Balozi Kagasheki: TCRA Mnachekesha

Nchi yetu hii. Kweli Lawrence Masha alikuwa Waziri na Mzee wetu Balozi Kagasheki Hamis
akawa msaidizi wa Waziri. Umri, elimu exposure. Kweli Masha anamtuma kaka yake. Jk hukutenda haki hata kidogo
 
Yaani Africa nzima ni moja na tabia zao ni moja

Rais akikanyaga katiba na wa chini wote wataogopa na kufanya anavyotaka
Na Rais ana mamlaka makubwa ya kumfanya awaambie wa chini la kufanya

Tuliona hawa hawa waliokuwa awamu ya 5 jinsi walivyotupelekesha na kukubali kuvunja sheria zote huku wakikingiwa vifua na yule

Leo kaja Rais mwingine na beat tofauti wao wanacheza na yeyote mradi wasikie mdundo tu
 
Balanced observation but with lots of fragility he has been kozikozii, Tareirota kwako Balozi, Thank you for daring.
 

Kwa jinsi walivyomlinda yule MWANAHARAKATI HURU [ Musiba] wa Magufuli akitukana watu hovyo kwa kutumia media hiyo hiyo anayotumia Polepole,TCRA hawana moral authority ya kumfutia leseni Polepole !! Hii ni wazi kuwa serikali inatumiwa na ccm kutaka kumthibiti Polepole ; wameisha ona kuwa ccm kumuadhibu kwa hayo wanayoyaita makosa ya uchochezi hayana ushahidi na yanaweza kukiweka chama tawala mahala pabaya. Polepole kama tujuavyo sio mwanachama wa kawaida bali alikuwa kiongozi aliyekijua chama kwa undani akiwa katibu mwenezi hivyo hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake ni lazima zitafakaliwe kwa kina!!
 
TCRA waliufyata kwa Musiba na wanatumikishwa kama watumikishwavyo mamluki wengine
 
Kama Katiba ya sasa tu inakanyagwa, nini kitazuia hiyo katiba mpya kukanyagwa? Ishu ni watu kama watu kubadilika!
Tatizo la msingi siyo katiba, ni watu.
Ni lazima kuwepo utaratibu wa kuwashughulikia watu wanaotenda kinyume na haki, maadili, sheria na kanuni kwa kutegemea madaraka waliyonayo kwa wakati husika.
Katiba ni muhimu kwa watu wanaoweza kuwadhibiti viongozi na watumishi wa uma wanaoivunja katiba yenyewe, sheria, na kanuni kwa nia ya kupindisha haki.
 
Huu uhuni TCRA wamefundishwa na Polepole na dikteta uchwara..walitumia wahuni kutukana watu na TCRA ilikaa kimya kwa maelekezo ya akina Polepole..Japo TCRA wamefanya Jambo la kipuuzi.. lakini nafurahi kwakuwa mtego umempata aliyeutega..tuache yamkute..Tena angefungwa kabisa keko mpuuzi huyu..
 
Tanzania kuna drama..... nyingi sana especially kwenye siasa... wajinga wengi wamepewa nafasi adhimu ndani ya taasisi nyeti.., wao wanaendesha porojo na umbea bullshit....
 
hana impact yoyote. Wamemwacha tu
 
..Ila mkiambiwa Katiba Mpya mnaanza kurusha mateke..

Katiba ni muhimu ila kupata kiongozi alieimara ktk usimamizi wa hio katiba ni muhimu zaidi ya sana

Chadema kwenye katiba yao walikuwa na ukomo wa uongozi wa Mwenyekiti ila kutokana na kulewa madaraka kwa Mwenykt aliyepo basi ikafanyika figisu kipengele hicho cha ukomo kikaondolewa,,,

Tangu mwaka 2004 ( takribani miaka 17) mpaka leo hii bado Mbowe ni Mwenyekiti ilhali CCM ndani ya miaka hiyo ishapata wenyeviti WANNE tofauti

Sasa ni namna ya kushangaza kidogo, Mbowe ámbae haamini wenzake ktk kuwaachia madaraka ya uenyekiti chamani ndie anataka Watanzania wamuamini ktk kuichukua nchi mikononi mwa CCM
 
TCRA chini ya awamu ya tano ilikuwa na taratibu zake ndio maana hata wanaharakati huru wapuuzi walitukana wastaafu na wakaonekana wanafanya mema tu na kwa wakati huu awamu ya sita it play its rolls accordingly yapo mambo ambayo endapo yataachwa tu yaendelee ni hatari mno kwa tanzania yetu CONGRATULATIONS TCRA AWAMU YA SITA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…