Wacha wee....
Hatimae umetoa reference ile ile ya UK Financial Regulator....
Acha kuruka ruka ngugu mtetezi wa mikopo ya mabeberu!!
Ulisema walioendesha hiyo show ni IMF, nami nikakuambia ni UONGO! Nilikuambia Credit Suisse walikuwa wanachunguzwa na UK Financial Regulator, US Financial Regulator pamoja na Swiss Financial Regulator kwa sababu mkopo waliotoa ulikiuka misingi ya money laundering pamoja na kugubikwa na corruption!!!
Na ni hao ndio walifikisha kesi mahakamani! Hapa unajifanya kuleta reference, halafu unaacha
details za kilichopelekea CS kupigwa faini kwamba:-
View attachment 1989187
Sasa hao FCA ni IMF hao? We jamaa vipi wewe?
Na ili kuendelea kutetea uongo wako, hoja za msingi kwenye hiyo ripoti ya FCA umeziruka, na moja wapo ni hii hapa:-
Haya... onesha kwenye hiyo ripoti ni wapi wamesema Credit Suise hawakuwa approved na IMF kutoka mkopo! Au weka hiyo ripoti hapa tuone popote ilipotajwa IMF!
Halafu unaniambia kwamba Credit Suisse walisamehe $200M wakati nilishasema tayari kwamba:-
Mbona unaruka ruka wewe?!
In short ni kwamba hukuwa ni details... ulikurupuka kuongea kitu ambacho hukutafiti huku ukibaki kujimwambafai kwamba eti u mtaalamu wa Public Finance, na kuleta porojo za namna gani IMF hutoa mikopo!!
Mjadala wetu ni wapi tumeongelea deni letu la taifa? Kitu ambacho niliku-challenge ni pale ulipoonesha kwamba it's okay kukopa private banks kwa sababu hizo banks huwa hazitoi mkopo kwa nchi maskini bila kupewa hidhini IMF Approval...
Na ukaendelea kudai kwamba, hata JK na Mkapa sio kwmaba hawakutaka kukopa kwa private banks bali walikuwa hawakupesheki!
Hapo ndipo nikakuambia suala la kukopa private banks sio la kuonea fahari kwa sababu mikopo ya hawa jamaa inaambatana na janja janja nyingi including corruption!
Na nikakupa hadi mfano wa serikali ya JK ilipokopa over USD 600 Million Stanibic ambayo na yenyewe walimwingizia middle man zaidi ya Shilingi 10 Billion za Tannzani!
Au unaeleza hayo katika harakati zako za kutetea hiyo mikopo iliyochukuliwa?
Sasa inahusiana na mjadala wetu? Btw, unadhani TANESCO wanaweza kuchukua mkopo bila guarantee ya serikali?! Na kwa akili yako, TANESCO wakishindwa kulipa unadhani nani atakuwa responsibile?
Look at you...
Eti hizo kampuni zilienda kukopa bila idhini ya serikali na hapo hapo serikali ikawadhamini?!
Unadhamini vipi kitu ambacho hujakibariki? Hivi unajua unachokiongea wewe?
Hujui unachokiongea...
Angalau ungesema "...wewe unaenda KUKOPA"!
IMF wana-deal na serikali na sio taasisi inayokopesha!!
Na ndo maana nikakupa mfano wa ANY LENDER VS ANY DEBTOR!
As long as Credit Suisse ndio walitoa mkopo, hapo ni CS ndio walikuwa na wajibu wa kufahamu loan portfolio ya Mozambique ili kujiridhisha endapo wataweza kulipa, lakini sio Credit Suisse kutaka approval ya IMF kabla ya kutoa mkopo!!
Na hiyo sababu ya ANY LENDER VS ANY DEBTOR ndiyo iliwaingiza (sio kwenye kesi) IMF kwa Msumbiji!
Kwamba, IMF walitaka kutoa mkopo kwa Msumbiji lakini uchunguzi wa named Financial Regulators ukafichukua mkopo waliochukua Msumbiji kwa Credit Suisse! Mkopo huo wa CS hukufahamika na IMF, na ndo maana wakaamua ku-cancel mkopo waliotaka kuwapa Mozambique!
Ni nani waliosema hivyo? Ni IMF, au?!
Achana na habari za IMF kwenye hii mada kwa sababu unachanganya madesa! Na hizo sio taratibu za kimataifa za kukopesha nchi maskini bali ni taratibu zinazo-apply duniani kote!!
However, as a banker, kuna more risky customers! Sasa unaokutana na mteja wa aina hiyo, unatakiwa kuwa makini zaidi katika kufuata operation procedures!!
Kwa kuchanganya changanya mambo tu, u hodari!
Yaani CEO wa Private Bank afukuzwe kazi kwa sababu hakufuata taratibu za IMF?!
We jamaa acha kuongea mambo usiyoyajua!! Fine, umesema wewe ni mtaalamu wa Public Finance lakini HUJUI LOLOTE KUHUSU MAMBO YA KIBENKI!!
Huyo CEO atafukuzwa endapo taratibu hazikufuatwa, including kufanya DUE DILIGENCE!!
Uzuri wa mabenki ni mmoja! Kama umefuata taratibu zote, kisha ukatoa mzigo lakini ukaishia kwa wajanja! Au finally ikagundulika mliowapa pesa ni matapeli... hapo bankers hawawezi kuwa held responsible unless kama hawakufanya due diligence ya kutosha!
