Balozi kumi zaitakia kila la kheri Tanzania kuelekea Uchaguzi

Balozi kumi zaitakia kila la kheri Tanzania kuelekea Uchaguzi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
1599065792966.png


Wakuu wa Balozi za nchi ya Ubelgiji, Canada, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Netherlands, Norway, Sweden na Uswizi zilizoko kwa pamoja zimeitakia Tanzania uchaguzi mwema

Katika tamko hilo la pamoja, wameonyesha kuwa wanatumaini Uchaguzi utauwa wa huru na wa haki utakaoruhusu kila mtu kushiriki katika kuchagua viongozi wa nafasi mbalimbali za kisiasa

Katika kauli yao wamesema kwa pamoja wako tayari kushirikiana katika kukuza demokrasia nchini Tanzania. Wamesisitiza uwazi kuwepo kwenye namna ambavyo vyombo vya habari vya ndani na vya nje vitakavyoruhusiwa kushiriki

Wamewataka wadau wote kuhakikisha mazingira salama ya uchaguzi kwa wagombea wote, na kuheshimu utawala wa sheria. Kama mabalozi wamesema watasaidia hatua zote za kukuza demokrasia nchini Tanzania
 
Ni ujumbe uliojificha kuwa wanafuatilia, wengine hapo walitegemea Lissu hatapewa nafasi.
 
Mbona haya maneno chaguzi zote zilizopita yalitolewa,hakuna jipya hapo ni kama kuteleza tu kwenye kuti la mnazi.
 
Kila wakati wa uchaguzi tumekuwa tukitakiwa kila la heri na kukumbushwa kuheshimu demokrasia. Kuna tatizo safari hii?

Si wawatakie na ndugu zao Marekani...ambako Hadi vituo vya police vinachomwa moto tujue wanajali kwelikweli?
 
Si wawatakie na ndugu zao Marekani...ambako Hadi vituo vya police vinachomwa moto tujue wanajali kwelikweli?
Hata ss tukipenda tutawatakia kila la heri na hao marekani wakiwemo. Ni ustaarabu tu wa kawaida kutakiana uchaguzi mwema na kukumbushana kutunza amani.
 
Back
Top Bottom