Balali apewe Kinga!

Balali apewe Kinga!

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji,

Tatizo linakuja katiba yetu inampa nguvu sana rais na sisi tuna utamaduni wa patronism. Hao IGP na DPR ni watu waliochaguliwa na Kikwete kuangalia usalama wa status quo, unategemea wanaweza kufanya kitu cha maana kweli?

Si ndiyo mambo haya haya tunalalamika kila siku tume ya uchaguzi inachaguliwa na mwenyekiti wa CCM (rais) halafu tunategemea objectivity?

Mawazo yako ni mazuri karatasini lakini katika hali halisi ya Tanzania yatakwamishwa na system yetu.Halafu isitoshe unaweza kuweka precedent mbaya, kwamba watu wakafikiri ukiiba halafu ukawa so central baadaye utapewa kinga utaje wenzako halafu na wewe unapeta.Message gani tutatuma kwa wafisadi wachanga?
 
Pundit, kuna kitu kingine unachosahau.... sidhani kama AG na DPP waendeshe mashtaka haya na hata kuchunguza hawatakiwi kuchunguza.. we can do a lot better. Jaribu kufikiria suluhisho jingine..
 
Mwanakijiji,
Nadhani uko influenced sana na mfumo wa Marekani kiasi kwamba unasahu jinsi Tanzania ilivyo na inavyoendeshwa. Hayo yote unayoyasema yanafanyika na yamefanyika Marekani.

Halafu rafiki yako Kwame vipi tena? Nimezisoma txt mgsg nikacheka hadi mbavi zinauma...
 
Suluhisho ni kuwaondoa mafisadi kwenye ofisi zao wanazozitumia vibaya katika uchaguzi.Upinzani unatakiwa ku-demonstrate kwa wananchi kuwa umekomaa na kujiandaa vya kutosha kuchukua nchi wananchi watawapigia kura kama uozo huu ukielezwa vizuri.

Tatizo langu lingine ni the armed forces na intelligence units.Inaonekana kuwa eventually upinzani ukifanya niliyoyasema hapo juu utashinda.Watu wetu siku hizi wanakuja mijini sana sehemu ambazo watu wanapata habari zote, na wale walio vijijini mawasiliano yanaimarika inawa kwa kiasi kidogo.Inaonekana kama wapinzani wakitumia vizuri udhaifu huu wa CCM hizi zinaweza kuwa siku za mwisho za CCM.

Sijui kama upinzani ukishinda uchaguzi Tanzania tunaweza kuepuka ya Kenya, au watu wa majeshi na security, ambao wanaonekana kama wamewekwa kulinda CCM (not so much jeshi, this si very much so for the intelligence units) sijui kama wanaweza kuachia nchi iende kwa wapinzani kirahisi ukitilia maanani kuna madili kibao wanafanya nao.

Kwa hiyo bila ya kubadili mfumo mzima pamoja na mabadiliko ya katiba tutakuwa tunacheza tu.
 
Hapa tulipofika siamini tena kwamba suluhisho la matatizo yetu ya ufisadi yatapatikana katika mfumo wetu wa sheria zaidi ya njia ya siasa. Haya matatizo ya BoT na mengine mengi ambayo akina Slaa hawajayafunua, hayakufanyika kwa bahati mbaya; ni mambo ambayo yalipangwa ili kufanikisha malengo mahsusi ya kisiasa. Hao waliopo katika mamlaka ya kisiasa ambao ndio wanaopaswa kuwafikisha akina Balali mahakamani wanajua jinsi hizo pesa zilivyopotea na zilivyotumika. Ni haohao ndio waliomsindikiza na pengine kumficha Balali huko aliko ili kuepusha aibu, sasa leo unaposema hawahawa ndio wampe kinga Balali ili awataje mahakamani, tunasoma vitabu au tunaongelea uhalisia?

Mimi nasema hawa wataweza tu kushughulikiana kama watagundua kwamba kusuasua kwao kutawanyima kura (kula) 2010. Vinginevyo, kama wananchi vijijini wataendelea kuwachekea na kutokuona uhusiano uliopo kati ya umaskini wao na wizi wa Bot na kwingineko, basi tujue haya majamaa yatasuasua tu hivihivi mpaka tusahau! Mbona tumeshasahau Richmond na mazira mengine kibao, kwa nini unafikiri hatutasahau hili?

