benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Picha: Balozi Dkt Marten Lumbanga
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Dkt Marten Lumbanga amesifu ujasiri na uwazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uongozi kiasi cha kukaribisha mawazo huru kutoka vyama vya siasa kwa manufaa ya nchi pamoja na kuruhusu vyama vya siasa vifanye mikutano ya hadhara kwa kuwa wanaokutana ni Watanzania.
Balozi Lumbanga alisema hayo nyumbani kwake Masaki Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wa kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Kiongozi huyo mzaliwa wa Mlimba mkoani Morogoro alihoji nchi ilinufaika na nini kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na je hilo ndilo taifa lilihitaji katika mazingira ya sasa.