Balaa jingine, Wataalamu wadai Gonorea halitibiki tena…..!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421


Hakuna anayependa kupata maradhi ya zinaa, lakini kama kwa bahati mbaya utapata ugonjwa kama Gonorea au Pangusa, magonjwa ambayo awali yalionekana kama yanayotibika kirahisi, hivi sasa wataalamu wa tiba huko kwa wenzetu wamethibitisha kwamba, maradhi hayo huenda ikawa ngumu kutibika kama ilivyodhaniwa.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni huko nchini Marekani umebaini kwamba zile dawa zilizokuwa zikiaminiwa kwamba zinatibu magonjwa ya zinaa kama hayo niliyoyataja zimeonekana kushindwa kukabiliana na magonjwa hayo. Kwa mujibu wa wataalamu hao walisema kwamba huu ni wakati wa kuchukua tahadhari kabla ya hatari.

“Tishio hili sio la kubeza, kwani Gonorea ni gonjwa la pili linaloongoza nchini Marekani” Walisema wataalamu hao. Inadaiwa kwamba takriban watu 600,000 waliripotiwa kuugua ugonjwa huo kwa mwaka nchini Marekani na mojawapo ya athari walizopata watu waliougua ugonjwa huo ni matatizo katika mfumo wa uzazi, na kwa upande wa wanawake wataalamu hao walieleza kwamba, wanaweza kuwaambukiza watoto wao wakati wa kujifungua.

“Ni vyema hivi sasa watu wakachukua tahadhari ili kuepuka magonjwa hayo ya zinaa, kwani athari zake ni kubwa kuliko inavyodhaniwa” walisema wataalamu hao………….

Haya sasa, wale waliokuwa wakiona kuwa Ukimwi ni tishio, kimbembe kingine hiki hapa.

Someni hapa
:
http://www.nejm.org/doi/full/10.1056/NEJMp1112456

Naomba Mods msipeleke hii post Jukwaa la JF Doctor, kwani inahusika sana hapa MMU……..
 
mmmh!sijui ni bora mashine isifanye kazi kabisa maana tunabanwa kila kona!!!
 
Ni kweli kwa mara ya kwanza imetoka mwaka jana mwezi may kwenye Lancet Journal. Mimi wameshakuja wagonjwa kadhaa kweli wengi wanatumia dawa muda mrefu sana ndo wanarespond. Kwa sasa Ceftriaxön ndo dawa pekee ambayo wengi wao wanarespond ukichanganya na doxy au clarythromicin. Kwa hiyo human being wake up
 
Mtambuzi free drug zina matatizo sana kwenye utendaji kazi wake hasa kwenye pharmacokinetics, drud metabolism and bio-availability. iko hivi dawa nyingi sana kwasasa zina prove failure hasa antibiotics kama vile tetracycline na ampicilline. tatizo kubwa linatokana na bioavailability na crossing of some barriers especially blood-brain barrier.

sasa unakuta drug metabolism iko poor, ukija kwenye crossing ya barriers bado kuna limitation zake na sasa ukienda kwenye bio-availability na yenyewe kuna limitation zake. haya yote yanaifanya free drug ingwa ina active ingredients za kuweza kuponya ila haziwez kuwa na dose staili ili ziweze kutibu. ndio maana sasa dunia imeamia kwenye ulimwengu wa NANOMEDICINE na hapa nia ni kuongeza uwezo wa dawa kutumika kwa dose inayotakiwa kwa kulenga target tu. yani ina ongeza value kwenye active ingredients zilizoko kwenye free drug na kuzifanya ziwe na uwezo wa kwenda kwenye target na kuponya ama kuua vijidudu vya magonjwa instead ya kuzunguka mwili mzima kama zilivyo free drugs.

anyways ni shule ndefu sana nikianza hapa tutakesha but naamini utakuwa umepata idea kwann wanasema ivyo.
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri kwa wale wagonjwa sugu wanaoambukizwa huo ugonjwa mara kwa mara ndo wanalo,kama hujawahi kuambukizwa je ukitumia hyo midawa vp c fresh au tuwaache wafweee tu,auu
 
it's a rare form of gono ambayo ni drug resistant. ile ya kawaida inatibika so don't worry wakubwa wenzangu.

of course this is irrelevant to practitioners of the "no glove no love" principle
 
katika wadudu ambao ni rahisi kufa wa gono watakuwa wanaongoza. tanzania imezoeleka kidonge kimoja cha siplofloksasini ya 500mg kinawamaliza kabisa lakini wanatengeneza usugu kila leo, wenzetu waliacha kutumia siplo toka 2002 baada ya kuona wadudu ni sugu. pia wamekuwa sugu kwa penicillins na tetracycline lakini wanakufa kirahisi mno ukichoma sindano moja tu ya ceftriaxone. kwa hiyo wandugu msitishike gono is under control. ukipiga sindano usisahau kuongeza dox kwa ajili ya chlamydia.
 
Hii ni hatari na pigo kubwa sana kwa figganigga mzee wa kunyakua wale wa Kimboka, Kisuma(Sugar Ray Tmk), Ambiance Kijitonyama Afrika Sana na kwingineko
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi hujui hii nchi inaongozwa na CCM chama cha takrima?
Huyu Mike McKee pamoja na kumhonga Gin ya Cotensa siku ile ya White Party, lakini anashindwa kumwambia Invisible asiihamishe hii Post kutoka jukwaa la MMU ambapo ndio ingesomwa na wadau kama kina mzabzab mzee wa kugegeda ili ajirekebishe.... Yule hasomagi hili jukwaa kwa sababu analiogopa. tuone kama atakuja huku.........
 
Last edited by a moderator:

kwa hiyo gfsonwin unashauri kwamba ni vyema tukageukia mitishamba badala ya kutegemea hayo madawa ya wazungu.

Sijui kama nimekuelewa lakini mwalimu maana hiyo lugha uliyotumia mie nimetoka kapa si unajua mie nimesoma Ngumbaru, kingeleza noti richabo........LOL
 

sijasema hivyo manake pia hakuna tafiti za kisayansi zilizofanywa zikatosheleza kwenye field ya phytomedicine ingawa madawa haya yamekuwa yakitumika miaka mingi sana.

jambo la msingi na unalotakiwa kujua ni kwamba hata hizi convetional drugs zinatokana na miti shamba. yaani zimekuwa synthesized from medicinal plants. na hapa huwa inaangaliwa active component ya said plant na function zake, kama ikioneka active component imekuwa bonded na toxic elements basi huwa tunaextract the structure ya active component
 

Sio kwamba natoka nje ya mada...
hebu nieleze kuhusu Muarobaini, inadaiwa au niseme imethibitika kutibu malaria na maradhi mengine yapatayo 40, (hayumkini ndio maana ukaitwa muarobaini) mbona naambiwa dawa za malaria zinatokana na mmea wa cinchona (sijui kama niko sahihi, maana hizi habari ni za vijiwe vya kahawa) je Muarobaini umeshawahi kufanyiwa extract ili kupata component inayoweza kutibu japo maradhi ya aina mbili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…