Balozi Kagasheki: TCRA Mnachekesha

Balozi Kagasheki: TCRA Mnachekesha

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,096
Reaction score
8,234
Anaandika Balozi Khamis Sued Kagasheki kupitia ukurasa wake wa Twitter na ninamnukuu;

Humphrey siyo rafiki yangu. Pia siyo adui yangu. Sikuwahi kuketi popote na yeye kwa maongezi. Mara moja tu niliongea nae kwa simu kuhusu jambo lililo mhusu mwanachama mwenzetu na Boss wake (Bashiru) alikuwa kalivalia njuga. Inasemekana zipo tuhuma zinazo mkabili na Chama chetu hakijatoa hukumu dhidi yake mpaka kisikie utetezi wake. Kingeweza kumchukulia hatua bila hata kufuata taratibu kama tulivyo ona huko nyuma. Najiuliza, TCRA kabla ya hatua zao dhidi ya Polepole, walimpa fursa ya kujieleza? Alisikilizwa? Alisema nini?

Nimeusikiliza mlolongo wa tuhuma dhidi yake lakini nikazidi kujiuliza ‘na ikawaje akapewa leseni?’ Vitu vingine TCRA ilipaswa ivijue kabla ya kutoa leseni. Pamoja na yote “Darasa” lake halikuwa hewani siku moja au mbili kwa uchache wa siku, kweli TCRA walikuwa bado tu hawajaona kwamba leseni yao haikuwa katika mikono salama? Niwambie tu, TCRA mnachekesha.

Huu uadilifu mnaupata wapi. Awamu ya tano mmetoa leseni kwa so-called wanaharakati huru wakitukana, kudhalilisha Wazee na Wastaafu wa Taifa letu. Mpo kimya. Maongezi ya Watanzania yamedukuliwa na kuwekwa hadharani.Mpo kimya. Leo mnasimamia maadili. Really? Mimi simtetei Humphrey kama Humphrey. Kuna maswala ya msingi ambayo ni zaidi ya mtu. TCRA if you want to be correct so be it. We aren’t interested in half baked, half cooked dishes.
 
TCRA wenyewe ni kama wanasiasa tu wenye kilemba cha profession tofauti, siku zote huendana na midundo ya mtawala aliyeko madarakani ili kumlinda na sio profession yao.

Kuwashangilia uamuzi wao wa leo umekupendeza ni upofu tu, kesho hao TCRA wakikukaanga usinune, kwasababu wakiwaumiza wengine huwa unachekelea.
 
Kama Katiba ya sasa tu inakanyagwa, nini kitazuia hiyo katiba mpya kukanyagwa? Ishu ni watu kama watu kubadilika!
Hiyo Katiba Mpya itaweka mipaka na majukumu ya kila mmoja kwenye nafasi yake, na adhabu gani atapata akienda kinyume.

Sio kama hii ya sasa Rais yuko juu ya Katiba kwa kuwa inamruhusu afanye chochote na asishtakiwe popote.

Nashangaa vitu vidogo kama hivi hamvielewi pamoja na ujuaji wenu.
 
Hiyo Katiba Mpya itaweka mipaka na majukumu ya kila mmoja kwenye nafasi yake, na adhabu gani atapata akienda kinyume.

Sio kama hii ya sasa Rais yuko juu ya Katiba kwa kuwa inamruhusu afanye chochote na asishtakiwe popote.

Nashangaa vitu vidogo kama hivi hamvielewi pamoja na ujuaji wenu.
Mkuu katiba hata ziwe nzuri vipi kama watu hawana nia ya kuzifuata na hawazifuati, Upinzani huko mlitengeneza katiba nzuri sana, utamu wa madaraka ukawafanya watu wachomoe baadhi ya vifungu kwa manufaa yao! Tatizo ni watu na siyo Katiba
 
Back
Top Bottom