Mimi tena sisemi tena "miafrika ndivyo tulivyo", sasa nasema miCCM ndivyo ilivyo. Hii mijamaa haiogopi sheria, inaogopa kunyang'anywa madaraka, henceforce the supremacy of political solution over a legal one.
 
Hahahahaha...Kitila unanifurahisha sana siku hizi. But this sounds a little bit better..Mafisadi ya CCM Ndivyo Yalivyo...what do you think?
 
Nyani, yaani leo wenzenu tuna burudani tosha.. sitashangaa jamaa atajiuzulu maana kuna watu hadi wanafanya maigizo...
 
Mwanakijiji,
Nadhani uko influenced sana na mfumo wa Marekani kiasi kwamba unasahu jinsi Tanzania ilivyo na inavyoendeshwa. Hayo yote unayoyasema yanafanyika na yamefanyika Marekani.

Halafu rafiki yako Kwame vipi tena? Nimezisoma txt mgsg nikacheka hadi mbavi zinauma...

Mkuu NN,

Inawezekana ni kweli Mwanakijiji yupo influenced sana na mfumo wa Marekani. Hata kama hii ni kweli, tatizo liko wapi? Mimi nafikiri kuwa anachotaka kufanya (Mwanakijiji), ni kutoa changamoto yenye kutafuta ufumbuzi wa kudumu. Sasa kama itabidi kubadili mfumo ili ufanane na wakimarekani, ili mradi the ultimate goal linapatikana, kwangu mimi ni RUKSA!

Kwa kifupi, tunao mfumo tunaotumia na kwa miaka 46 ya uhuru, mfumo huo haujawa very effective. Pengine suala hili la ufisadi litapelekea mapinduzi ya mfumo wa sheria na katiba nchini kwetu, kitu ambacho it's long overdue!
 
Utaona kuwa pendekezo ninalotoa lina mtego mkubwa sana. Nilitumaini mtauona. Angalieni tu implication ya hiyo immunity hasa kwa mwanga ni interest ya nani inatishiwa kwa Balali kupewa kinga na kwanini serikali ya CCM haiwezi kumpa kinga..

Kudai wampe kinga ni kuwapa wao kamba ambayo ndani yake shingo zao zimetiwa kitanzi! Balali ndiyo kiti walichosimamia, kutoa kinga ni kujaribu kumwambia Balali asogee na kuwaacha waning'inie...!! Lakini, tunawataka wao ndio wakisukume hicho kiti..

think about it..
 
Hope watu watagundua mapema na kuanza kujikita mapema na kupiga kampeni kabla ya 2010,solution ni kupelekeshana nao bungeni mpaka kieleweke na hapo ndio itakuwa ground ya kuelekea kwingine lakini kama hakuna wabunge wa kutosha wenye uwezo wa kujenga hoja za uhakika tusitegemee chochote....haya kina Kitula anzeni kampeni mapema kwa wananchi na sisi tutajitahidi kuwarushia support tutakavyoweza.
 
Mwanakijiji,
Nadhani uko influenced sana na mfumo wa Marekani kiasi kwamba unasahu jinsi Tanzania ilivyo na inavyoendeshwa. Hayo yote unayoyasema yanafanyika na yamefanyika Marekani.

Halafu rafiki yako Kwame vipi tena? Nimezisoma txt mgsg nikacheka hadi mbavi zinauma...

Nyani, you might be right.. lakini nani hajawa influenced na dominant culture

- Tunaimba kama wamarekani (nina mifano mia moja na moja)
- Tunazungumza kama wamarekani
- TUnacheza kama wamarekani (leo ukicheza Sindimba watu wanakushangaa)
- Tunakula kama Wamarekani (nasikia siku hizi kuna hadi McD bongo, na sijui kama wanauza ugali na maharage)
- Tunavaa kama wamarekani
- Lafudhi yetu imekuwa kama Wamarekani (we angalia watangazaji wakitamka neno Dar-es-Salaam)
- Tunajenga na kutaka vitu vikubwa kama Wamarekani (siku hizi watu hawashindani uzuri wa nyumba bali ukubwa wake)
- Tumefikia mahali pa kutukana kama Wamarekani

Ila ikija kwenye kuiga mambo ya msingi tunajifanya sisi ni waafrika.

