Sasa mtoto wa kwako, unasubili upewe kibari na mahakama, bakwata Ili aolewe!
Kwanza hakuna waziri, mkuu wa wilaya, mkoa, mtumishi wa umma, mwenye uchumi wa kati anayeweza kuoza mtoto wake wa miaka 14, hata 18!. Umri huo mtoto Bado yupo chuo kikuu,au secondary,wale wa kishua ndio kwanza Bado anqcheza video game nyumbani!
Hizi sheria zinafanya kazi kwa watoto wa maskini, mafukara wasiojiweza, unakuta sheikh kakapenda kabinti, ambako wazazi wake ni choka mbaya, anatoa mpunga anaenda kukarukia.
Hivi mzazi mwenye akili timamu, unaozaje Binti wa miaka 14!
Utasikia shule imemshinda!!binadamu Wana vipawa vingi sana, hata Elimu rasmi ikimshinda, zipo Elimu zingine