Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #21
Mzee ES, sijuia kama unafahamu sheria zetu au la. Tunayo sheria ya kinga. Nilimuuliza Prof. Shivji kabla ya kuandika makala hii na hakukumbuka kama kuna wakati wowote ambapo sheria hiyo imewahi kutumika.
Labda niweke hoja yangu hapa ili watu wasome na kuelewa nilichosema badala ya kuchukua maneno juu juu tu.
Ballali apewe kinga
M. M. Mwanakijiji
KATIKA mapambano dhidi ya ufisadi ambayo ndiyo karibu yanaanza nchini, awali hatukuyatafuta bali yametutafuta sisi, yale ambayo hatukuyafuata, bali yametufuata, na ambayo ushindi wake ni lazima, kuna wakati maamuzi magumu lazima yachukuliwe.
Maamuzi magumu ambayo ni ya lazima, ya msingi na ambayo yatawezesha kushinda vita nzima badala ya pambano moja moja.
Mojawapo ya maamuzi ambayo napendekeza kwa watawala wetu wachukue ni uamuzi ambao kwa kuuangalia haraka haraka au kwa kuangalia kichwa cha habari tu, unaweza kushtua watu, ni wa kumpatia kinga ya kisheria dhidi ya mashitaka, Daudi Ballali, aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na sasa akiwa uhamishoni kwa kujitakia nchini Marekani, ili arudi na kuwa shahidi wa kwanza dhidi ya waliotuibia huko BoT.
Mpendwa msomaji, leo nitaandika vitu vigumu kidogo lakini ukinivumilia na ukiniamini kwa mara nyingine utaona ni kwa nini wazo la kumpa kinga Ballali si tu kwamba ni zuri, bali pia ni la muhimu.
Linapaswa wazo hilo kuzingatiwa hasa kama kweli tunataka kuvunja mtandao wa uhalifu wa watu wenye tai katika serikali yetu na watendaji wa ngazi mbalimbali, hususan kwenye jungu la BoT.
Kama wengi mnavyojua, mpaka sasa hakuna ‘fisadi mkubwa' ambaye ameibuka katika nchi yetu na ambaye jina lake limetangaa ndani na nje kama la Ballali, anayeaminika kuhusika kwa upotevu wa sh bilioni 133, kutoka akaunti moja (ukiondoa akaunti nyingine ambazo hazijaangaliwa bado).
Kwa wiki kadhaa sasa tangu utenguzi wa Ballali, Rais Kikwete, misumari ya tuhuma za ufisadi imeendelea kugongomewa kwenye ngozi ya Ballali na kuwambwa kwenye miti na kila anayeweza.
Si viongozi wa upinzani tu, bali pia baadhi ya viongozi wa serikalini ambao wanamnyoshea Ballali kidole cha ufisadi. Imefikia mahali kwamba wananchi wenye hasira wamemjua ‘mbaya' wao na wanaanza kujigawia mashamba ya gavana huyo mwenye jina lililochafuka.
Mimi kama ninyi, nimefuatilia kwa karibu pande zote mbili na nimebahatika kuzungumza na watu wachache wanaojua nini kinachoendelea upande wa nyumbani na upande wa huku aliko Ballali. Jambo moja ambalo dhahiri ni jaribio la kitoto la kumrundikia Ballali ufisadi wote na hivyo kufanya iwe vigumu kwake, si tu kujitokeza hadharani bali pia kurudi nyumbani, kwani sasa anaweza kabisa kudai ‘hofu ya mateso ya kisiasa' na hivyo akakimbilia uhamishoni!
Ballali (kama alivyo mwanadamu yeyote yule), atahisi kuwa usalama wake na wa mali zake vipo hatarini (kama tulivyoona) sheria za Marekani zinamruhusu kuomba ukimbizi na kwa vile Tanzania haina mkataba wa kubadilishana washitakiwa na Marekani, basi ndio itakuwa imempa sababu ya kutorudi kabisa nyumbani na mniamini, sheria za Marekani zitamkinga zaidi kuliko kumfutia viza yake.
