Balozi Kombo: Wizara ya Mambo ya Nje sasa inaheshimiwa, si tena ya kupanga Viti

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabith Kombo, amesema kuwa taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inaheshimiwa na kushirikishwa katika uamuzi muhimu wa kitaifa na kimataifa, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilionekana kuwa ya kupanga viti tu.

Akizungumza Jumapili, Mei 11, 2025, katika uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuacha kuficha upungufu wao kazini, na badala yake wawe tayari kujifunza na kushirikiana ili kuimarisha ufanisi wa kazi.

“Taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Zamani watumishi wa wizara walionekana kama watu wa kupanga viti na kumkaribisha Rais sehemu anayokaa, lakini leo nina fahari kusema kwamba kila kikao muhimu nchini tunashiriki na tunashirikishwa. Hii inaonesha thamani ya mchango wa wizara yetu katika maendeleo ya Taifa,” amesema Balozi Kombo.

Amesisitiza kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, na kwa mantiki hiyo kila mmoja anapaswa kutambua upungufu wake na kuushughulikia kwa kujifunza kutoka kwa wenzake.

“Mara kadhaa nimekaa na Balozi Kilima, nikamwomba msaada kwenye eneo ambalo mimi mwenyewe sikusomea sana. Nimegundua kila mtu ana udhaifu wake, lakini ukiuficha huwezi kwenda mbele. Mimi sijawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika maisha yangu, siyo baba yangu, babu wala mjomba. Mimi ndiye wa kwanza katika familia. Kama nisingekubali kujifunza, tusingefika hapa,” ameongeza.

Balozi Kombo amesema hayo ikiwa ni miezi 10 na siku 10 tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo na amesisitiza umuhimu wa unyenyekevu na utayari wa kujifunza kama misingi ya mafanikio katika utumishi wa umma.

Akija mwengine atasema hivi sasa wizara yake inaheshimiwa sana na inatambulika kimataifa kuliko mtangulizi wake
 
Sasa mtu kama huyu ndio anawaelekeza mabalozi wa EU mini cha kufanya kweli,yeye mwenyewe bado mwanafunzi
 
Mmmmh kumkaribisha Rais sehemu ya kukaa? Mbona kama hii kauli imekaa kichuro
Maana yake walikua ni waandalizi tu na Sasa wana mchango mkubwa unao thaminiwa wa wizara ya mambo ya nje.
Kitu kikubwa amewakumbusha wote kua binaadamu ana mapungufu na ni muhimu kujifunza kwa wazoefu na amemtaja moja kati ya walio msaidia. Pia amewataka wafanyakazi wote wa wizara yake kuweka bidii katika kujifunza na kupata uzoefu.
Kumbuka hapa alikua hawapondi watangulizi kwake ila amezungumzia mapungufu ambayo hata yeye alikua nayo.
Mwana diplomasia anajitahidi vizuri sana
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabith Kombo, amesema kuwa taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inaheshimiwa na kushirikishwa katika uamuzi muhimu wa kitaifa na kimataifa, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilionekana kuwa ya kupanga viti tu.

Akizungumza Jumapili, Mei 11, 2025, katika uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuacha kuficha upungufu wao kazini, na badala yake wawe tayari kujifunza na kushirikiana ili kuimarisha ufanisi wa kazi.

“Taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Zamani watumishi wa wizara walionekana kama watu wa kupanga viti na kumkaribisha Rais sehemu anayokaa, lakini leo nina fahari kusema kwamba kila kikao muhimu nchini tunashiriki na tunashirikishwa. Hii inaonesha thamani ya mchango wa wizara yetu katika maendeleo ya Taifa,” amesema Balozi Kombo.

Amesisitiza kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, na kwa mantiki hiyo kila mmoja anapaswa kutambua upungufu wake na kuushughulikia kwa kujifunza kutoka kwa wenzake.

“Mara kadhaa nimekaa na Balozi Kilima, nikamwomba msaada kwenye eneo ambalo mimi mwenyewe sikusomea sana. Nimegundua kila mtu ana udhaifu wake, lakini ukiuficha huwezi kwenda mbele. Mimi sijawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika maisha yangu, siyo baba yangu, babu wala mjomba. Mimi ndiye wa kwanza katika familia. Kama nisingekubali kujifunza, tusingefika hapa,” ameongeza.

Balozi Kombo amesema hayo ikiwa ni miezi 10 na siku 10 tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo na amesisitiza umuhimu wa unyenyekevu na utayari wa kujifunza kama misingi ya mafanikio katika utumishi wa umma.

Okay sawa.
Je, waTanzania wamepata tija gani hasa kutoka katika Wizara hii?

Aidha, anapaswa ashughulikie matatizo yote ya Wizara hiyo kwa kuwa na Ofisi za Balozi zenye hadhi huko nje ya nchi. Ofisi nyingi za Balozi za Tanzania huko nje zimechoka vibaya sana mpaka zinatia aibu. Ni aibu kubwa sana ukiwa huko nje ya Tanzania kujitambulisha kuwa wewe ni mTanzania kutokana na Ubovu au ubaya wa Ofisi za Ubalozi wa Tz. Ni aibu kujitambulisha kwamba hii Ofisi ya Ubalozi wa nchi yangu.
 
Ta

Taja ofisi mojawapo.
 
Ta

Taja ofisi mojawapo.
Siyo kazi yangu,
Wana Maafisa wao huko. Wawaulize ili wapatiwe majibu, lakini hata wewe binafsi unaweza kuzitembelea Ofisi za Balozi za Tanzania huko nje ya nchi ili ujionee wewe mwenyewe kwa macho yako.
 
Aongee kwa takwimu..otherwise aache bra bra
 
Back
Top Bottom