Balozi Ahmed Haggag: Bara la Afrika linahitaji kuacha utegemezi wa nje na kujiamini

Balozi Ahmed Haggag: Bara la Afrika linahitaji kuacha utegemezi wa nje na kujiamini

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
IMG-20260824-WA0091.jpg.jpeg
CAIRO, Misri: Balozi Ahmed Haggag, Mshauri wa Umoja wa Waandishi wa Afrika, amewataka Waandishi wa Habari kuongoza kampeni ya kuitangaza Afrika na kukuza uchumi wake kwa kutumia rasilimali zake wenyewe.

Akizungumza na Waandishi wa nchi mbalimbali za Afrika Jijini Cairo, Balozi Haggag amesema ni wakati wa bara hilo kuacha utegemezi wa nje na kujiamini.
IMG-20260824-WA0097.jpg.jpeg

IMG-20260824-WA0100.jpg.jpeg
"Afrika ina maeneo mazuri na nafuu kuliko Ulaya kwa nini tupeleke fedha zetu nje?" alihoji Balozi Haggag.

Akitoa mfano wa kukosa visa ya kwenda Ulaya licha ya kumiliki pasipoti ya Kidiplomasia amesema hiyo ni moja ya changamoto zinazowakabili Waafrika.

Amesisitiza kuwa badala ya Waafrika kusafiri kwenda Ulaya, wanapaswa kuitangaza Afrika wenyewe.

"Tuwekeze katika vivutio vyetu, hoteli zetu na utamaduni wetu," alisema.

Balozi alisema ni aibu Afrika kuendelea kuagiza nje vitu vinavyoweza kutengenezwa ndani ya bara.

Balozi Haggag aliongeza kuwa Afrika inapaswa kutumia vijana na wataalamu wake kujenga teknolojia.

Alitaja mifano ya Misri na "Smart Village", Nigeria na "Yaba Silicon Valley" na Afrika Kusini kama ushahidi kuwa Afrika ina uwezo wa kujitegemea katika uchumi wa kidijitali na akili bandia.

Alimalizia kwa kusema kuwa endapo Afrika itakuwa na mashirikiano katika kiuchumi na kiteknologia inaweza kutoa ajira kwa vijana na kushindana na dunia.

"Tukiungana kiuchumi na kiteknolojia, tutatoa ajira kwa vijana wetu na kushindana na dunia nzima".

“Kwa nini tununue magari ya Japan na Ufaransa wakati Nigeria inatengeneza yake? Kwa nini tusitengeneze chokoleti yetu wakati Cameroon inayo?" aliuliza Charles Ndi Chia, Rais wa Chama cha Waandishi wa Habari cha Cameroon.

Charles aliita tabia hiyo "kuchukua makaa Newcastle" kwenda kununua nje kitu ulicho nacho nyumbani. Alisema Waandishi wana jukumu la kubadilisha fikra za viongozi na wananchi ili wawekeze ndani.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Umoja wa Waandishi wa Afrika kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Udhibiti wa Vyombo vya Habari la Misri kwa lengo la kukuza maendeleo ya bara.
 
Back
Top Bottom