Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Akhy, nashukuru kwa mchango wako!Expert sikubaliani na mawazo yako,kwahiyo waache kupinga mambo haramu kwakuwa hawajatoa solution ya nini kifanyike,naona hapo umeingia chaka
Kwa maana nyingine hawa viongozi wa dini au taasisi za dini zisikemee uovu kisa hawajatoa njia mbadala? Hivi kabla ya betting watu walikuwa wanaendeshaje maisha yao?
Unazungumzia sijui wananyima tende,hivi una ushahidi au na wewe yale unayoyasikia vijiweni nawe unayaamini tu,natambua kama wewe ni muislamu tunaambiwa katika qur'aan tukufu kwamba anapo wajia mtu na kuwapa habari yoyote basi kwanza muichunguze ili msije mkawa dhuru watu bure pasina kujua
sasa expert mwenzangu,je umejiridhisha na habar hii au unataka kuwavunjia watu heshima bure,tuchunge sana vinywa vyetu
Binafsi si mbetiji na siungi mkono suala la betting. Imam Ghazali anasema unapotaka kutibu tatizo kwanza dili na chanzo chake.
Hata kwenye dini mtu akiiba hakatwi mkono papo hapo! Ni lazima kwanza ichunguzwe kwa nini kaiba. Ikiwa kama wizi wake ni kutokana na hali ngumu ya kimaisha inatakiwa awezeshwe! Ila ikowa ni sababu nyenginezo ambazo hazina mashiko hukumu itampitia.
Vijana wengi wao kwa sasa wanabeti kutokana na hali ngumu ya maisha. Ajira hakuna na hata kujiajiri kwenyewe kunaitaji kuwezeshwa na hizo fursa hakuna. Kijana kama huyu unafikiri kipato chake kitatokana na nini kama siyo betting ambayo sasa imefanywa shughuli rasmi?
Bakwata ingejikita kwanza kuishauri serikali itanue wigo wa raia wawe na shughuli rasmi na za kihalali ambazo zinakwenda sambamba na maadili ya jamii zetu pamoja na maadili ya dini zetu.
Kwa namna hiyo ingeishauri serikali kwa namna kama wataalamu wa masuala.ya uchumi wanavyo washauri. Baada ya hapo ndipo wangetoa ushauri wao huu. Yaani kwa kufanya hivyo, itasaidia vijana kujiepusha na betting kwani ni suala baya linaongeza umasikini. Kwa misingi hiyo tunaishauri serikali ipige marufuku kwa kulinda maadili na kukiokoa kizazi.