Balozi Mpoki Ulisubisya: Dudubaya anachosema ni Mapambio na Anapaswa kuwa Mzalendo

Balozi Mpoki Ulisubisya: Dudubaya anachosema ni Mapambio na Anapaswa kuwa Mzalendo

D

DeletedMember281674

Guest
Nipo kwenye ziara ya Waziri wa AFYA - Mh. Mohammed Mchengerwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala muda huu saa 7 Mchana.

Katika ziara hii, Katibu Mkuu - Wizara ya Afya kamkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MOI Balozi Dr. Mpoki Ulisubya aweze kutoa ufafanuzi kuhusiana na vifaa vya MRI na CT-SCAN katika Hali ya kushangaza Balozi huyu ambaye kitaaluma ni Daktari anadai Kwamba Yale yaliyozungumzwa na Dudubaya eti ni Mapambio na Dudubaya anapaswa kuwa Mzalendo.

Mbaya zaidi analinganisha Mashine za MRI za MOI ni sawa na gari aina ya IST na zile za India ni Discovery ndiyo maana zinatoa kelele Sana.

Na zaidi huyu Balozi Dr. Mpoki anaiomba Serikali kupitia Katibu Mkuu wa AFYA amsaidie kununua Mashine za MRI zisizopoliga kelele yaani Silent MRI, kwa majibu yake yaliyojaa mipasho na dharau bila kujali afya za watanzania huyu anapaswa kutumbuliwa.

Kwako Dudubaya kuwa makini unapoenda kutibiwa katika hizi Hospitali za Umma, wasije wakakupiga sindano ya simu ukafa. Shauri Yako Dudubaya, Mwanakulitafuta ni Mwanakulipata wewe umeshaonekana siyo Mzalendo wa nchi hii.

Nawasilisha

Pia soma: Kwa maelezo haya ya Dudu Baya ukiwa na hela bora ukatibiwe India

Na

 
Dudubaya kwa muda huu akitaka kuwa mjumbe wa kamati kuu CHADEMA anakuwa bila shida yoyote. Kwa sasa ni shujaa huko CHADEMA.
 
Hii inji ina tafsiri zake za maneno sijui kwa hapa inji hii yenyewe ina tafsiri vipi neno UZALENDO??

maana hata neno Taifa tafsiri ya hapa ni tofauti,ukisikia kwa maslahi ya Taifa ina maana tofauti kqbisa na unayoijua.
 
Dudubaya kwa muda huu akitaka kuwa mjumbe wa kamati kuu CHADEMA anakuwa bila shida yoyote. Kwa sasa ni shujaa huko CHADEMA.
Dudubaya ni shujaa wa Tanzania wewe juha, maana kwa kupaza kwake sauti, serikali yenu haramu imeanza mchakato wa kupata MRI bora zaidi.
 
Back
Top Bottom