Kwamba, watu wanaweza kuja na docs ZOTE zinazoonekana ni halali, kwa mfano kutoka Serikali X! Hapo ukifuata taratibu zote na ukatoa mzigo kwa kutumia hizo docs... utakuwa free kwenye kipengele cha kufuata taratibu!
Lakini je, ulifanya Due Diligence kujiridhisha mamlaka husika zinahusika na hizo docs zinazoonekana ni legit?
Back in the days iliwahi kutokea issue kama hiyo pale NMB Morogoro Rd Branch!
Wajanja wameenda pale na docs ZOTE HALALI kutoka Wizara ya Afya! Jamaa wakafungua akaunti kama signatories wa wizara! Ulipoingizwa mpunga tu, jamaa wakatoa mzigokutoka kwenye akaunti, na wakapotea!
Hapo NMB Morogoro Rd Branch walifuata taratibu zote za kufungua akaunti lakini hawakufanya due diligence kujiridhisha kwamba zilitoka kwenye mamlaka halali!!
Kuna "Wajanja" wengine wanaitumia sana BRELA kupiga mpunga!! Kwa mfano, watu wanaweza kwenda benki na legit docs za kampuni X maybe inayofanya kazi na serikali! Hapo wataenda hadi na Docs za BRELA kuthibitisha existence ya kampuni husika!
Sasa bankers wakiwa makini kwenye due diligence, wanaweza kukuta ni kweli kampuni ipo, na imesajiriwa BRELA lakini walio mbele yako sio TRUE OWNERS wa kampuni husika! Sasa kwanini wamekuja kufungua akaunti ya kampuni ambayo sio yao?
More likely, watakuwa wamepiga cheque ya kampuni husika, na wanajua ili kutoa pesa kutoka kwenye hiyo cheque, ni LAZIMA wafungue akaunti yenye jina lililopo kwenye cheque (of that company)!
Naona unageuza gia angani...
Kwahiyo sasa ni "...nchi maskini kwenda kukopa bila ya kuongea na IMF" na sio tena:-
Yaani umeshasahau ulisema hata hizo private banks za mabeberu hazikopeshi nchi maskini bila IMF kufanya yao, halafu hapa unapinduka na kusema nchi maskini haziwezi kukopa kwenye private banks bila IMF kufanya yao!!
Na hata kwenye post yako hii umesahau ulisema:-
Hivi hiyo sentensi inamaanisha nini kama sio private banks kutokopesha nchi maskini bila kufuata miongozo ya IMF?
Halafu few hours ago, ulileta fix zingine kwamba mapato makubwa ya IMF yanatokana na mikopo wanayochukua kutoka private banks!
Kituko ni pale unapojaribu kuaminisha watu kwamba MWENYE PESA YAKE/CREDITOR, yaani Private Banks, hawezi kukopesha bila kupewa idhini DEBTOR wake wakati huyo Creditor wala haendeshi shughuli zake chini ya mamlaka ya huyo anayemdai!
Ona fix ulizokuwa unapiga watu mwanzoni kabla sija-reveal uongo wako na hatimae ukabadilika na kuanza kuongelea habari za FCA!!
Hebu twende taratibu ndugu mwananchi...
Credit Suisse wamepewa za uso na IMF au FCA, pamoja na other finacial regulators (SEC & FINMA)?
Endelea tu kuchanganya madesa....
Btw, ni nani alikudanganya "...private banks wakaja na Brady Bonds"?!
Hivi unafahamu huyo ni Brady ni nani?!
FYI, kwanza hiyo crisis haikutokea in 70's bali in 80's!!
Na Brady Bond ni matokeo ya ku-fail mpango wa awali ambao ulinzishwa na James Baker, na program yenyewe ilikuwa inaitwa Baker Plan!!
Failure ya Baker Plan, iliyokuwa imeletwa na James Baker during Reagan Administartion, ndiyo ikaleta Brady Plan during Bush Sr Administration!
Both, James Baker na Nicholus Brady at the time walikuwa Treasury Secretaries. Hivyo basi, Brady Bond zilizotokana na Brady Plan ilikuwa ni mpango wa Serikali ya Marekani na sio private banks!!
Umebaki tambo tu lakini HUJUI LOLOTE....
Na hivi unakumbuka ulisema eti nakupotezea muda ingawaje hujaacha kuni-quote?!
Hatimae nimebaini ni wewe ndie unanipotezea muda manake mara kwa mara unaleta mambo tofauti lakini unayaleta bila kuwa na ufahamu nayo!!
So, stay blessed, coz' you're the one now wasting my time!
Jifunze kwanza kusimama kwenye hoja moja, na ukija na hoja tofauti basi iwe inalenga kukazia hoja ya msingi iliyobeba mjadala!!
On top of that, unapoleta hizo hoja tofauti basi uwe na uelewa wa hicho unacholeta! Sio tu unampelekea bosi chai, njiani unasikia kwa mbali watu wwanazungumzia Brady Bonds na hatimae unafanikiwa kudaka mawili matatu, kutoka kwao, basi hapo hapo unakurupuka kuja hapa kabla hujawa na uelewa whicho ulichosikia!!