Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Akija mwengine atasema hivi sasa wizara yake inaheshimiwa sana na inatambulika kimataifa kuliko mtangulizi wakeWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabith Kombo, amesema kuwa taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inaheshimiwa na kushirikishwa katika uamuzi muhimu wa kitaifa na kimataifa, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilionekana kuwa ya kupanga viti tu.
Akizungumza Jumapili, Mei 11, 2025, katika uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuacha kuficha upungufu wao kazini, na badala yake wawe tayari kujifunza na kushirikiana ili kuimarisha ufanisi wa kazi.
“Taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Zamani watumishi wa wizara walionekana kama watu wa kupanga viti na kumkaribisha Rais sehemu anayokaa, lakini leo nina fahari kusema kwamba kila kikao muhimu nchini tunashiriki na tunashirikishwa. Hii inaonesha thamani ya mchango wa wizara yetu katika maendeleo ya Taifa,” amesema Balozi Kombo.
Amesisitiza kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, na kwa mantiki hiyo kila mmoja anapaswa kutambua upungufu wake na kuushughulikia kwa kujifunza kutoka kwa wenzake.
“Mara kadhaa nimekaa na Balozi Kilima, nikamwomba msaada kwenye eneo ambalo mimi mwenyewe sikusomea sana. Nimegundua kila mtu ana udhaifu wake, lakini ukiuficha huwezi kwenda mbele. Mimi sijawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika maisha yangu, siyo baba yangu, babu wala mjomba. Mimi ndiye wa kwanza katika familia. Kama nisingekubali kujifunza, tusingefika hapa,” ameongeza.
Balozi Kombo amesema hayo ikiwa ni miezi 10 na siku 10 tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo na amesisitiza umuhimu wa unyenyekevu na utayari wa kujifunza kama misingi ya mafanikio katika utumishi wa umma.
Maana yake walikua ni waandalizi tu na Sasa wana mchango mkubwa unao thaminiwa wa wizara ya mambo ya nje.Mmmmh kumkaribisha Rais sehemu ya kukaa? Mbona kama hii kauli imekaa kichuro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabith Kombo, amesema kuwa taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inaheshimiwa na kushirikishwa katika uamuzi muhimu wa kitaifa na kimataifa, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilionekana kuwa ya kupanga viti tu.
Akizungumza Jumapili, Mei 11, 2025, katika uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuacha kuficha upungufu wao kazini, na badala yake wawe tayari kujifunza na kushirikiana ili kuimarisha ufanisi wa kazi.
“Taswira ya Wizara ya Mambo ya Nje imebadilika ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Zamani watumishi wa wizara walionekana kama watu wa kupanga viti na kumkaribisha Rais sehemu anayokaa, lakini leo nina fahari kusema kwamba kila kikao muhimu nchini tunashiriki na tunashirikishwa. Hii inaonesha thamani ya mchango wa wizara yetu katika maendeleo ya Taifa,” amesema Balozi Kombo.
Amesisitiza kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, na kwa mantiki hiyo kila mmoja anapaswa kutambua upungufu wake na kuushughulikia kwa kujifunza kutoka kwa wenzake.
“Mara kadhaa nimekaa na Balozi Kilima, nikamwomba msaada kwenye eneo ambalo mimi mwenyewe sikusomea sana. Nimegundua kila mtu ana udhaifu wake, lakini ukiuficha huwezi kwenda mbele. Mimi sijawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika maisha yangu, siyo baba yangu, babu wala mjomba. Mimi ndiye wa kwanza katika familia. Kama nisingekubali kujifunza, tusingefika hapa,” ameongeza.
Balozi Kombo amesema hayo ikiwa ni miezi 10 na siku 10 tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo na amesisitiza umuhimu wa unyenyekevu na utayari wa kujifunza kama misingi ya mafanikio katika utumishi wa umma.
Taja ofisi mojawapo.Okay sawa.
Je, waTanzania wamepata tija gani hasa kutoka katika Wizara hii?
Aidha, anapaswa ashughulikie matatizo yote ya Wizara hiyo kwa kuwa na Ofisi za Balozi zenye hadhi huko nje ya nchi. Ofisi nyingi za Balozi za Tanzania huko nje zimechoka vibaya sana mpaka zinatia aibu. Ni aibu kubwa sana ukiwa huko nje ya Tanzania kujitambulisha kuwa wewe ni mTanzania kutokana na Ubovu au ubaya wa Ofisi za Ubalozi wa Tz. Ni aibu kujitambulisha kwamba hii Ofisi ya Ubalozi wa nchi yangu.
Siyo kazi yangu,Ta
Taja ofisi mojawapo.