Kuna jambo limenishangaza jana la kitendo cha ball boys kuiba begi la golikipa wa TP Mazembe na kukimbia nalo.
Kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha Rais wa Yanga Hersi Said ambaye pia ni kiongozi anayetafuta heshima Afrika akiwa anashikilia cheo cha Mwenyekiti wa Taasisi ya Vilabu kuwapongeza ball boys hao. Hii inaleta picha gani kwa mpira wa Afrika?
View attachment 3193255
Kesho keshokutwa hawa ball boys watatumika kuvamia viwanja na kuwamwagia "maji" wachezaji wa timu pinzani. Watatumika kuondoa upepo kwenye mipira na uhuni mwingine ambao akili yangu bado haijapevuka kubuni.
NYONGEZA: Sisemi msifanye uhuni ila kuna njia za kufanya uhuni bila kuonekana washamba.