BAKWATA waiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini Bungeni

Akhy, nashukuru kwa mchango wako!

Binafsi si mbetiji na siungi mkono suala la betting. Imam Ghazali anasema unapotaka kutibu tatizo kwanza dili na chanzo chake.

Hata kwenye dini mtu akiiba hakatwi mkono papo hapo! Ni lazima kwanza ichunguzwe kwa nini kaiba. Ikiwa kama wizi wake ni kutokana na hali ngumu ya kimaisha inatakiwa awezeshwe! Ila ikowa ni sababu nyenginezo ambazo hazina mashiko hukumu itampitia.

Vijana wengi wao kwa sasa wanabeti kutokana na hali ngumu ya maisha. Ajira hakuna na hata kujiajiri kwenyewe kunaitaji kuwezeshwa na hizo fursa hakuna. Kijana kama huyu unafikiri kipato chake kitatokana na nini kama siyo betting ambayo sasa imefanywa shughuli rasmi?

Bakwata ingejikita kwanza kuishauri serikali itanue wigo wa raia wawe na shughuli rasmi na za kihalali ambazo zinakwenda sambamba na maadili ya jamii zetu pamoja na maadili ya dini zetu.

Kwa namna hiyo ingeishauri serikali kwa namna kama wataalamu wa masuala.ya uchumi wanavyo washauri. Baada ya hapo ndipo wangetoa ushauri wao huu. Yaani kwa kufanya hivyo, itasaidia vijana kujiepusha na betting kwani ni suala baya linaongeza umasikini. Kwa misingi hiyo tunaishauri serikali ipige marufuku kwa kulinda maadili na kukiokoa kizazi.
 
Dola siku zote ni chombo kandamizi, viongozi hawa wanatakiwa wasiwe sehemu ya wafanya maamuzi katika vyombo vya dola.

Viongozi wa kidini waendelee kukemea maovu ya kila aina wakiwa huru nje ya vyombo hivi wanavyolilia wapewe viti maalum vya ubunge.
 
Kazi kweli kweli
 
Sasa kuroga si kama kunywa maji tu 😀 unazunguka tu nyuma ya nyumba ha ha h
Aah wapi ndugu yangu!

Mambo ya kutupiana majini nawaachia wao wenyewe.

Viongozi wapo kwa maslahi yao binafsi na hawapo kama dini inavyofundisha.
 
Aloo nimecheka as I reacted to your post
Amini Mkuu Scars.

Na ndiyo maana kibongo bongo viongozi wa dini wanaojielewa na wenye hofu ya Mungu kwa namna ya mafundisho yanavyosema wamechagua kutojihusihsa kwenye mambo ya kiuongozi wa Taasisi mfano wa Bakwata.

Wao wanafundisha watu dini na kuwalea malezi ya kiroho. Na huwa hawapendi kuonekana kwenye TV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…