Ni baada ya kuangalia mambo haya kwa kina na maana yake katika mapambano haya dhidi ya ufisadi nimejitolea kutoa pendekezo ambalo naamini si tu litasaidia Ballali kurudi nyumbani, lakini pia litasaidia katika kuwatambua na kuwanasa mafisadi wengine nyuma ya pazia ambao kutorudi kwa Ballali ni furaha yao na hasa kama atarudi akiwa mshtakiwa pekee wa ngazi za juu.
Hivyo, ninaamini kuna sababu ya serikali yetu kupitia Mwanasheria Mkuu na vyombo vingine kumpatia kinga ya kisheria ili Ballali arudi na kuwa shahidi muhimu katika kuwaumbua mafisadi wote waliochota fedha zetu BoT.
Kuna kinga kubwa za aina mbili ambazo Ballali anaweza kupatiwa, kuna ile kinga ya jumla, kwamba chochote atakachosema mbele ya mahakama (au chombo kitakachochunguza suala hili) hakitatumiwa kama ushahidi dhidi yake katika mashitaka yoyote yale ya kihalifu dhidi yake.
Hii ina maana kama Ballali atasema ‘waziri fulani alinijia na kuniambia tufanye hivi…ushahidi huu hapa' basi mahakama inaweza kumuangalia waziri huyo bila kutumia maneno ya Ballali kama ushahidi wa kujifunga mwenyewe.
Kinga ya pili ni ile ya matumizi, ambapo Ballali kama shahidi atapewa kinga ya mashitaka kwa kadiri ya kile anachosema. Ni kweli na haitatumika dhidi yake mahakamani.
Hata hivyo katika kinga hii, endapo sehemu ya ushahidi wake utathibitika kuwa uongo (perjury), basi yale aliyoyasema yanaweza kutumika dhidi yake.
Wataalamu wanaita aina hizi za kinga kama kinga kamili (full immunity) na ile nyingine kama kinga ya sehemu (partial immunity). Nitawaacha wanasheria wachambue aina nyingine za kinga ambazo zinatokana na ofisi za watu (kama rais, mawaziri, mabalozi), lakini hapa nazungumzia zile zinazohusiana na uendeshaji wa mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa uhalifu.
Lengo la kumpatia kinga Ballali ni kumfanya awe huru kurudi nyumbani, kutoa ushahidi wote alionao kuhusu mafisadi wote waliochota fedha zetu bila haya, pasipo yeye mwenyewe kuwa na shaka ya kuishia Keko au Maweni.
Yaani kuhakikisha kuwa kile atakachosema Ballali hakitatumiwa dhidi yake katika mashitaka ya kihalifu.
Kwa kufanya hivyo, si tu tunaweza kuwaangalia kina Basil Mramba, bali pia Zakhia Meghji, Gray Mgonja, mawaziri wengine, kina Jeetu Patel, wafanyabiashara na wahusika wengine na wale wote ambao walihusika na ufujaji mkubwa wa fedha za wakesha macho wa Tanzania kupita BoT.
Hata hivyo kuna sababu nyingine kubwa zaidi za kwanini Ballali apewe kinga. Ya kwanza ni kuwa katika sakata hili la ubadhirifu katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kama kuna mtu anayejua nini kilifanyika na kwanini kilifanyika ni Ballali.
Kwa mujibu wa Sheria ya Benki ya 2006 Ibara ya 13, kifungu cha 3(c) Gavana anaweza yeye peke yake au na maofisa wengine wa benki kutia sahihi nyaraka na mikataba mbalimbali kwa niaba ya Benki Kuu.
Gavana pekee ndiye ambaye ana uwezo huo na hivyo, kuna mengi ambayo ameyaona kwa macho yake na kuyashuhudia katika miaka karibu minane aliyotumikia BoT.
Kama hilo hapo juu ni kweli, basi kumrundikia tuhuma na kutaka kwa haraka awe mtuhumiwa mkubwa na pekee na hivyo kuwezekana kabisa kuharakisha kifungo chake si tu kutamzuia kuelezea ukweli wote na kutoa ushahidi, hasa ukizingatia asili ya tuhuma dhidi yake.
Naamini ni kinga tu, itakayomwezesha Ballali kusimama mbele ya wadai wake na kueleza ‘ukweli mtupu' ili haki iweze kutendeka.
