Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

View: https://youtu.be/lU_QbyAtMUM?si=Qdt19WOd_IGi962F

Duuh, mimi sikuwahi kufikiri wala kudhani kabisa kuwa kamanda wa anga na mwanaharakati wa siasa za mageuzi Tanganyika ndugu Freeman Mbowe kuwa ni shetani wa CCM - kijani aliyejificha kwenye gwanda la khaki la CHADEMA...!!

Katika VideoAudio Clip hiyo, Balozi Dr. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA kwa miaka 12 (2003 - 2015) na kufanya kazi chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe anafichua siri ya vikao kati ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CCM (Taifa) ambaye pia ni Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan...

Dr Wilbroad Slaa anasema, amepewa taarifa na vijana wake ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) juu ya kikao kati Rais Samia/CCM na Freeman Mbowe kujadili namna atakavyosaidiwa kushinda uenyekiti...

Anaendelea kusema kuwa, Rais Samia amekubali kumuongezea pesa Freeman Mbowe ili kugharamia mikakati ya ushindi wake na kwa hiyo wajumbe wajiandae kula pesa za bure za Samia Suluhu Hassan...

Aidha ameitahadharisha kambi ya Tundu Lissu kufahamu kuwa, Freeman Mbowe atapata msaada toka TISS, polisi na UVCCM wengi wataingia kama wajumbe wapiga kura na watavalishwa magwanda au jezi rasmi za CHADEMA...

Je, wajumbe 1,200 watashindwa kufahamiana na kudhibitiana ndani ya ukumbi? Timu Tundu Lissu fahamuni hili, jiandaeni kwa mapambano. Fanyeni kama TLS walivyofanya kumpigani Boniface Mwabukusi na kuibuka mshindi wa u - Rais wa TLS...

Huyu msaliti a upadre mpeleke mahakamani atoe ushahidi, mbuzi takataka
 
🤣 mwanzoni nilikuwa sielewi naona mapichapicha. Baada ya tetesi toka Twitter kuwa kuna mtu kalambishwa asali ya 12B nikaelewa picha nzima 🤣🤣. Na bado mwamba anataka mabilioni mengine ya kubustia 🤣🤣🤣🤣🤣

Tuambiane ukweli, Ni vigumu kwa mtu yoyote kukataa 12B+
Story za kwenye vijiwe vya boda boda.
 
We ushaona mkakati wa ushindi unapangwa hadharani hivyo.

Hapo 80% ya diaspora wana sikiliza sio kwa kujali bali wako vitandani wanatafuta usingizi. Rant kama hizo za mambo ya nchi yao zinaliwaza stress.
Kina Samora Michel wa Msumbiji na wenzake harakati zao kuiokomboa nchi yao toka kwa ukoloni wa Kireno zilikuwa zinafanyika wakiwa nje na wenzao wengine wakiwa ndani ya nchi...

Tena wakati huo teknolojia ya mawasiliano ilikuwa duni sana ukilinganisha na sasa...

Kwa leo, ishu nyeti kabisa inaweza kufanyikia ikulu ya magogoni DSM lakini ikaibukia London Uingereza...!

Kuweni makini. Msifikiri hamjulikani...
 
Huyu msaliti a upadre mpeleke mahakamani atoe ushahidi, mbuzi takataka
Usimchukulie poa Dr. Slaa wewe hao anaowasema usalama wa taifa huenda ni sehemu yao maana najua wako level tofauti tofauti lakini mama lazima alifanye hilo ili akipita Mbowe ni rahisi kumwamuru aweke mgombea dhaifu na atakayefuata matakwa ya Samia.

La fomu moja ni kama kalifanikisha sasa anataka na upinzani uwe dhaifu ili asipate shida kwenye kampeni maana ni mweupe sana hoja za kukubalika kwa wapiga kura.
 
We ushaona mkakati wa ushindi unapangwa hadharani hivyo.

Hapo 80% ya diaspora wana sikiliza sio kwa kujali bali wako vitandani wanatafuta usingizi. Rant kama hizo za mambo ya nchi yao zinaliwaza stress.
Hizo tetesi zimeanzia Twitter na Dr Slaa kazungumzia hilo suala, mtu kalambishwa asali ya 12B+ lazima pachangamke, 12B sio pesa ya kitoto 🤣
 
Kina Samora Michel wa Msumbiji na wenzake harakati zao kuiokomboa nchi yao toka kwa ukoloni wa Kireno zilikuwa zinafanyika wakiwa nje na wenzao wengine wakiwa ndani ya nchi...

Tena wakati huo teknolojia ya mawasiliano ilikuwa duni sana ukilinganisha na sasa...

Kwa leo, ishu nyeti kabisa inaweza kufanyikia ikulu ya magogoni DSM lakini ikaibukia London Uingereza...!

Kuweni makini. Msifikiri hamjulikani...
Mkuu embu jiunge sauti ya wa Tanzania kama bado.

Hapo room ikifunguliwa utaona watu kadhaa wanaomba kuongea. Baada ya masaa kadhaa wakiitwa japo bado wapo ila washambonji kitambo. .

Wana kundi lao la wakereketwa wachache, halafu moderator ni madiketa hao Kim Jong Un (afadhali).

Sasa audio kama hiyo ukiipiga kwenye mkutano wa CDM na kuwaambia wapiga kura wa mkutano mkuu, hawa ndio walio nyuma ya Lissu wakiongozwa na Dr Slaa si umeshamaliza kazi mapema.

Ni watu wanaojifurahisha tu
 
Nimecheka kwa nguvu vibaya, eti siasa chafu cdm ndio waanzilishi, kwanza una umri gani? Kuelekea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini wa 1995, makada wa ccm na Nyerere akiwa hai, walikuwa wanazunguka mitaani wakionyesha video za vita ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, wakisema mkichagua wapinzani wataleta mauaji kama hayo. Sasa endelea na upotoshaji wako mwingine kwenye waasisi hao wa siasa chafu hapa nchini.
Wamachame wamevurugwa sana na counter attack ya Lissu kila mmoja anabwabwaja kivyake utafikiri wamekunywa maji ya chooni.
 
Mbona yeye alipewa na ubalozi akahongwa!
Simtetei huyu lakini walau yeye alifanya hadharani na kila mtu aliona, mwamba (kama madai ya Dr. Slaa ni ya kweli ) kafanya gizani, watu hawaoni and hence jambo alilolifanya ni OVU mbele ya jamii.
 
Back
Top Bottom