Balozi Ami Mpungwe, kuwadi maarufu wa soko huria aliyepitwa na wakati

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Balozi Ami Mpungwe ni moja ya makuwadi maarufu wa soko huria akianza awamu ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete. Ni mtu ambaye anajihisi ana ukubwa wa tembo, na kuna watu wenye akili kama zake wanamuona gwiji.

Alianza kufanya ukuwadi wa Tanzanite yetu wakati akiwa balozi wa Tanzania Afrika Kusini. Baadae akaingia kwenye ukuwadi wa viwanda vya sukari.

Aliingizwa katika Bodi kadhaa za kampuni ili awe anapenya penya kwenye korido za watawala kwa kuwa huwa anawaahidi kwamba yeye anajuana na watu, hivyo mambo hayatakwama.

Juzi nimemuona katika sakata la sukari, hakika kuwadi amechoka haswa, kimwili ana mvi mpaka kwenye kope, hoja zake zimechakaa.

Hakuna lenye mwanzo lisilo ncha
 

Mhukumu kwa matendo yake. Siyo kwa mvi zake mpaka kwenye kope. As you say.

Old age is a privilege denied to many. Ukifika hata nusu ya umri wake mshukuru Muumba wako.

Again, mhukumu kwa matendo yake.
 
Mhukumu kwa matendo yake. Siyo kwa mvi zake mpaka kwenye kope. As you say.

Old age is a privilege denied to many. Ukifika hata nusu ya umri wake mshukuru Muumba wako.

Again, mhukumu kwa matendo yake.
Katika Tanzanite yeye ndiye alikuwa upande wa wanyonyaji
 
mtu mzima mwenye heshima zake, halafu anapotosha mambo kwa makusudi kabisa ni fedheha na hatua mbaya sana ya ukomo wa fikra mbadala 🐒
 
😄 huyu pesa ipo mzeendomqna anatuona mambugila

Ova
 
Picha tafadhari

USSR
 
Kifupi namuunga mkono Mzee na mwanadiplomasia nguli Ami Mpungwe
 
Hivi ww mwenye jina la tusi, unapotumwa kutetea mafisadi wanatuibia pesa za kutosha, na ww unaona ni haki yao kuiba.?Hakika utalaaniwa ndugu.

Yaan huyo msomali mwizi ametuibia pesa ya kutosha, ww unatumwa, kunawaponda wazee wenye hekima zao.? Hakika njaa ni mbaya sana. Lakin kila jambo lina mwisho na wahuni na wezi wote watabainika na watashughulikiwa.
 
Kwa hayo yote uliyoyaeleza,ni kipi amekuudhi sana?
 
Ami Mpungwe Balozi, mmoja wa watu waliokuwa karibu na late Mandela na Mkapa ..acha ANUKIE!
 
mtu mzima mwenye heshima zake, halafu anapotosha mambo kwa makusudi kabisa ni fedheha na hatua mbaya sana ya ukomo wa fikra mbadala 🐒
amepotosha kivipi, semeni ukweli la sivyo ni majungu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…