- Tenganisheni nguzo za Serikali - "hayo ni mambo ya Marekani"
- Fuateni utawala wa demokrasia - "sisi tuna demokrasia yetu ya kiafrika"
- Punguzeni nguvu za Rais - "hapana, hii ya kwetu ndiyo nzuri"
- Tumieni sheria kupambana na ufisadi - "hayo ni mambo ya kimarekani"
- Msiibe fedha za umma - "mbona hata Marekani wanaiba"

Sasa, nakubali niko influenced na Wamarekani because it works.. kwanini tusiige vitu vya msingi na vinavyofaa? Hatuona aibu kuvaa kama Wamarekani na wengine hadi vilemba vina bendera ya Wamarekani lakini ikija kwenye sheria tunang'aka!

Kama mmoja alivyosema hapa "only in Tanzania..."
 
Mwanakijiji
Makala yako nzuri. Ila sirikali hii tuliyonayo haina ubavu wa kuyatekeleza matakwa hayo.

Tuing'oe kwanza CCM madarakani. Watawala wajao wanaweza wakatumia huo ushauri ...inshallah.
 
Nyani, you might be right.. lakini nani hajawa influenced na dominant culture

- Tunaimba kama wamarekani (nina mifano mia moja na moja)
- Tunazungumza kama wamarekani
- TUnacheza kama wamarekani (leo ukicheza Sindimba watu wanakushangaa)
- Tunakula kama Wamarekani (nasikia siku hizi kuna hadi McD bongo, na sijui kama wanauza ugali na maharage)
- Tunavaa kama wamarekani
- Lafudhi yetu imekuwa kama Wamarekani (we angalia watangazaji wakitamka neno Dar-es-Salaam)
- Tunajenga na kutaka vitu vikubwa kama Wamarekani (siku hizi watu hawashindani uzuri wa nyumba bali ukubwa wake)
- Tumefikia mahali pa kutukana kama Wamarekani

Ila ikija kwenye kuiga mambo ya msingi tunajifanya sisi ni waafrika.

- Tenganisheni nguzo za Serikali - "hayo ni mambo ya Marekani"
- Fuateni utawala wa demokrasia - "sisi tuna demokrasia yetu ya kiafrika"
- Punguzeni nguvu za Rais - "hapana, hii ya kwetu ndiyo nzuri"
- Tumieni sheria kupambana na ufisadi - "hayo ni mambo ya kimarekani"
- Msiibe fedha za umma - "mbona hata Marekani wanaiba"

Sasa, nakubali niko influenced na Wamarekani because it works.. kwanini tusiige vitu vya msingi na vinavyofaa? Hatuona aibu kuvaa kama Wamarekani na wengine hadi vilemba vina bendera ya Wamarekani lakini ikija kwenye sheria tunang'aka!

Kama mmoja alivyosema hapa "only in Tanzania..."

Very true, MM,

Yaani hata wizi wa kimafia na cronyism ni vya kimarekani. Can I get a witness if someone sees Meremeta,Tangold,AnBen or Kagoda similar to Haliburton-type of dealing?

I think I see the mtego...which can virtually sambaratisha the entire govt. and CCM. Just imagine, Ballali is guaranteed only two years in Segerea (instead of, say,15) in exchange for explaining in detail how CCM got money from the Central Bank (in addition to ruzuku), who were the key players and how are they connected, how did Jeetu Patel and company goes without paying taxes for over years and how he robs the nation with a blessing of the top treasury officials (Mramba, Mgonja) and perhaps Ikulu. Halafu patamu zaidi, kwa vile ni karibu na uchaguzi in two years, watatokea wanaCCM watakaotaka kujidistance na mafisadi, na watataka pia kwenda Ikulu hivyo watavunja chama. Halafu labda kama ilivyokuwa historia kwa gavana wa BoT kufukuzwa kazi, labda itakuwa mara ya kwanza kwa Rais wa zamani kufunguliwa mashtaka na pengine kuswekwa lupango!! Yaani tutayarishe popcorn tu!
 
labda itakuwa mara ya kwanza kwa Rais wa zamani kufunguliwa mashtaka na pengine kuswekwa lupango!!

