The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Duuh, mimi sikuwahi kufikiri wala kudhani kabisa kuwa kamanda wa anga na mwanaharakati wa siasa za mageuzi Tanganyika ndugu Freeman Mbowe kuwa ni shetani wa CCM - kijani aliyejificha kwenye gwanda la khaki la CHADEMA...!!
Katika VideoAudio Clip hiyo, Balozi Dr. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA kwa miaka 12 (2003 - 2015) na kufanya kazi chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe anafichua siri ya vikao kati ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CCM (Taifa) ambaye pia ni Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan...
Dr Wilbroad Slaa anasema, amepewa taarifa na vijana wake ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) juu ya kikao kati Rais Samia/CCM na Freeman Mbowe kujadili namna atakavyosaidiwa kushinda uenyekiti...
Anaendelea kusema kuwa, Rais Samia amekubali kumuongezea pesa Freeman Mbowe ili kugharamia mikakati ya ushindi wake na kwa hiyo wajumbe wajiandae kula pesa za bure za Samia Suluhu Hassan...
Aidha ameitahadharisha kambi ya Tundu Lissu kufahamu kuwa, Freeman Mbowe atapata msaada toka TISS, polisi na UVCCM wengi wataingia kama wajumbe wapiga kura na watavalishwa magwanda au jezi rasmi za CHADEMA...
Je, wajumbe 1,200 watashindwa kufahamiana na kudhibitiana ndani ya ukumbi? Timu Tundu Lissu fahamuni hili, jiandaeni kwa mapambano. Fanyeni kama TLS walivyofanya kumpigani Boniface Mwabukusi na kuibuka mshindi wa u - Rais wa TLS