Sababu ya pili inatokana na hiyo ya hapo juu, kwenye akaunti ya EPA ni makampuni 22 yanayotuhumiwa kuchota fedha zetu kama mtu anavyochota mchele kwa pishi.
Hata hivyo katika sakata zima la BoT ndani ya utumishi wa Ballali na akaunti nyingine zote, kuna kampuni zaidi ya themanini ambazo zimefanya vivyo hivyo na wanajulikana ni kina nani hao.
Hivyo, kumpa kinga si tu kwa ajili ya EPA, bali pia kumpa nafasi ya kufunua ni kina nani walihusika na Mwananchi Gold, Deep Green, Meremeta, Tangold na mengine mengi.
Kuna mengine sitashangaa ambayo sisi hatuyajui lakini tukimpa kinga ya kisheria tunaweza kuyajua hata yale yaliyofanywa sirini, chini ya uvungu au darini.
Si tu kujua ni kina nani walihusika, bali pia kujua ni kwa jinsi gani walihusika hadi wakaweza kufanya ufisadi huo. Endapo Ballali atapewa kinga ya mashitaka, lazima iwe kwa masharti yatakayohakikisha kuwa genge la mafisadi nchini linaumbuliwa na kufumuliwa kutoka ngazi zote.
Mtu pekee anayeweza kufanya hivyo kwa mamlaka ni Ballali. Pia kuna sababu nyingine. Anajua fedha zetu zimewekwa wapi na kina nani wameziweka fedha hizo.
Akiwa kama ofisa wa BoT, Gavana Ballali baada ya kupewa kinga anaweza kutueleza fedha zetu karibu dola bilioni moja (sh trilioni moja) zilizopotea BoT zimewekwa wapi.
Hili ni muhimu, kwa sababu hakuna furaha ya kusema fedha zimepotea, kwa sababu pesa huwa hazipotei, zinatoweka na kutumika mahali fulani.
Sh trilioni moja kupotea ndani ya miaka kama minane si mchezo. Katika mojawapo ya nyaraka za Benki ya Dunia (WB) na zile za Shirika la Fedha Duniani (IMF), na zile za taasisi mbalimbali za kiutafiti, inaonyeshwa kuwa ndani ya miaka 30 iliyopita Tanzania imepokea misaada ya karibu dola bilioni mbili.
Kama tukichukulia maneno ya Rais Kikwete kwa mabalozi hivi karibuni kuwa fedha zilizopotea BoT si za wafadhili, basi hatuna budi kukuna vichwa, kwani zilizopotea ni fedha zetu wenyewe.
Na kama alimaanisha kuwa fedha zote zilizopotea BoT si za wafadhili (zile za EPA) kama nilivyoelewa, ina maana zilizochotwa pale ni fedha zetu Watanzania.
Kwa maneno mengine, kama misaada tuliyopokea ni sh bilioni mbili na watawala wetu wakatafuna sh bilioni moja ya fedha zetu wenyewe, ina maana kama wasingetafuna kama mchwa fedha zetu, tusingehitaji msaada wa dola bilioni moja na kuwa omba omba!
Kwa maneno mengine, kama wasingetumbua pesa yetu leo hii kina Bernad Membe, wasingetutambia kuwa rais amekwenda kuomba dola milioni 698, kwani kwa kweli hatukuzihitaji!
Hivyo, kujua fedha zetu zilipo ni jambo muhimu ili si tu tuweze kuzirejesha, bali pia kuhakikisha kama zimebadilishwa na kuwa mali isiyohamishika, itaifishwe kwa manufaa ya umma na fedha zetu zirudi.
Ballali anaweza kufanya hivyo, kichocheo kikubwa itakuwa ni kinga ya kisheria ili si tu atutajie kina nani wamekwapua fedha zetu, bali pia wamezificha wapi, kwani naamini anajua!
Hata hivyo kuna sababu nyingine ya kumpa kinga. Kwa vile baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika na kashfa hizi ni watu wakubwa na wengine si tu wana nguvu za fedha, bali wanazo nguvu za madaraka, kuna haja ya kulinda usalama wa Ballali na mali zake.
Tukio la hivi karibuni ambapo wananchi walitaka kujipongeza kwa kugawana mashamba ya Ballali, ni ishara ya kile ambacho kinaweza kumkuta pindi arudipo nyumbani.