For some reasons I do not know, I have a feeling kuwa this is coming yaani siamini kwamba Mkapa na kundi lake watarudi kwa muumba wao bila ya kuonja jela, I know it sounds crazy lakini ninaamini kuwa iko siku itatolewa kafara tu, maana madhambi ya viongozi wetu yatazidi kupita kiasi kwamba kutakuwa hakuna jinsi, ila someone ku-pay the price na ninaaamini kwamba itaanzia na Mkapa!
 
Mkuu FM ES,

Kwa kweli hiyo siku ikija ingefaa wana JF tujipongeze na champagne ifunguliwe. Kwa watu wenye uwezo kuiba urithi wa taifa letu wakati kuna wengi wasio na uwezo (kama ulivyosema katika waraka wako mmoja kuna watu wanasubiri mishahara kwa miezi miwili)wanapata shida, I do not have a bit of sympathy. I feel violated by the person who was supposed to work for our interests.

Mimi ni mwamini, na naamini hiyo siku itakuja! Wakati Chiluba ananyolewa, BWM angekuwa anatia maji (which shouldn't have been a hard task, given the fact he literary doesn't have much hair🙂 ). Evidently yeye ni kichwa ngumu!
 
Ben alisema "wavivu wa kufikiri", inawezekana yeye alifikiri sana na kufikia kufanya aliyofanya kwa hiyo sisi tuliochoka kufikiri anaona kama hatuwezi kumfanya kitu, labda anaota. maji ya kichemka atakuja jua tumefikiria vibaya!
 
Huu moto unaowaka sasa hivi with in wananchi wa kuchoshwa na ufisadi, hauwezi kuzimwa hivi hivi na kama kuna anayeamini hivyo, kwa akina Mkapa basi hajui historia ya mapinduzi na wananchi kuchoka kuchezewa,

Just think like this, kwa mfano Balali amerudi na kutinga mhakamani unafikiri Ben na kundi zima watapona? Ni nani atakayepona? Hao kina Ben siku zao zinakaribia kufika mwisho viongozi wengi wa CCM hawasemi hadharani, lakini in private wengi wanaisubiri hiyo siku, and ninaamini kuwa it is coming!

Na very soon atajionea hasa mvivu wa kufikiri ni yupi kati yake na wananchi.
 
Kabla ya kumpa hiyo kinga ajulikane alipo ,akamatwe na kuissue statemement yake kwanza na ushahidi muhimu alionao.Kinga atapewa in return. Unajua mafia tena: " Once you are in you stay, you can't get out ALIVE!!
Lukwizi

Pia wenzangu, tuanze kulingalia hili bomba kuu la kupitishia ufisadi yaan BUNGE. Ukweli ulio wazi Tz hailihitaji, na in fact tumekuwa tukienda bila bunge sasa kwa miaka mingi N NOTHING HAS GONE WRONG, 'as far as wabunge majority are concerned' - Kamati ya bunge ya fedha na mipango imetuhakikishia kuwa hakuna shida BOT na mahesabu safi hata baada ya wabunge wa upinzani kuanza kupiga kelele. Mikataba mibovu, miswada ya ovyo, Budget na taarifa hewa za mawizara, nk nk imeungwa mkono mia kwa mia na hao wabunge wenu mafisadi!! Bado ni gharama kubwa mmno isiyobebeka na walipakodi. Mmmmm Hayaaaa!!!
Lukwizi
 
Ballali angepewa Kinga..!!!

MKJJ kinga asingeweza kupewa kwasababu alikuwa haitajiki!
Umeshaiuliza serikali kama Ballali alikuwa shahidi ama mtuhumiwa?
Maana naona unaisemea serikali wakati yenyewe bado haijasema!
KINGA WANAPEWA MASHAHIDI AMA WATUHUMIWA MUHIMU KWENYE KESI!
Yeye si mtuhumiwa wala shahidi na ndio maana tunaitaka serikali itoe tamko rasmi ama ripoti iwekwe wazi tujue yaliyojiri na kama Ballali alikuwa mtuhumiwa ama shahidi kwa siri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom