sekuka secular wafaidi mambo ya kidunia

Baadaye watakuwa wanapokea amri kutoka Rome, Jerusalem, Mecca, Najaf, Karbala, Alexandria, Tehran n.k kuzileta bungeni zijadiliwe, hii ni hatari ipo siku kila kitu kitaangliwa kidhehebu dhehebu na kiimani badala ya kiuchumi, kidemokrasia, kijamii na kisayansi kutokana na akili za mtu mweusi kupeleka akili zao kwa imani za kigeni.
 
Kuna Mzee mmoja sheih nani sijui mweupe hivi alikuwa na meno ya mbalimbali sijamuona siku nyingi mada za dini walikuwa sana chanel 10 hivi yupo wapi? Ha ha ha hii hajachangia kweli Mzee mdini yule mmm!
 
Ni waislamu wachache wanaweza kuwa na vision kama yako.
Nikiliweka hili suala kiujumla, si kwamba najizungumzia mimi kwa sababu binafsi bado najijua ni mdogo sana kimaarifa ila nafahamu hili kuhusu Bakwata: Bakwata huwa hawahitaji waislamu wenye elimu na wenye kujielewa. Ukiwa na hizo sifa watakupiga vita humo ndani.

Hili suala aliniambia baba yangu tangu mwaka 2003 kipindi hicho nipo naye sebuleni tunatizama tv Bakwata viongozi wa dini wakihojiwa stesheni ya TVT. Kulikuwa na muislamu mmoja ni PhD holder na amesoma dini alikuwa anahitaji nafasi ya u-Mufti.

Ila baada ya kukua nikajua viongozi wa Bakwata wengi sana wanaendekeza ushirikina, si ajabu wakakuroga.
 
Sasa kuroga si kama kunywa maji tu πŸ˜€ unazunguka tu nyuma ya nyumba ha ha h
 
Bora hata amri ya Roma maana ni watu wenye elimu zao zakutosha, hawaokotani kama kuchambua chuya.
 
Walivyosikia "Separation of Church and State" wakasema "Sisi wa msikitini haituhusu hiyo" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Labda viongozi wa Dini wapewe nafasi ya ''observers" lakini wasiwe wabunge, wakuu mnaonaje?
 
VIONGOZI WA KIDINI KUAMUA KUWA CHAWA, WALILIA KUWA WABUNGE WA VITI MAALUM KUSHIRIKIANA NA MIHIMILI KANDAMIZI

Fast forward 2025 viongozi wa kidini karne hii nchini Tanzania kuwa chawa, mawakala, madalali, vibaraka na mamluki wa mstari wa mbele kabisa kutetea ubeberu na ukoloni mamboleo, kunyamazia unyanyasaji, mauaji, nini kimewapata wazee wa mjini wa kileo ambao mababu zao wa miaka ya 1950 walipinga kuwa watwana ndani ya nchi yao...

Je kuna tatizo kwa baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Uislamu, Ukristo nchini Tanganyika kukemea ukoloni kwa sasa ?


Nyerere azungumzia dini ziwe mstari wa mbele katika ukombozi wa kweli

21 Mar 2020
Managua, Nicaragua

Julius Nyerere - Nini Kimewapata viongozi wa dini mmeamua kukaa kimya huku mnaona uonevu ukitamalaki !

View: https://m.youtube.com/watch?v=TAP6O3MeqiADescription
 
Aloo nimecheka as I reacted to your post
 
haya maV8 mjapan anayotoa inasababisha waafrika kutoana roho, Kila mtu anapambana akae kwenye kilo ale keki ya nchi.
 
gTurn Ritz FaizaFoxy Malaria 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…