Bila kuhakikishiwa usalama wake, wa familia na mali zake itakuwa ni ndoto za Alinacha kudhania Ballali atateremka Kipawa na kukodi ‘teksi' kwenda nyumbani kwake!
Kadiri watu walivyo na shauku naye (kihalali au kimakosa), asije kurudi nyumbani akakutana na wajanja ambao ni wataalamu, wakamnyamazisha milele!
Hivyo kuna haja katika kinga hiyo kumhakikishia usalama wake katika muda wote ambao kesi itakuwa ikiendelea na bila ya shaka si yeye tu, bali pia na mashahidi wengine ambao watakuwa tayari kushuhudia katika kesi hiyo.
Hata hivyo, yeye ana umuhimu wa pekee katika kufunua ufisadi katika nchi yetu, na kutompatia kinga itakuwa ni kumtisha na hivyo kumfanya asiwe shahidi mzuri.
Jambo la kutoa kinga kwa wanaodaiwa kufanya uhalifu si geni duniani, na limetumika katika nchi mbalimbali hasa walipotaka kutokomeza uhalifu mkubwa na magenge ya kihalifu duniani.
Wamarekani walitumia mtindo huo katika kuvunja genge la mafia pale ambapo waliwakatama Mafioso kadhaa na kuwapatia kinga ili wawataje wenzao na jinsi wanavyofanya mambo yao bila ya wao wenyewe kushitakiwa.
Mfano wa hivi karibuni ni pale Bunge la Marekani lilipompa kinga bosi wa Mafia kwenye Jiji la Boston, Francis Salemme, ambaye alikuwa ametoweka na kwenda kusikojulikana, na alikuwa anajua jinsi gani baadhi ya maofisa wa FBI walikuwa wanashirikiana na kundi la Mafia.
Si yeye tu, bali pia kaka yake ambaye alikuwa Rais wa Chuo Kikuu cha Massachusetts, William Bulger, ili alieleze bunge hilo aliko kaka yake bila yeye kushitakiwa.
Kutokana na ushirikiano wake na serikali, mahakama ilimfunga kifungo kifupi hasa baada ya Selemme kuwezesha kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa ofisa wa FBI, John J. Connoly.
Hapo baadaye Selemme alijikuta kwenye matatizo mengine ya kisheria yasiyohusiana na kinga yake.
Katika mojawapo ya kesi zinazojulikana sana kutoka Marekani ni lile sakata la Monica Lewinsky na uchunguzi wa Mwendesha Mashitaka, Ken Starr.
Julai 28, mwaka 1998, Ken Starr alikubaliana na timu ya mawikili wa Monica Lewinsky, jambo lililompatia kinga binti huyo ili aseme ukweli kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton.
Makubalianao yaliyompa kinga Monica yalisaidia pia kumpa kinga mama yake na upande mwingine dada Linda Tripp, na alipewa kinga ya aina fulani ili aseme anayoyajua pasipo hofu ya kushitakiwa.
Kimsingi, hiyo ndiyo hoja yangu, kama tunataka kufahamu nini kilifanyika BoT, nani alifanya nini na kwa kiasi gani basi hatuna budi kulipa gharama hiyo kwa kumpa kinga samaki mmoja ili tutengeneze nyavu ya kuwanasa wengi wakubwa.
Kinga hii ni tishio na sidhani kama serikali itakuwa tayari kufanya hivyo, kwani si tu itafungua uwezekano wa mambo makubwa, bali watakosa mtu wa kumbebesha mzigo wote wa lawama.
Nimezungumza na mmoja wa wanasheria na hakumbuki kama kuna historia ya kutoa kinga katika Tanzania, hasa katika kesi kubwa kama hizi.
Natumaini kama hatujafanya hivyo, naamini hii itakuwa ni nafasi ya kwanza kufanya hivyo kama kweli tunataka ‘watajane'.
Sheria ya kufanya hivyo ipo. Katika mojawapo ya magazeti yaliyotoka juzi yalielezea ni jinsi gani Mwanasheria Mkuu anaangalia ni sheria gani zitamwongoza katika suala hili.
Ametaja sheria tatu kwa kadiri ya gazeti hilo, ile ya Mapato yanayotokana na Uhalifu ya 1991, ile ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya 2007 na ya Usafirishaji Fedha Kinyume cha Sheria ya 2006.
Hata hivyo kwa heshima nipendekeze sheria yetu ya Kuhujumu Uchumi ya 1984 ambayo inazungumzia kuhusu usalama na kinga ya washitakiwa na mashahidi.
Ibara ya 52, 53 na 54 zinaweza na zinapaswa kutumika. Ibara ya 53 kimsingi ndiyo inayoweza kutumika (na mabadiliko yake kama yapo) ili kuweza kumpatia kinga Ballali na hivyo kuwezesha si tu kurudi kwake nyumbani bali pia kuweza kusimama kama shahidi dhidi ya watuhumiwa wa ubadhirifu.
Hata hivyo, swali moja ambalo naogopa jibu lake ni uwezo wa vyombo vyetu vya sheria kuchunguza, kuwatia mbaroni na kuwafikisha mahakamani wahusika, ukizingatia unyeti wa suala hili.
Ukiondoa zile kesi za uhaini za miaka ya 1960 na 1980 yawezekana kabisa kuwa sakata hili litatuletea kesi katika historia ya Jamhuri yetu, kesi ambayo itatufanya tuamue kweli tunataka kwenda wapi kama taifa na jinsi ya kuwasimamia watawala wetu.
Macho yetu yanashuhudia tukio la kihistoria ambalo naomba kwa Mungu vizazi vijavyo visishuhudie tena.
Ni kwa misingi hiyo, kabla sijamaliza nipendekeze kuwa serikali itoe mwaliko rasmi kwa vyombo vyenye uzoefu wa mambo haya kama FBI na New Scotland Yard ili kusaidia katika uchunguzi huru badala ya kuwaachia polisi wetu na waendesha mashitaka kutoka Jumuiya ya Madola waweze kuendesha kesi hii ili iwe huru kabisa.
Kwa kufanya hivyo, si tu haki itatafutwa bali pia itaonekana. Sasa hivi licha ya maneno mazuri ya ahadi, baadhi ya watu nikiwemo hatuamini kuwa serikali ina nia ya kweli ya kuingia ndani na kwenye kina cha kashfa hii kubwa na iliyoumiza mioyo ya watu wengi.
Hii inachangiwa pia na usiri ambao unaendelea kuficha ripoti ya uchunguzi na pia kujaribu kutumia watu waliotakiwa kuwa wasimamizi wa sheria kufanya uchunguzi huo!
Haiingii akilini kuwa Mwanasheria Mkuu ambaye ndiye mshauri mkuu wa serikali katika masuala ya sheria aliridhia kuletwa kwa sheria ya BoT ya 2006, na kwa muda wote wa miaka minane hakuwa jasiri kufanya uchunguzi wake mwenyewe kuhusu uvunjwaji wa sheria hadi pale Waziri Meghji alipotoa ombi na uchunguzi kufanywa na chombo cha nje.
Inasikitisha kuwa Jeshi la Polisi linashirikishwa kwenye uchunguzi huu ambao madai yake yamekuwepo kwa miaka karibu kumi sasa.
Kwa maneno mengine, bila rais kuwatuma kufanya uchunguzi huo wasingeangalia ufisadi BoT na wao kama Takukuru wanasubiri maagizo kutoka juu ndipo waanze kazi zao, na kwa vile hawako huru watafanya uchunguzi na badala ya kuuweka hadharani watarudisha Ikulu ambako rais ataamua kuunda tume nyingine kuchunguza uchunguzi uliochunguzwa na tume ya uchunguzi!
Natoa hoja, tumpatie kinga Ballali kwa misingi niliyoitaja hapo juu na zaidi ili si tu aweze kurudi na kusimama kizimbani bali kutuelekeza wengine walioingia bandani mwetu na kuchukua kuku, kuwachinja na kuwakaanga humo humo bandani, huku wakirusha mifupa na manyoya nje!
Mapambano dhidi ya ufisadi yana uamuzi mgumu, huu ni mmojawapo, je, serikali ipo tayari kumpa kinga Ballali?
Kwa habari, nyaraka na taarifa mbalimbali wakati wote wa siku tembelea: http://www.klhnews.com
Niandikie: mwanakijiji@klhnews.com