Balile: DPP, IGP, DCI lifutieni taifa aibu kesi ya Mbowe

Nadhani kwasababu kesi ipo Mahakamani, hizi makala zingekuja baada ya hukumu........Mahakamani ndiyo patamsafisha vizuri.....haki huwa inachelewa tu ila haipotei
 

Hivi Mandela alisafishwa na mahakama ya afrika ya kusini mbona alifungwa kwa kesi za kutengeneza kama hii. Kwahiyo upo radhi akina kingai watengeneza ushahidi huo wa kubumba na kutumia mahakama kumfungia wakati ukweli unajulikana siyo gaidi. Kwanini kesi is ifutwe tu na DPP. Na hao walio inging nchi kwenye aibu ugaidi wachukuliwe hatua wote walijifanya mashahidi wa uwongo hao. Ili liwe fundisho kwa polisi wengine.
 
Ni aibu kiongozi mkubwa wa police kumbe ni mwizi na anaiba hadi 260,000/-!!
 
“… milele Rais hashinikizwi …”

Hapa ndipo lilipo tatizo kubwa la Tanzania. Huenda ndio moja ya mambo ya “kijinga” aliyosema Nyerere kuwa “viongozi wetu leo wameacha mazuri yetu yote na kuchukua yale ya kijinga”.

Hadi siku tutakapoachana na dhana ya “Rais ni mungu-mtu” ndipo tutaanza kufanya mambo ya maana nchini. Vinginevyo, tutaendelea kuhangaika na mambo ya ovyo sampuli hii siku zote. Bila shaka Mbowe ashukuru sana suala lake limepata international limelight. Na kwamba hii si awamu ya tano. Ama sivyo hatma iliyokusudiwa kwa Lissu 2017 ingemhusu mapemaa.
 
Kesi inajadiliwa wakati wowote na watu wowote, isipokuwa na jaji tu au prosecutor.
Ni ushamba kufikiria kesi ikiwa mahakamani haiwezi kujadiliwa kupitia redio, TV, makala magazetini n.k
Nadhani kwasababu kesi ipo Mahakamani, hizi makala zingekuja baada ya hukumu........Mahakamani ndiyo patamsafisha vizuri.....haki huwa inachelewa tu ila haipotei
 
Niliandika haya muda kidogo. Ramadhani Kingai kuna vyeo alitaka wakati wa JPM. Hii kesi yeye na Sirro wana jambo lao wanalijua. Sirro anamtaka Kingai kwenye nafasi moja juu ya polisi. Hesabu zinagoma kwa sasa.
 
Hata mdomoni?
 
Ubishi wenye ujinga ndani yake kama wako huu ndo unatuletea umasikini hapa nchini !!! Kwa nini Mzee Rugemalira ameachiwa huru,huku tukijua kesi yake ya Escrow ilifanya hadi wazungu kurunyima hela za Maendeleo?
Vijana wa kundi la Uamsho,nao wameachiwa huru karibuni kwa makosa ya kudhaniwa kama ya Mbowe!!!
Hii Kesi ya Mbowe kwa hatua za awali tuu za kusikiliza ni vituko na vingi kama vya kubuni.
 
haya sifa za kuajiriwa kama judge zinataka elimu ipi???

elimu haihusiki kabisa kwenye reasoning ya mtu.kama huamini hujastaarabika bado,tena wewe ni hatari kuliko hawa polisi failure.
Waulize polisi kwanini vijana wenye division 1,2 na 3 wapo lakini wao wanataka wenye division 4
 
Naunga mkono hoja hii
 
Mahakama ya nchi gani?
 
Kesi inajadiliwa wakati wowote na watu wowote, isipokuwa na jaji tu au prosecutor.
Ni ushamba kufikiria kesi ikiwa mahakamani haiwezi kujadiliwa kupitia redio, TV, makala magazetini n.k
Acha niendelee kubaki mshamba tu,nijuavyo ukweli unapatikana Mahakamani na siyo vijiweni
 
Jaji Mutungi anataka usuluhishi kuhusu mikutano, Sirro anasema mikutano ya ndani inatia mashaka japo CCM kila kukicha wanafanya! Anasita kusema wazi kuwa hataki wapinzani wafanye! Kwake kukamata ni muhimu kuliko suluhu! Ulichokiandika Sirro hatakubaliana nacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…